JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Sports. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Sports. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 20 Machi 2025

UKOROFI WAMPONZA SERGIO RAMOS WAMEXICO WAMJIA JUU

  Mkongwe wa timu ya Taifa ya Hispania Sergio Ramos mwenye rekodi za kipekee Ulaya na Duniani  amejikuta katikati ya utata baada ya mechi ya hivi majuzi huko Mexico. Nyota huyo anayekipiga Monterrey  aliwekwa kikaangoni na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka la Mexico na kuthibitisha rasmi kumfungia Ramos, kwa kukiri makosa makubwa ya mwamuzi wakati wa mchezo.


. Tukio hilo lilitokea katika dakika ya 20 wakati Ramos alipopiga teke la kizembe lililoelekezwa kwa mshambuliaji Guillermo Martínez.Ugomvi huo ulipelekea  machafuko katika mchezo na  tukio hilo limesababisha mzozo kutoka kwa viongozi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kocha mkuu wa Pumas Efraín Juárez.

 Juárez alionyesha kutoridhika kwake, akisisitiza kwamba Ramos hakupaswa kuruhusiwa kusalia uwanjani kwa zaidi ya dakika 70 baada ya kumzonga mlinzi Pablo Bennevendo. Hali hii inazua maswali kuhusu uthabiti wa wasimamizi wa ligi na viwango vinavyotarajiwa vya mwenendo wa wachezaji. 

Wakati jumuiya ya soka ikifuatilia kwa makini, vitendo vya Ramos na maamuzi yatakayofuata ya waamuzi bila shaka yataibua mjadala juu ya hitaji la uwajibikaji katika mchezo huo, na kuhakikisha kuwa matukio kama hayo yanashughulikiwa kwa haraka na kwa ufanisi. Athari za hali hii zinaenea zaidi ya Ramos pekee, na kuathiri mitazamo ya usalama wa wachezaji na uadilifu wa mchezo wenyewe.

Ijumaa, 1 Novemba 2024

MASHUJAA FC VS SIMBA SC NANI KUIBUKA NA ALAMA 3?


Kama ilivyo kuwa desturi ya shujaa lazima aibuke shujaa kwenye kila kitu, 

Kuelekea mchezo wa leo Mashujaa Fc  @mashujaafcofficial  akiwa nyumbani akimkaribisha mnyama simba mwanalunyasi @simbasctanzania 


Je, Mashujaa Fc watalitendea haki jina la Mashujaa na kuibuka kidedea kubeba alama 3, ?


Je, Simba Sc ataweza kufurikuta mbele ya mashujaa hawa? 

Au ndokusema ataziokota alama zake tatu kiulaini?


Ni upi mtazamo wako kuelekea pambano hili leo hii ifikapo saa 10;00 jioni.


Vipi kuhusu correct score, unaweza kuwa ngapi ngapi kwa dakika 90 za mchezo huu.

 

Alhamisi, 8 Agosti 2024

"Najivunia kuwa mwanamke licha ya huu muonekano wangu" Loveness (Stanley Tarimo )

 

"Ndoto yangu kubwa ilikuwa kuwa mchezaji mpira lakini ilikwama kipindi ambacho wazazi hawakuelewa kuwa kuna haja ya kuendeleza vipaji,walikasirika kila nilipotoka shule na kiatu kimeharibika kwa sababu ya kucheza mpira wakati mimi ni binti, kwanini nicheze mpira’’

Loveness Stanley Tarimo 38 ,anasema anapenda kutambulika kama mwanamke wa kawaida kabisa anayejipenda na asiye na majivuno. Muonekano wake haumbadilishi jinsia yake na anajivunia kuwa alivyo.

Loveness amezaliwa katika familia ya watoto wa kike watatu na mmoja wa kiume huko mkoani Kilimanjaro.

‘’Mimi nimetokea kwenye familia ya kawaida ya kikristo kabisa ya wacha Mungu,ingawa mimi ninaonekana kama niko tofauti kidogo,’’anaeleza Loveness huku akicheka.

Nilipokuwa mtoto nilichukia kuitwa 'jike dume'

Baada ya kumaliza darasa la saba katika shule ya msingi Kijenge, Arusha Loveness hakubahatika kuendelea na masomo ya sekondari kwa kushindwa kupata ufaulu mzuri na wazazi hawakuwa na uwezo wa kumuendeleza katika shule za kulipia.

Hivyo aliamua kujikita zaidi kwenye michezo jambo alilofurahia sana katika kipindi chote.

Ingawa mazingira ya mpira wa miguu yakiwa ya chini sana kwa upande wake aliamua kuachana na mchezo huo kwani haukumlipa akaamua kujiunga na kujifunza mazoezi ya kujenga mwili.

‘’Maisha ya shule yalikuwa mazuri sana kwangu muda mwingi nilipenda kucheza mpira. Watoto wenzangu walinishangaa kwanini kila mara nilipokwenda uwanjani nilivaa sketi ya shule na kaptura kwa ndani ili nicheze mpira kwa uhuru’’anaeleza akitabasamu

Loveness anasema zipo nyakati hakufurahia wakati wa utoto wake akieleza namna baadhi ya wanafunzi walivyokuwa wakimtania kwa kumuita majina kama 'Tomboy' au jike dume kwa sababu tu alipenda kuongozana na wavulana, "Nilikuwa nikiitwa hivyo ninaenda chumbani ninalia".

‘’Hata nikihitaji kitu sasa hivi siwezi kuomba msichana,ni rahisi sana kumuomba mwanaume kuliko mwanamke."

Pamoja na kuwa tofauti kwa muonekano wa jamii, anajivunia kuwa hakuwahi kuwavunjia heshima wazazi wake, na wanajivunia kuwa na mtoto kama yeye.

Loveness anasema haikuwa rahisi kujenga mwili kuwa na misuli namna hii.

Ni takribani miaka 10 sasa tangu alipoanza kufanya mazoezi ya kujenga misuli,na sasa anafurahia muonekano wake kwani unampa utofauti na wanawake wengine,anajisikia mrembo zaidi.

Anasikitishwa na namna baadhi ya watu wasivyomtathmini na kumpa majina kama Tom boy na mtu ambaye amekataa jinsi yake, anasema inamshangaza haelewi tatizo nini.

‘’Kipindi cha nyuma kweli ilinisumbua lakini sasa hivi ninazidi kupenda nilivyo kwani hakuna kitu kizuri kama kujikubali.

Kwa maisha ya sasa hivi ukisema uhangaike na kila mtu ili akuelewe utasumbuka sana. Siwezi kuwalazimisha watu kunielewa nimeachana nao".

Muonekano wake umempa fursa ya kujiingizia kipato kwa kutoa mafunzo kwa watu mbalimbali ambao wamekuwa wakimfikia na kuwafundisha.

‘’Namshukuru Mungu nimekuwa nikipata sana wateja ambao wengi ni wanawake kidogo imeniongezea kipato’’

Idadi ya walimu wa mazoezi wa kike kuwa ndogo, kwa Loveness imekuwa fursa, "Wateja wangu wengi wa kuwafundisha mazoezi ni wanawake waislamu, wahindi na waarabu kwasababu ya imani yao wanaona ni bora wanichague mimi mwanamke kuliko kufundishwa na mwanaume. Wameshaniamini mimi ni jinsi ya kike na muonekano wangu hauwapi wasiwasi wowote, "Loveness anaeleza.

Loveness anasema ‘’Unajua wenzetu kidogo haiwasumbui kwani michezo hii ya wanawake kuwa na misuli mikubwa kwao ipo,lakini kwa hasa watanzania kushangaa nawaelewa tu’’

Yanga yatamba kuendeleza Ubabe, Simba yajiandaa kisaikolojia ( Unatabili Kwenye Kariakoo derby ya leo 8.8.2024 )

 



Mtaani raia husema, ‘ni noma sana’ , sasa ni hivi..! Pambano la watani wa jadi nchini Tanzania kati ya Simba na Yanga lazima lipate mshindi.

Bila shaka huzuni na butwaa litawakumba mashabiki wa timu moja kati hizo mbili kongwe za Afrika Mashariki kwani timu moja itatakiwa kushiriki fainali ya Ngao ya Jamii.

Timu hizo kubwa na kongwe zinazobeba taswira ya soka la Tanzania na Afrika Mashariki, zitavaana majira ya saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam

Pambano lingine nusu fainali litawakutanisha matajiri wa jiji la Dar es Salaam, Azam FC dhidi ya Coastal Union katika dimba la New Amaan Complex kule visiwani Zanzibar.

Kuelekea mchezo huo, mashabiki wa Yanga wanatamba kuwa kikosi chao kiko kwenye kiwango cha juu kikiongezewa nguvu na wachezaji mastaa wanaolijua vyema soka la Bongo, Clatous Chama (Mzambia) , Duke Abuya ( Mkenya) , Prince Dube (Zimbabwe) na Jean Baleke (Mkongomani) hivyo hivyo wanatamba kuendeleza ubabe wao kwa kuifunga Simba kama walivyofanya msimu uliopita, walipoifunga mara mbili kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwemo 5-1 kwenye mchezo wa Ligi.

Kwa upande wa wanachama na mashabiki wa Simba nao wameonekana kuwa na matumaini mapya, hasa baada ya kufanya usajili mkubwa wa wachezaji kutoka Ivory Coast, Zambia, Nigeria, Guinea, Burkina Faso na sehemu mbalimbali.

Wachezaji kama Valentin Nouma Joshua Mutale, Debora Fernandes, Jean Ahoua, Augustine Okejepha, Awesu Awesu, na wengineo wameanza kuwapa kiburi mashabiki wa Simba ambao wamesema wanaweza kupata ushindi, lakini hata kama watapoteza mechi hiyo, haitokuwa kizembe kama walivyochapwa mabao 5-1 msimu uliopita.


Jumatano, 7 Agosti 2024

FILBERT BAYI NDANI YA JUMBA LA WANARIADHA NGULI (LEGENDS) DUNIANI NCHINI UFARANSA

 

Filbert Bayi katika akiwa na picha yake itakayowekwa kwenye makumbusho hayo wakati wa hafla  maalumu ya Shirikisho la Riadha la Dunia (World Athletics - WA) lililofanyika Jumanne usiku Agosti 6, 2024  ya kumjumuiisha rasmi mwanariadha huyo nyota waTanzania Filbert Bayi kwenye makumbusho ya wanariadha nguli (legends) duniani (MOWA)  ya shirikisho hilo yaliyoko mjini Monaco, Ufaransa 


Shirikisho la Riadha la Dunia (World Athletics - WA) mnamo Jumanne usiku Agosti 6, 2024 liliandaa hafla ya tatu ya Museum of the World Athletics (MOWA) ambapo mwanariadha nyota waTanzania Filbert Bayi alijumuishwa rasmi kwenye jumba la makumbusho ya wanariadha nguli (legends) duniani ya shirikisho hilo.

- Kwa Kiingereza; ‘Filbert Bayi has been indicted in the Hall of Fame of World Athletics in the MOWA.

Hafla hiyo, iliyoandaliwa na Rais wa Shirikisho hilo Lord Sebastian Coe, imefanyika ukumbi wa Monnaie de Paris Museum, jijii Paris kama sehemu ya Michezo ya Olympic ya Paris 2024 kwa heshima ya Bayi kwa kushikilia rekodi mbili za riadha za dunia, ambazo zimeorodheshwa katika Makumbusho ya MOWA yaliyoko mjini Monaco nchini Ufaransa.

Lord Sebastian Coe, ambaye ni bingwa wa dunia wa mbio za kati wa zamani, tayari alishatangaza kujumuishwa kwa Bayi katika MOWA kabla ya uzinduzi wa makumbusho hayo Machi 11, 2021 mjini Monaco, ambapo Bayi alikuwa ni mmoja wa nyota wa riadha dunia walioalikwa kuhudhuria hafla ya uzinduzi huo.

Filbert Bayi, ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki ya Tanzania (TOC), amepewa heshima hiyo kwa kuwa mmoja wa wanariadha nyota  waliovunja rekodi mbili za dunia wakati huo jambo ambalo halikuwa rahisi kutokana na ushindani mkali uliokuwapo pamoja na wanariadha hodari.

Mafanikio makubwa zaidi ya Bayi yanatajwa kuwa kwenye  fainali ya mita 1500 katika Michezo ya Jumuiya ya Madola ya 1974 huko Christchurch, New Zealand, aliposhinda medali ya dhahabu mbele ya mwanariadha wa New Zealand John Walker na Mkenya Ben Jipcho.

Katika ushindi huo, Bayi aliweka rekodi mpya ya dunia ya dakika 3 32.16 s, iliyoidhinishwa na IAAF kama 3:32.2, na Walker akaenda chini ya rekodi ya zamani ya dunia iliyowekwa na Mmarekani Jim Ryun.

Mchuano huo wa Bayi na John walker hadi leo unatajwa kama moja ya mbio kubwa zaidi za 1500 m wakati wote.

Baada ya Bayi kuweka rekodi hiyo ya dunia ya mita 1500 mwaka 1974, mwaka mmoja baadaye (1975)  katika Mashindano ya ‘Dream Mile’ huko Kingston Jamaica akavunja rekodi ya maili moja iliyokuwa inashikliliwa na huyo huyo Jim Ryun.

Bayi pia alivunja rekodi ingine ya kuwa mmiliki kwa muda wa miaka 48 wa rekodi ya ubingwa wa 1500m ya Michezo ya Jumuiya ya Madola ambayo hatimaye ilikuja kuvunjwa mwaka 2022 kwenye michezo hiyo huko Birmingham, Uingereza.

Kwenye michezo hiyo ya Birmingham Bayi ndiye aliyepewa heshima ya kumvalisha medali ya dhahabu Ollie Hoare wa Australia aliyeshinda na kuvunja rekodi yake ya dakika 3:32.2 wa kutumia dakika 3:30.12

Mafanikio mengine ya Bayi yalikuwa Katika michezo ya Olympic ya Moiscow Urusi mwaka 1980 ambapo alishinda fedha katika mita 3,000 kuruka vikwazo (Steeple Chase).


Filbert Bayi akiwa na Kutoka Kushoto: Marc Schwartz, Mwenyekiti & Mkurugenzi Mtendaji wa Monnaie de Paris Museum, Lord Sebastian Coe na  Billy Mills (USA) mshindi wa 1964 Tokyo Olimpiki mbio za mita 10000. 

Filbert Bayi akiwa na Rais wa Shirikisho la Riadha Duniani  (World Athletics - WA) Lord Sebastian Coe wakati wa  hafla  maalumu ya Shirikisho hilo lililofanyika Jumanne usiku Agosti 6, 2024  ya kumjumuiisha rasmi mwanariadha huyo nyota waTanzania Filbert Bayi kwenye makumbusho ya wanariadha nguli (legends) duniani (MOWA)  ya shirikisho hilo yaliyoko mjini Monaco, Ufaransa 

"Malengo Yangu ni ushindi mfululizo katika mbio kwenye michezo ya Olimpiki 2024" Kipchoge

 

Eliud Kipchoge, Mkenya anayetaka kuweka jina lake katika vitabu vya historia ya michezo ya kukimbia kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris, Tarehe 10 Agosti mkimbiaji huyo mwenye umri wa miaka 39, atatafuta nafasi ya kuwa mtu wa kwanza kushinda mara matatu mfululizo katika mbio za marathoni katika michezo ya Olimpiki.

Atapambana na wakimbiaji wachanga, lakini pia atakuwa na changamoto nyingine ya kupambana na hali ya hewa. Joto katika mji mkuu wa Ufaransa ni kali, na huongezeka hadi nyuzi joto 30.

“Mashindano yatakuwa magumu sana – karibu 40% ni milima – na nadhani joto litachangia ugumu,” ameviambia vyombo vya habari.

Kutoka mwinuko wa kuanzia wa mita 36 kutoka usawa wa bahari katikati mwa jiji, njia hiyo itapanda hadi mita 183 kwenye barabara ya Versailles, kuelekea mwinuko wa pili mkali wa mita 172 kabla ya kuifikia alama ya kilomita 30 wakati wakimbiaji wanaporejea Paris. .

Mashindano yataanza saa 02:00 asubuhi kwa saa za Ufaransa, na Kipchoge amebadilisha mfumo wake wa mazoezi katika kituo chake cha Kaptagat katika jitihada za kuongeza medali nyingine ya dhahabu, mbali na zile za Rio, Brazil 2016 na Tokyo, Japan 2020. 

“Nitaweka akilini mwangu kuhusu ukimbiaji wa milimani na katika joto kali ili kuufanya mwili wangu umudu kuelekea mashindano ya Paris,” alielezea katika mahojiano wakati wa maandalizi yake.

“Wakati mwingine hufanya mazoezi saa nne asubuhi, tano ili kuhisi joto hilo. Lakini katika Olimpiki hatuzingatii muda.”

Wanazi wa Mashujaa FC Kigoma waonesha balaa

 

Hivi ndivyo hali inayoendelea Mkoani Kigoma kwa Mashabiki wa soka Mashujaa FC wakiendelea na hamasa ambapo wametangaza tarehe 10 August 2024 kuwa kilele cha wiki ya Mashujaa Day kuelekea msimu ujao.

Ni utamaduni wa vilabu kadhaa Tanzania bara kuwa na matamasha maalumu ambayo hutumiwa kutambulisha wachezaji wapya na kuhitimishwa kwa kucheza mchezo wa kirafiki ambapo kwa Mashujaa FC watacheza na timu kutoka nchi ya Burundi.

Utambulisho wa kikosi cha Mashujaa FC kuelekea msimu wa 2024/2025 utaambatana na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa Mkoa wa Kigoma na hatimaye mchezo wa kirafiki ambao utawafanya mashabiki wa Mashujaa FC kushuhudia kiwango cha kusakata kabumbu kutoka kwa kikosi kipya katika Uwanja wa Lake Tanganyika.

Kwa mujibu wa takwimu zilizowahi kutolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Timu ya Mashujaa FC, yenye maskani yake mjini Kigoma, ilishika nafasi ya tatu kwa kuingiza mashabiki,Maahujaa ikiingiza mashabiki 45,638, huku Tabora United ikiwa nafasi ya nne, ikikusanya 43,808 na Azam FC, imekuwa ya tano ikiingiza jumla ya mashabiki 35,379.

Jumamosi, 3 Agosti 2024

Dondoo Za Soka La Ulaya Kwenye Sajili Za Wachezaji

 

Tottenham hawana nia ya kumsajili Federico Chiesa, 26, kutoka Juventus licha ya ripoti kuwahusisha na mshambuliaji huyo wa Italia. (Football Insider)

Aston Villa wametoa dau rasmi kwa Sunderland kumnunua mshambuliaji wa umri wa miaka 17 Mason Cotcher. (Fabrizio Romano)

Manchester City wamekubali kumuuza mlinzi wa Finland Tomas Galvez, 19 kwa mkopo kwa mabingwa wa Austria LASK. (Teamtalk)


Inter Milan wameungana na West Ham katika mbio za kutaka kumsajili beki wa kulia Mwingereza Aaron Wan-Bissaka kutoka Manchester United, 26. (Football Insider)

Bournemouth wanamfikiria mshambuliaji wa Aston Villa Muingereza Cameron Archer, 22, kama mbadala wake iwapo mchezaji Dominic Solanke, 26, atauzwa kwa Tottenham. (Football.London)

QPR na Celtic wako katika mbio za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Liverpool mwenye umri wa miaka 21 Owen Beck. (Sky Sports)

Arsenal wanamtaka mshambuliaji wa Brighton wa Brazil Joao Pedro, 22. Football Transfers)

Fulham wanavutiwa na beki wa Aston Villa Mbrazil Diego Carlos, 31. (Mail)

West Ham wako katika mpango wa kumsajili kiungo wa Argentina Guido Rodriguez, 30, kama mchezaji huru baada ya kuondoka Real Betis. (Standard)

Mlinzi wa Villarreal Mhispania Jorge Cuenca, 24, anatazamiwa kujiunga na Fulham. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Rennes Desire Doue, 19, anapendelea kuhamia Bayern Munich kuliko kusalia katika nchi yake ya asili ya Ufaransa na Paris St-Germain. (Sky Germany)


Bayern Munich imekataa dau la Manchester United mara mbili kwa mlinzi wa kati wa Uholanzi Matthijs de Ligt, 24, na beki wa Morocco, Noussair Mazraoui, 26. (Telegraph - subscription required)

Newcastle wanapanga kuanzisha mazungumzo kuhusu mkataba mpya na winga wa Uingereza Anthony Gordon, 23, atakaporejea kutoka mapumzikoni baada ya mashindano ya Euro 2024. (Athletic - subscription required)



Mashabiki wa Simba Wilayani Mkalama wameadhimisha Simba Day kwa kutoa msaada katika hospitali ya Wilaya pamoja na shule ya sekondari Nduguti.

 

Mashabiki wa Simba Wilayani Mkalama leo Agosti 3,2024 wameadhimisha Simba Day kwa kutoa msaada katika hospitali ya Wilaya pamoja na shule ya sekondari Nduguti.

Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo, kiongozi wa mashabiki wa Simba wilayani Mkalama, Bwana Tesha Daniel amewaomba wananchi Mkalama kuwa na tabia ya kujitolea katika matukio ya kijamii kwa kutoa msaada mbalimbali kwa watu wenye uhutaji kwa lengo la kujenga jamii yenye upendo na amani.

"Tuifanye dunia kuwa sehemu salama, tunawajibu wa kujitolea pale inapobidi kwa ajilii ya kuleta tabasamu kwa ndugu zetu, niwaombe tuwe na desturi kama hii ya kuitika pale tunapoitwa kwa ajili ya wengine" Tesha 

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nduguti, Rosemary Richard ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha Nne amewashukuru mashabiki wa Simba kwa upendo wao na kuwaomba wananchi wilayani Mkalama kuiga mfano wa mashabiki hao wa Simba. 


Vifaa vilivyotolewa na mashabiki wa Simba leo katika wodi ya wazazi ya hospitali ya Wilaya ni pamoja na Sabuni, Sukari na kwa upande wa shule ya sekondari Nduguti mashabiki hawa wametoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wakike  pamoja na sabuni kwa wanafunzi wa kiume



Morocco na Misri zatinga nusu fainali Kwenye Mashindano ya soka ya Olimpiki 2024

 

Afrika itakuwa walau na medali moja katika mashindano ya soka ya Olimpiki ya wanaume baada ya Misri na Morocco zote kutinga nne bora.

Morocco ilianza na mafanikio maradufu kwa ushindi murua wa 4-0 dhidi ya Marekani kwenye uwanja wa Parc des Princes mjini Paris.

Mkwaju wa penalti kipindi cha kwanza wa Soufiane Rahimi - bao lake la tano kwenye michuano hiyo - uliipa Atlas Lions fursa ya kuongoza hadi wakati wa mapumziko.

Lakini katika kipindi cha pili ambacho kilionekana kuwa na bahati ya mtende kwao, Ilias Akhomach, nahodha Achraf Hakimi na penalti nyingine iliyofungwa na Mehdi Maouhoub ilimalizia mambo kwa mtindo wa kipekee.

Katika marudio ya mechi ya hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia la Qatar 2022, Morocco sasa itamenyana na Uhispania mjini Marseille Jumatatu (16:00 GMT) kuwania nafasi ya kutinga fainali.

Baada ya mechi hiyo, Hakimi alisifu uungwaji mkono mkubwa wa Morocco ambao umeisaidia timu hiyo nchini Ufaransa.

"Mashabiki wamekuwa wakitufuatilia katika mashindano yote," alisema mlinzi huyo ambaye anachezea soka uwanja wa Parc des Princes klabu la Paris St Germain.

"Natumai wanaweza kutufuata hadi fainali. Tunataka kuwafanya wawe na fahari."

Joshua Cheptegei wa Uganda ajishindia medali ya dhahabu Katika Mashindano ya Olimpiki 2024

 

Joshua Cheptegei wa Uganda ameshinda mbio za mita 10,000 kwa wanaume - medali ya kwanza kupatikana katika riadha na kuipatia Afrika dhahabu yake ya pili katika mashindano ya Olimpiki ya Paris, 2024.

Cheptegei, mshikilizi wa rekodi ya dunia wa Uganda, alitoka mbio za kufa mtu katika raundi ya mwisho na kuweka rekodi mpya ya saa 26:43.14 akitia kibindoni medali ya dhahabu ya kwanza uwanjani Stade de France.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 27, na bingwa wa dunia mara tatu, alimaliza mbele ya Berihu Aregawi wa Ethiopia na mshindi wa medali ya shaba Grant Fisher, wa Marekani.

Jumanne, 30 Julai 2024

Mchezaji wa Benfica anayevutia klabu kuu za Ulaya

 

Ikiwa klabu yako itakuwekea kipengele cha kuachiliwa cha zaidi ya £100m, kwa kawaida ni ishara kuwa wewe ni mchezaji maalum. Hiyo inaweza kuwa hivyo kwa mchezaji Joao Neves, kiungo wa kati wa Benfica ambaye anatarajiwa kuhamia klabu kubwa msimu huu.


Neves, 19, ameripotiwa kuvutiwa na Manchester United na Arsenal, lakini ni Paris St-Germain ambayo inazungumziwa kuwa klabu anayoelekea kujiunga nayo zaidi.


Kijana huyo tayari ameisaidia klabu yake ya utotoni kutwaa taji la ligi na kucheza michuano ya Uropa kabla ya kufikisha miaka 20.


Je, Neves atafuata nyayo za wachezaji maarufu kama vile Bernardo Silva, Ruben Dias na Enzo Fernandez na kuwa mchezaji anayelekea kujiunga na klabu kubwa kutoka Lisbon?

Chanzo BBC Swahili

Jumatatu, 29 Julai 2024

ALLY KAMWE ATANGAZA KUJIUZULU NAFASI YAKE

Ally Shaban Kamwe leo Julai 28, 2024 ametangaza kujiuzulu nafasi yake kama Meneja wa idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga Sc baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka miwili kwa mafanikio tangu Septemba 25, 2022.

TAARIFA zilizotufikia kutoka vyanzo vya uhakika zimedokeza kuwa aliyekuwa afisa habari wa Yanga SC Ally Shaban Kamwe Ameandika barua kwa uongozi wa Yanga SC Kujiuzulu nafasi yake ya idara ya Habari na mawasiliano baada ya kuitumikia nafasi hiyo toka Septemba 25 mwaka 2022 Hadi leo alipojiuzulu Rasmi .

Kupitia page yake ya Instagram Ally Kamwe mwenyewe ameandika hivi .

"Mtumbuizaji mzuri anatakiwa kujua ni wakati gani wa kuondoka Jukwaani..

Maneno ya hekima kutoka katika kinywa cha Patrick Loch Otieno Lumumba;

Na ni Hekima hii, inanituma mbele yenu Wananchi, Mashabiki na Wanachama wa Klabu yetu pendwa, kuwaambia kuwa, Ni wakati sasa wa kijana wenu kuondoka Jukwaani.

Nimesimama Miaka miwili juu ya hili Jukwaa, Tumeimba, Tumecheza, Tumefurahi na Alhamdulillah Tumeshinda pamoja kila pambano Lililokuja mbele yetu.

Muda wangu umemalizika na Asanteni sana.

Tutaonana tena Wakati mwingine nikiwa na kitu kizuri cha kuwaonyesha Juu ya Jukwaa.

 

Jumapili, 28 Julai 2024

YANGA SC MABINGWA TOYOTA CUP

 

KLABU ya Yanga imefanikiwa kubeba Kombe la TOYOTA nchini Afrika Kusini ambapo Yanga walialikwa kucheza na timu ya Kaizer Chiefs.

Yanga Sc imefanikiwa kubeba kombe hilo mara baada ya kuifunga Kaizer Chiefs mabao 4-0 kwenye mchezo huo.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Aziz Ki ambaye amefunga mabao mawili, Mzize pamoja na Prince Dube.




Listen Mkisi Radio