JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Top Stories.. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Top Stories.. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 23 Mei 2025

ATCL, TAA, TCAA PAMOJA NA TMA ZA SAINI MAKUBALIANO YA MAGEUZI MAKUBWA KATIKA ANGA LA TANZANIA


 Big moves in aviation! ATCL, TAA, TCAA na TMA sign one game-changing MoU – future of Tanzania’s skies looks digital, united & full of global dreams. 


Mageuzi makubwa kwenye sekta ya anga! ATCL, TAA, TCAA&TMA wasaini makubaliano ya Ankara Jumuishi– anga la Tanzania kuendelezwa kidijitali. 

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imepiga hatua zaidi kuelekea kwenye masoko ya dunia ambapo inaendelea kuunganisha mifumo yake na wadau wa kisekta.


Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Mha. Peter Ulanga, amesema muunganiko wa mifumo hiyo ni hatua madhubuti inayoendana na mageuzi ATCL ili kuendelea kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwenye masoko ya ndani na nje ya Tanzania.

"Tunaamini huu ni mwanzo wa safari mpya. Safari ya kuifanya ATCL kuwa kidigitali zaidi", amefafanua, Mha. Ulanga.


Taasisi zote nne kwa pamoja zimetambua mchango wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwezesha mafanikio haya.

TANZANIA YAJIKITA KUPAMBANA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

 

TANZANIA YAJIKITA KUPAMBANA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA 


Na, WAF-Dodoma


Tanzania imeongeza juhudi za kupambana na magonjwa yasiyoambukiza kwa kuimarisha elimu ya afya kwa umma, kuhamasisha mabadiliko ya mtindo wa maisha, na kuboresha upatikanaji wa huduma za afya, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).


Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mkutano wa mwaka wa Chama cha Madaktari wa Magonjwa ya Ndani Tanzania (APHTYA), Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema kuwa Serikali imeweka mkazo mkubwa katika kupambana na magonjwa yasiyoambukiza kama vile shinikizo la damu, kisukari, magonjwa ya moyo na saratani, ambayo yamekuwa chanzo kikubwa cha vifo na kupungua kwa tija ya nguvu kazi nchini.


Hatua hizo ni sehemu ya mkakati mpana wa taifa katika kufikia dira ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Serikali inatambua kuwa mafanikio ya mpango huu yanategemea uwepo wa wataalam waliobobea katika taaluma zao pamoja na wananchi wenye afya njema, ambao kwa pamoja wataweza kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.


Dkt. Mollel ameeleza kuwa ongezeko la magonjwa haya linachangiwa na mabadiliko ya mtindo wa maisha, ikiwa ni pamoja na lishe duni, kutofanya mazoezi, matumizi ya tumbaku, na unywaji wa pombe kupita kiasi, hali ambayo inahatarisha ustawi wa taifa na kuathiri juhudi za maendeleo.


Serikali kwa kushirikiana na wadau wa afya, inaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kinga, lishe bora, na upimaji wa afya mara kwa mara. Vilevile, huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa haya zinaendelea kuimarishwa katika vituo vya afya nchini kote.


Pia, Dkt. Mollel, amebainisha kuwa juhudi hizi ni muhimu ili kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma stahiki, na taifa linakuwa na jamii yenye afya bora, tayari kushiriki katika kujenga uchumi imara unaojali ustawi wa watu wake.

CHALAMILA, SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI


CHALAMILA, SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amewataka wauguzi nchini kufanya kazi kwa uadilifu na kwa kufuata misingi ya sheria ya kazi yao ili kulinda afya za wananchi na kwamba Serikali Mkoani humo inatambua na kuthamini kazi ya uuguzi katika kulinda afya za wananchi

Akizungumza leo Mei 23,2025 Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya wauguzi kimkoa yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amesema wauguzi ni nguzo muhimu kwenye utoaji wa huduma za afya hivyo ni muhimu kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu kama ambavyo kanuni za kazi hiyo zinavyowataka

Aidha RC Chalamila ameitaka jamii kutambua na kuthamini kazi inayofanywa na wauguzi na kusisitiza kuwa Serikali Mkoani humo itaendelea kushirikiana na wizara ya afya ili kuimarisha zaidi mazingira ya utolewaji wa huduma za afya, pia akiisisitiza jamii kuendelea kutambua sera ya afya inayohitaji wananchi kuchangia huduma hiyo


Sanjari na hayo amesisitiza wakazi wa jiji hilo na watanzania kwa ujumla kuendelea kulipa kodi kwa mujibu sheria kwani kodi ndio nyenzo ya kuboresha huduma za kijamii ikiwemo  huduma za afya na amemshukuru Rais Dokta Samia kwa namna ambavyo amekuwa akiimarisha upatikanaji wa huduma za Afya hivyo amesisitiza kuwa wauguzi ndiyo faraja kubwa kwa wagonjwa

Kwa upande wake Rais wa chama cha Wauguzi Tanzania Tanna Ezekiel Henry amewataka wauguzi kuendelea kufanya kazi zao kwa weledi na kwa kufuata sheria na kanuni za kazi hiyo huku akiitaka jamii kuheshimu kazi ya uuguzi kwenye kulinda afya za wananchi

Kwa upande wake Rais wa chama cha wakunga Tanzania TAMA Dokta Beatrice Mwilike amezungumzia umuhimu wa ushiriki wa wanaume kwenye Afya ya mama mjamzito wakati wa kujifungua na kwamba wanaendelea kuimarisha mafunzo kwa wakunga ili kuboresha huduma huku Kaleb Kiula Muuguzi kutoka hospitali ya Mloganzila wakati akisoma risala ameiomba Serikali kudhibiti kazi za baadhi ya wasanii wanaodhihaki kazi ya uuguzi.


Maadhimisho hayo yamebeba kaulimbiu isemayo "Wauguzi Nguvu ya Mabadiliko Duniani"ambapo kupitia maadhimisho hayo wauguzi wamewasha mshumaa wa upendo na kula kiapo cha kufanyakazi kwa uadilifu na kutunza siri mbele ya mkuu wa Mkoa. 

WANAJAMII TUJIPANGE KUEPUSHA MIGOGORO - DKT. BITEKO


📌 Dkt. Biteko azindua kitabu cha miaka 35 ya TAWLA


📌 Rais Samia aipongeza TAWLA kushiriki kampeni za kisheria


📌 TAWLA yaipongeza Serikali miradi ya kimkakati 


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka wanajamii kujiepusha na mazingira yanayoweza kusababisha migogoro baada ya wao kufariki


Dkt. Biteko amesema hayo Mei 23, 2025 Jijini Dar es Salaam alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua Kongamano na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wanasheria Wanawake nchini - TAWLA


Amesema endapo wanajamii watajiandaa na kuweka mazingira mazuri, wataepusha migogoro isiyo ya lazima na jamii itaishi kwa amani na kupunguza gharama zinazotumika kurekebisha jamii yenye migogoro

Aidha, ameipongeza TAWLA kwa kazi nzuri iliyodumu kwa miaka 35 tangu kuazishwa kwake mwaka 1990


“ Tangu mlipoanzishwa kuna vyama vingi vya kijamii vilianzishwa sambamba na chama chenu, lakini vingine vilikufa baada ya mwaka mmoja, vingine vilikufa baada ya miaka mitano na vingine vilisambaratika baada ya miaka 10. Ninyi mmeimarika na kukua hadi leo na mnaendelea kufanya kazi nzuri,” ameoongeza Dkt. Biteko

Pia amewasilisha pongezi za Rais Samia kwa TAWLA kupitia kushiriki kampeni ya msaada wa kisheria ya Samia Legal Aid na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao kuhakikisha jamii inaishi kwa amani na upendo kama ilivyo ndoto ya TAWLA ya kuwasaidia watu wenye uhitaji.


“Bila mchango wenu, mafanikio yanayozungumzwa serikalini huenda yasingekuwa yanazungumzwa kwa kiwango hicho, amesema Dkt. Biteko


Ameutaka uongozi wa TAWLA kuendelea kuwashawishi na kuwavutia wanachama wapya watakaoweza kutoa msaada bila kusita katika jamii yao.


Amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali za kuhakikisha wanawake wanakuwa katika nafasi mbalimbali za maamuzi ikiwemo kuongeza uwiano wa majaji wanawake na wanaume katika mahakama za rafani na mahakama Kuu Akizungumzia Uchaguzi Mkuu ujao, Dkt. Biteko amewahimiza wajumbe wenye nia kujitokeza na kugombea uongozi ili kuwakilisha wananchi hususan wanawake wanaongezeka

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila ameipongeza TAWLA kwa kazi ya kutetea kundi maalum la wanawake na kuliwezesha kupata msaada wa kisheria


“TAWLA inafanya kazi kubwa ya kufanyia kazi tabia za watu na kazi hiyo inahitaji mawanda mapana” amesema na kuongeza kuwa wadau wa sheria wanashughulia watu wenye malezi na makuzi tofauti hivyo, kazi yao ni kubwa inayohitaji kufanyika kwa weledi wa hali ya juu

Mwenyekiti wa TAWLA Wakili Suzan Ndomba ameipongeza Serikali kwa hatua zake za kulinda haki na kushughulikia changamoto za zinazowakabili wanawake na watoto nchini


Amesema hatua ya Serikali kuwekeza katika utekelezaji wa miradi ya nishati, maji na elimu ni fursa zaidi kwa kundi la wanawake wa Tanzania ambao wamekuwa waathirika wakubwa madhara yanayotokana na ukosefu wa miundombinu hiyo


Amefafanua kuwa tangu kuanzishwa kwa TAWLA, chama hicho kimeshiriki kutoa mafunzo kwa baadhi ya mawakili, kuanzisha huduma ya simu ya bure kwa ajili ya wateja wake kurupoti vitendo na matukio ya ukatili, kuwatetea wateja wake mahakamani, kushiriki katika kuandaliwa na kutungwa kwa sheria ya mtoto ya mwaka 2009 pamoja na kutungwa kwa kifungu maalum cha makosa ya kujamiiana SOSPA (2008)

TAWLA ilianzishwa mwaka 1990 ikiwa na wanachama 40 na idadi yao imeongezeka hadi 420 miaka 35 baadaye.

WAZIRI MKUU KUMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA MAONESHO YA WORLD EXPO 2025 OSAKA, JAPAN


 WAZIRI MKUU KUMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA MAONESHO YA WORLD EXPO 2025 OSAKA, JAPAN


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 23, 2025 amewasili Osaka nchini Japan kumwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye maonesho ya kimataifa ya Osaka (World Expo 2025 Osaka).

 

Akiwa nchini Japan, Mheshimiwa Majaliwa atashiriki katika kongamano la biashara, uwekezaji na utalii ambalo litahusisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Japan.

 

Pia, Waziri Mkuu atashiriki katika Mikutano ya Uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan.

 

Maonesho hayo yalianza tangu Aprili 13, 2025 na yanatarajia kumalizika Oktoba 13, 2025, hii ni mara ya pili kwa Japan (Osaka) kuwa mwenyeji wa maonesho haya ya kimataifa, ambapo mara ya mwisho yalifanyika 1970 (EXPO 1970).

SERIKALI IMETOA RUZUKU YA ASILIMIA 20 HADI 50 KWENYE MITUNGI YA GESI LAKI 4.4 – KAPINGA


📌 *Asema lengo ni kupunguza gharama na kuhamasisha Nishati Safi ya Kupikia*


*📌  REA kusambaza majiko banifu 200,000 kwa punguzo la hadi asilimia 75*


📌 *Baada ya umeme kufika kwenye vijiji vyote; Serikali kuendelea kuhamasisha matumizi ya majiko ya umeme*



Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali imetoa ruzuku ya asilimia 20 hadi 50 kwenye mitungi ya gesi ya LPG takribani 452,445 kwa watumiaji wa mwisho ikiwa ni jjtihada za kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.


Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Mei 23, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Grace Tendega aliyetaka kufahamu Serikali ina mkakati gani wa muda mfupi wa kuhakikisha Wananchi wa Vijijini wanatumia Nishati Safi ya kupikia badala ya Kuni na Mkaa.

 

"Mheshimiwa Mwenyekiti Serikali kupitia REA pia  itasambaza majiko banifu 200,000 yenye bei ya punguzo la hadi asilimia 75 pamoja na kuwezesha ufungaji wa mifumo ya nishati safi ya kupikia katika Taasisi za Umma zinazohudumia watu zaidi ya 100."  Amesema  Kapinga


Aidha, amesema Serikali imekamilisha kazi ya usambazaji umeme katika vijiji vyote hivyo kwa sasa inaendelea kuhimiza matumizi ya majiko ya kupikia yanayotumia umeme ikiwa ni njia mojawapo ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi wa vijijini badala ya kutumia kuni na mkaa.


Mhe. Kapinga ametanabaisha  kuwa, Mkakati wa Taifa wa  Nishati Safi ya Kupikia ni wa miaka kumi lakini Serikali inao mkakati wa matumizi bora ya nishati ambao unahusisha pia sekta binafsi kwa ajili ya kusaidia kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.


Akijibu swali la Mbunge wa Mbulu, Mhe. Zacharia Isaay aliyeuliza Serikali imejipangaje kuhakikisha Vitongoji vyote vilivyokusudiwa katika mwaka huu wa bajeti kufikiwa  na umeme katika kipindi cha mwezi mmoja uliobaki, Mhe. Kapinga amesema Serikali inayo mikakati na miradi mbalimbali ya kupeleka umeme katika Vitongoji. 


Amesema kuwa, moja ya mikakati hiyo ni kupeleka umeme katika Vitongoji 15 kwa kila Jimbo, na pia  Serikali imekuja na mkakati wa kupeleka umeme katika Vitongoji 20,000 ambapo   awamu ya kwanza inaanza kupeleka umeme katika Vitongoji 9000 na hatua iliyopo ni utafutajj wa wakandarasi.


Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Anatropia Theonest aliyeuliza bei ya Serikali ya ruzuku imeanza kutumika lini kutokana na mitungi ya gesi kuendelea kuuzwa kati ya 22,000/- na 25,000 na kwa mitungi mikubwa ya kilo 15 shilingi 50,000/- na 60,000/-,  Mhe. Kapinga ameeleza kuwa kwa maeneo ya mjini Serikali imepeleka ruzuku hadi asilimia 25 na maeneo ya Vijijini ni kati ya asilimia 50 hadi 75 na kutolea mfano iwapo mtungi ulikuwa unauzwa shilingi 45,000/- kwa bei ya ruzuku inapatikana kwa shilingi 17,000/- hadi 21,000/- na kusema ni zaidi ya nusu ya bei yake.


Ameongeza kuwa, katika kila Wilaya kuna takribani mitungi 3,255 inayopatikana kwa ruzuku na kuongeza kuwa ndio kwanza mkakati umeanza.


Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Yustina Rahhi alieuliza mpango wa Serikali kuwapelekea jamii ya wafugaji teknolojia ya biogas au kuwajengea majiko yanayotumia samadi ya gesi ambayo ni rahisi, Mhe. Kapinga amesema Serikali inatekeleza mradi huo kupitia umoja wa Ulaya (mfuko wa UNCDF) ambao unateknolojia alizozitaja Mhe. Mbunge.


Akijibu swali la Mbunge wa Nyang’wale, Mhe. Hussein Amar aliyeuliza kuhusu mpango wa Serikali kuzipelekea nishati safi ya kupikia  Shule za Sekondari 19 na Sekondari 12 za bweni zilizo Wilaya ya Nyang’wale ili kulinda mazingira,  Mhe. Kapinga amesema Wizara ya Nishati inaompango wa kuzipelekea nishati safi ya kupikia Taasisi za umma kwa kushirikiana na TAMISEMI.


Katika hatua nyingine Mhe. Kapinga amezishauri Halmashauri  kufunga mifumo ya nishati safi ya kupikia  katika Taasisi zilizopo katika Halmashauri wanazoziongoza kwa kutumia mapato ya ndani.

TBS IMEWATAKA WATANZANIA KUWA NA MAZOEA YA KUSOMA NA KUELEWA TAARIFA ZILIZOPO KWENYE VIFUNGASHIO

 

Dar es Salaam — Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewahimiza wananchi kuwa na mazoea ya kusoma na kuelewa taarifa zilizoandikwa kwenye vifungashio vya bidhaa kabla ya kuzinunua, likieleza kuwa taarifa hizo ni muhimu katika kuhakikisha ubora na usalama wa bidhaa zinazotumiwa.

Akizungumza na vyombo vya habari, Meneja wa Ukaguzi na Utekelezaji wa Sheria wa TBS, Nuru Mwasulama, alisema taarifa zinazopatikana kwenye vifungashio ni kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya mtengenezaji na mtumiaji. Alifafanua kuwa taarifa hizo zinahusisha jina la bidhaa, maelekezo ya matumizi, uthibitisho wa ubora, usalama pamoja na tarehe ya mwisho ya matumizi.

"Taarifa za kwenye vifungashio maana yake ni utambulisho wa bidhaa kwa mlaji. Zinakuambia bidhaa hiyo ni nini, inakupa maelekezo ya matumizi, uhakika wa ubora, usalama, na tarehe ya mwisho ya matumizi," alisema Mwasulama.
Kwa upande wake, Afisa Mkaguzi Mwandamizi wa TBS, Baraka Mbajije, alitoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika kulinda afya zao kwa kutoa taarifa pindi wanapokutana na bidhaa zilizoisha muda wa matumizi au zenye kasoro.

"Mtumiaji naye ana wajibu wa kuripoti bidhaa yoyote yenye dosari au iliyopita muda wa matumizi kabla mamlaka haijafika," alisema Mbajije.

TBS imeendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kusoma vifungashio, ikisisitiza kuwa ulinzi wa afya ya mlaji unaanzia katika uelewa wa kile anachonunua na kutumia.

USHIRIKIANO WA WADAU UMEPUNGUZA VIFO VYA WAKINA MAMA, WATOTO TANZANIA


 USHIRIKIANO WA WADAU UMEPUNGUZA  VIFO VYA WAKINA MAMA,  WATOTO TANZANIA

Na WAF - Geneva, Uswisi

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ameelezea mafanikio ya Tanzania yanayopatikana yanatokana na ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na wadau ambayo ni pamoja na kupungua kwa vifo vya kina mama wajawazito pamoja na watoto wachanga. 

Waziri Mhagama ameeleza hayo wakati akifanya mazungumzo na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya ya Laerdal Global Health, Bw. Tore Laerdal,  ambao ni wadau wakubwa katika sekta ya afya nchini Tanzania. 

"Serikali ya Tanzania imejidhatiti katika kuboresha afya na ustawi wa wanawake na wasichana pamoja na watoto ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili kwa kulenga maeneo ya kuimarisha mifumo ya afya kama ilivyoainishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO)," amesema Waziri Mhagama.

Aidha, Waziri Mhagama amesema Serikali ya Tanzania imeanzisha mikakati mbalimbali ya kuboresha afya za wanawake na wasichana, ikiwemo kuboresha mfumo wa fedha za afya, kuanza utekelezaji wa huduma ya afya kwa wote. 

"Lakini pia tumeanza uboreshaji wa mfumo wa rufaa za dharura kama vile mradi wa m-mama, kufanya tathmini na ufuatiliaji wa vifo vya kina mama na watoto, kuboresha ubora wa huduma kwa wanawake, wasichana na watoto wachanga, kuimarisha ujuzi wa wahudumu wa afya kupitia mafunzo na mazoezi ya vitendo," amesema Waziri Mhagama.

Katika kikao hicho wamekubaliana kuendeleza ushiriikiano baina ya Taasisi hiyo na Serikali ya Tanzania ili kuboresha zaidi katika maeneo hayo.

CHANGAMOTO ZA NJAA NA UMASKINI ZINAHITAJI MAJIBU YA PAMOJA YA KIMATAIFA

 

kuangaziwa katika kukabiliana na njaa na umasikini ikiwemo vita na migogoro ya kisiasa, mabadiliko ya tabianchi, ukosefu wa miundombinu muhimu kwaajili ya kilimo kama vile umwagiliaji, uhifadhi mazao pamoja na TEHAMA ambayo husaidia taarifa muhimu za mbegu, masoko na bidhaa za kilimo.



Ametaja changamoto zingine za kuangaziwa kama vile ukosefu wa ufadhili katika sekta ya kilimo, changamoto ya kuuza malighafi ambazo hazijaongezwa thamani, uwekezaji katika utafiti na maendeleo, kukosekana kwa taarifa muhimu katika sekta ya kilimo, changamoto za kiteknolojia katika nyanja zote za uzalishaji pamoja na changamoto ya sera za ushuru na biashara ambazo hazihamasishi kukua kwa kilimo na shughuli za kilimo.

Majadiliano kati ya Brazil na Nchi za Afrika ni ya pili katika mzunguko wa majadiliano ya namna hiyo, ambapo majadiliano ya kwanza yalifanyika mwaka 2010 nchini Brazil. Majadiliano hayo huandaliwa na Serikali ya Brazil kupitia Wizara ya Kilimo ya nchi hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kiufundi la Brazil (ABC) Pamoja na Shirika la Utafiti wa Kilimo la Brazil (EMBRAPA).

Majadiliano hayo huwaleta pamoja Viongozi wakuu wa Serikali, Mawaziri wa Kilimo kutoka Afrika, Mashirika ya Kimataifa kama FAO, IFAD, WFP, Benki ya Dunia pamoja na wataalamu na washirika wa kiufundi. Kadhalika majadiliano hayo yametoa fursa ya kipekee ya kuangazia maeneo ya ushirikiano chini ya Mpango wa Kimataifa dhidi ya Njaa na Umaskini (Global Alliance against Poverty and Hunger) uliozinduliwa kwenye Kikao cha G20 Novemba 2024, jijini Rio de Janeiro, pamoja na kujadili mafanikio ya moja kwa moja katika sekta za kilimo, usalama wa chakula na lishe, ushirikiano wa kiufundi na biashara ya kimataifa.

Katika Mkutano huo, Makamu wa Rais ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo anayeshughulikia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula Dkt. Hussein Omar Pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Brazil Mhe. Balozi Dkt. John Simbachawene.

MBUNGE MAVUNDE AKABIDHI MATOFALI 41,000 NA SARUJI TANI 102 KUCHOCHEA SHUGHULI ZA MAENDELEO DODOMA JIJI


▪️Ni kuunga mkono miradi inayoibuliwa na wananchi kwa kata zote 41


▪️Jiji la Dodoma latenga Bilioni 6 kuunga mkono miradi inayoibuliwa na wananchi


▪️Vifaa kulenga kuboresha sekta ya Afya na Elimu


▪️Rais Samia apongezwa kwa maendeleo makubwa Dodoma Jiji


Mwenyekiti wa kamati ya Mfuko wa kuchochea maendeleo ya Jimbo na Mbunge wa Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde leo amekabidhi matofali 41,000 na Saruji tani 102 kwa kata zote 41 za Dodoma Mjini kwa lengo la kuunga mkono miradi inayoibuliwa na wananchi katika ujenzi wa miundombinu ya Elimu na vituo vya Afya.

“Mfuko wa Jimbo hujielekeza katika miradi ya kipaumbele ya Elimu,Afya na uwezeshwaji wananchi kiuchumi.


Leo tunakabidhi matofali na saruji kwa kata zote 41 kwa lengo la kuunga mkono miradi inayoibuliwa na wananchi.


Kwasasa Jiji la Dodoma limetenga Shilingi Bilioni 6 kuunga mkono miradi yote inayoibuliwa na wananchi ili kuchochea maendeleo zaidi ndani ya Dodoma Jiji.

Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan amefanya kazi kubwa sana ya kuiendeleza Dodoma hivyo ni wajibu kazi hii nzuri kuungwa mkono kwa wivu mkubwa”Alisema Mavunde


Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh. Jabir Shekimweri na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Dodoma Ndg. Charles Mamba wamepongeza hatua ya Mfuko wa Jimbo kujibu mahitaji ya jamii na hasa katika kuboresha sekta ya Elimu na Afya na hivyo kusaidia kusogeza maendeleo kwa wananchi kwa ukaribu zaidi.


Akitoa taarifa ya mfuko wa Jimbo,Mratibu wa Mfuko Bi. Debora Muwinje amesema mfuko wa Jimbo la Dodoma Mjini unapokea kiasi cha Shilingi Milioni 93 kuchochea maendeleo kiasi ambacho kimetumika na kugharamia mahitaji ya vifaa husika na kumpongeza Mbunge Mavunde kwa kuchangia mifuko ya saruji 1000 ya ziada ili kuhakikisha eneo kubwa zaidi linaguswa.

Alhamisi, 22 Mei 2025

Rais wa Zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki azuru Mazimbu Morogoro

Rais wa Zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki ametembelea eneo la kihistoria la Mazimbu, lililoko mkoani Morogoro ikiwa ni katika Maadhimisho ya Siku ya Afrika ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 25 Mei.


Ziara hiyo maalum imebeba uzito mkubwa wa kihistoria na kiishara, ikikumbusha mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi kwa Afrika Kusini wakati wa mapambano dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo .


Eneo la Mazimbu, kwa sasa ni sehemu ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), lilikuwa makazi na kituo cha mafunzo kwa wapigania uhuru wa Chama cha African National Congress (ANC) kilichokuwa kinaongozwa na Hayati Nelson Mandela. 

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Mbeki ametembelea makaburi ya wapigania uhuru waliofariki na kuzikwa katika eneo hilo na kuweka shada la maua, amepanda mti wa kumbukumbu na kutembelea hospitali ya SUA ambayo ilikuwa ikiwahudumia wana ANC  hao katika eneo la Mazimbu na kuzungumza na uongozi wa SUA ulioongozwa na Mkuu wa Chuo hicho Mzee Joseph Warioba.


Mheshimiwa Mbeki ameahidi kuwa Taasisi yake kwa kushirikiana na Taasisi ya Mwalimu Nyerere itaenda katika eneo hilo na kuandaa makala maalum ya picha Mwendo kwa lengo la kuhifadhi na kuipeleka historia ya eneo hilo kwa wananchi wa Afrika Kusini ili wajionee mchango wa Tanzania kwao.

Akizungumza baada ya kuzuru Makaburi hayo Mheshimiwa Mbeki wa  ametoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Tanzania na wananchi wake kwa uungwaji mkono usioyumba ambao walioutoa kwa ndugu zao wa Afrika Kusini wakati wa nyakati za dhiki.


“Mazimbu ni nyumbani kwetu, eneo hili si sehemu ya historia ya Afrika Kusini tu, bali ni alama ya mshikamano wa kweli wa Afrika. Tanzania ilisimama nasi wakati wa giza kuu la ukandamizaji. Leo tuko huru kwa sababu mlitupokea, mkatufundisha, na mkatupa hifadhi,” alisema Mbeki kwa hisia.

Taasisi ya Thabo Mbeki kwa Kushirikiana na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kwa pamoja wameshirikiana na kuandaa Maadhimisho ya Siku ya Afrika 2025 ambapo Mhadhara wa 15 wa Taasisi ya Thabo Mbeki utafanyika jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei ili kuadhimisha siku ya Afrika nchini. 

DKT. NATU MWAMBA ATETA NA BALOZI WA IRELAND NCHINI

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na  Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mhe. Nicola Brennan, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadiliana kuhusu ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Ireland. 


Dkt. Mwamba aliishukuru Serikali ya Ireland kwa kuendelea kuiunga mkono Tanzania kupitia ufadhili wa programu mbalimbali za maendeleo, zikiwemo Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) na Mfuko wa Pamoja wa Afya (Health Basket Fund).

Kwa upande wake, Balozi wa Ireland alishukuru kwa ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili na akasisitiza kuwa Ireland itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kufanikisha malengo ya pamoja ya maendeleo.


Aidha, viongozi hao walijadili kwa kina maoni na maazimio yaliyotokana na Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Majadiliano kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo uliofanyika tarehe 28 Februari 2025, Hazina-Dodoma, ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa maazimio ya mkutano huo.

Katika kikao hicho, Mhe. Balozi Nicola Brennan, aliambatana na Naibu Balozi wa Ireland hapa nchini, Bi. Mags Gaynor na Meneja Programu anayesimamia masuala ya Uchumi Jumuishi, katika Ubalozi wa nchi hiyo, Bw. Francis Sampa na kwa upande wa Tanzania alikuwepo pia Bw. Norbert Mwitta, Mchumi, Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha.

 




SUMA JKT YACHANGIA BIL.2.66 KWA SHUGHULI ZA VIJANA WA JKT


 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) amesema kwa kipindi cha miaka minne kuanzia Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi 2024/25, SUMAJKT limechangia jumla ya Shilingi Bilioni 2.66 kwa ajili ya kugharamia shughuli za malezi ya vijana wa JKT, na limetoa gawio lenye jumla ya Shilingi Bilioni 4.27 kwenda Mfuko Mkuu wa Serikali (HAZINA).

Waziri Dkt. Tax ameyasema hayo leo tarehe 22 Mei 2025 Jijini Dodoma, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Amesema Wizara hiyo kupitia SUMAJKT pia imefanikiwa kuchangia katika ujenzi wa uchumi ili kuipunguzia Serikali gharama za uendeshaji wa mafunzo kwa vijana wa JKT kwa kutekeleza miradi mbalimbali kama vile Ujenzi wa vituo vya madini katika mikoa ya Tanga (Handeni), Ruvuma (Songea), Katavi (Mpanda), Mbeya (Chunya), Simiyu (Bariadi), Mara (Musoma) na Kagera (Bukoba) na Vile vile, ujenzi wa ukuta katika migodi ya Mirerani Simanjiro, Manyara.

"Kuimarisha viwanda vyake ikiwemo Kiwanda cha Maji ya kunywa Mgulani kilichofikia uwezo wa kuzalisha katoni 2500 za nusu lita na 4400 za lita moja kwa siku, Kiwanda cha ushonaji Mgulani chenye uwezo wa kuzalisha mavazi ya kijeshi 300 hadi 400 kwa siku, Kiwanda cha bidhaa za ngozi Mlalakuwa, Kiwanda cha Kuchakata mahindi Mlale Songea chenye uwezo wa kuchakata tani 20 kwa siku, Kiwanda cha Samani Chang’ombe na kiwanda cha taa za LED kilichopo Dar es Salaam.

"Ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa umeme vijijini kupitia mradi wa REA  katika mikoa ya Morogoro, Shinyanga na ufungaji wa umeme (Installation) katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Singida, Shule ya Mfano jijini Dodoma na Ofisi ya Rais (Ikulu) Chamwino" alisema Waziri Dkt.Tax.

GST NA BGS YA UINGEREZA ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO UTAFITI WA MADINI

 

London, na Mwandishi Wetu

 Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Taasisi ya Jiolojia ya Uingereza (BGS) zimesaini makubaliano ya ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya tafiti za madini.

Hati ya Makubaliano (MoU) hayo imesainiwa leo Mei 22, 2025 jijini London Uingereza na kushuhudiwa na Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo pamoja na Balozi wa Tanzania nchini humo Mhe. Mbelwa Kairuki.

 Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo ambayo pia yamefanyika Kwa njia ya mtandao, Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Daniel Budeba amebainisha maeneo ya ushirikiano kuwa ni pamoja na kufanya tafiti za madini; vifaa vya teknolojia ya kisasa na uchunguzi wa sampuli za madini maabara.

Dkt. Budeba ametaja maeneo mengine ya ushirikiano ni kufanya miradi ya pamoja katika utafiti wa jiolojia, jiokemia, utafiti wa jiofizikia kwa kutumia ndege, ugani wa jiolojia, ufuatiliaji na usimamizi wa masuala ya majanga asili ya jiolojia, usimamizi wa taarifa za jiosayansi na masuala ya kimazingira na mafunzo kwa watumishi na kubadilishana uzoefu.

Aidha, Dkt. Budeba ameongeza kuwa, makubaliano hayo yatakuwa na manufaa kwa pande zote mbili ambapo Tanzania itanufaika na ujuzi na teknolojia mpya katika kufanya tafiti za madini, huduma za maabara na usimamizi wa taarifa za jiosayansi.

Awali, akifungua hafla hiyo ya utiaji Saini Makubaliano hayo, Naibu Katibu Mkuu Mbibo amezishukuru pande zote mbili kwa kufanikisha kuandaa Hati hiyo na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha shughuli hiyo muhimu.

RAIS MWINYI KUMWAKILISHA RAIS SAMIA SADC ZIMBABWE


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameondoka Zanzibar na kuwasili nchini Zimbabwe kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Rais Dkt. Mwinyi, akiambatana na Mkewe, Mhe. Mama Mariam Mwinyi, alipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe, jijini Harare, na Balozi wa Tanzania nchini humo, Balozi CP Suzan Kaganda.

Rais Dkt. Mwinyi anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika mkutano huo ambao utajadili Mwongozo na Uhifadhi Endelevu wa Biashara ya Kaboni katika nchi wanachama wa SADC.



MRADI WA UJENZI WA DARAJA LA WASHI LENYE UREFU WA MITA 13 LAFIKIA ASILIMIA 45

Mradi wa ujenzi wa daraja la Washi lililopo kata ya Heradu, Wilaya ya Same, ambalo linaunganisha mkoa wa Kilimanjaro na Tanga katika barabara kuu ya Same - Dar es Salaam lenye urefu wa mita 13 limefikia asilimia 45.


Daraja hilo pamoja na kipande cha barabara chenye urefu wa kilomita 0.675 inayojengwa katika barabara hiyo kwa gharama ya Sh 1.4 bilioni  inatarajia kukamilika Agosti 28, mwaka huu.

 


Akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo, wakati kamati ya usalama ya Wilaya hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea eneo hilo la mradi,  Mhandisi Witness Maeda amesema kukamilika kwa mradi huo kutapunguza changamoto ya mafuriko katika eneo hilo ambalo  kipindi cha mvua kubwa barabara hiyo hujaa maji na kusababisha adha kwa watumiaji wa barabara hiyo.


Aidha, Mhandisi Maeda amesema kukamilika kwa daraja hilo kutasaidia kurahisisha huduma za mawasiliano ya barabara hiyo kuu ambayo imekuwa ikikumbwa na mafuriko mara kwa mara  kutokana na maji kujaa barabarani kutokana na changamoto ya daraja.



Akizungumza katika ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amemtaka mkandarasi anayesimamia mradi huo kuhakikisha unajengwa kwa ubora na kwa viwango vinavyotakiwa na kuhakikisha unakamilika ndani ya muda uliopangwa.

Listen Mkisi Radio