Header Ads Widget

Responsive Advertisement

WANAWAKE TUMIENI FURSA NA UWEZESHWAJI KIUCHUMI, ACHANENI NA KAUSHA DAMU


 

Na. WAF, Dodoma


Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anna Makinda ametoa wito kwa Wanawake nchini kuhakikisha wanatumia kikamilifu fursa za uwezeshaji kiuchumi na mikopo yenye riba na masharti nafuu ili waweze kufikia lengo la kujiinua kiuchumi.


Mhe. Makinda ameyasema hayo Machi 03, 2025 wakati akizungumza katika kongamano la kanda ya kati inayojumuisha mikoa ya Dodoma, Singida na Iringa kuelekea kilele cha siku ya Wanawake Dunia, lililofanyika jijini Dodoma.


“Niwasisitize wanawake wote kuhakikisha mikopo inayotolewa kwnu iwe yenye tija na na sio ile ya kausha damu, kila mkoa una fursa hawa wakuu wa mikoa wanafahamu mengi hivyo acha kukata tamaa na kusikitika nendeni kwenye mabanki msiogope kwa sababu huko kwenye mabanki pia mtafundishwa kulingana na biashara unayotoka kufanya,” amesisitiza Mhe. Makinda 

 

Amesema Serikali inatengeneza program ya kitaifa ya kizazi chenye usawa ya mwaka 2021/2026 ambayo imejikita kutoa msukumu wa masuala ya uwezeshaji kwa kuhakikisha inakuza haki na fursa za kiuchumi hii ni kutokana na umuhimu kwamba mwanamke akiimarika kiuchumi ni nyenzo muhimu kwake katika kumpatia uwezo wa kugombea nafasi za uongozi.


Aidha, Mhe. Makinda ametoa rai kwa wanawake waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali kuwashika mkono wanawake wengine ili kwapamoja waweze kuinuka kwa ustawi na maendeleo ya familia na Taifa kwa ujumla.


“Waliopata nafasi na kufanikiwa kama sisi inabidi tushirikiane nanyi ili kuwaeleza ni changamoto na njia gani tumepitia nakufika katika nyanja za uongozi n ahata kibiashara ili muweze kupata moyo wa Kwenda mbele zaidi,” amesema Mhe. Makinda.


Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita (6) imeendelea kuona umuhimu wa wanawake katika jamii na ndio maana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amepeleka madaktari Bingwa kwa jamii kwa lengo la kujali hasa wanawake na Watoto.


Awali, akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewataka wanawake wenye sifa kujitokeza kugombea nafasi za udiwani na ubunge kwenye uchaguzi wa mwaka 2025.


“Takwimu za uongozi kwa mkoa wa Dodoma zinaonyesha asilimia 71 ya wakuu wa wilaya ni wanawake ambapo katika wilaya saba za mkoa wetu wakuu wa wa wilaya wanaume ni wawili na wanawake ni watano na wanafanya vizuri, na kwa wabunge asilimia 11 ni wanawake, kwa hili linaonyesha nafasi za kuteuliwa ni wengi kulikuto nafasi za kuchaguliwa hivyo nitoe rai kwa wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi,” amesema Mhe. Senyamule

Post a Comment

0 Comments