......................
Serikali imeonya watu wote wasio na utalaam kujiepusha kutoa taarifa za afya huku wakijua hawana weledi au taaluma ya kufanya hivyo.
Imesema hatua kali za Sheria zitachukuliwa dhidi ya mtu yoyote atakayetoa na kusambaza taarifa zinazopotosha jamii na kufifisha juhudi za Serikali na wadau katika kupambana na maambukizi ya Virusi Vinavyosababisha Ugonjwa wa Ukimwi (VVU).
Taarifa ya Wizara ya Afya iliyosainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Roida Andusamile ilisema imeona taarifa ya video inayosambaa katika mitandao ya kijamii wa Instagram inayoonyesha mtu anayejitambulisha kuwa anaishi na virusi vya Ukimwi kwa jina la Mentor Chery and wellbeinghub akitoa taarifa kuwa dalili mojawapo ya kuwa na virusi hivyo ni mtu kuwa na vidoti vyeusi katika dole gumba la mguu hadi kisigino.
"Mtu huyo ameenda mbali zaidi na kuiasa jamii hasa walio katika uhusiano wachunguze wenzi wao wasiojua hali zao za maambukizi ya Virusi hivyo na endapo watabaini hayo ni wazi kuwa wenzi hao wameathirika kwa kuwa wenye ugonjwa huo nyao.zao haziwi nyeupe," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, taarifa hiyo inapotosha jamii. Ukweli ni kwamba huwezi kumtambua muathiriia wa Virusi vinavyosababisha Ukimwi kwa kumuangalia kwa macho au kwa kuangalia baadhi ya dalili zilizoelezwa katika video hiyo. Badala yake njia pekee ya kumtambua hali ya anayeishi na virusi hivyo ni kwa kufanya vipimo kwa mujibu wa miongozo iliyopo

0 comments:
Chapisha Maoni