Monday, March 24, 2025
WIZARA YA NISHATI YATAJA VIPAUMBELE VYA BAJETI YA MWAKA 2025/2026
WATAALAM OFISI YA MSAJILI HAZINA WAJIFUNGIA KUCHAMBUA BAJETI
URENO YAISAMBARATISHA DENMARK IKITINGA NUSU FAINALI KIBABE
Timu ya Taifa ya Ureno chini ya Kapteni Cristiano Ronaldo imefanikiwa kutinga nusu fainali ya Ligi ya Uropa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-3 dhidi ya Denmark. Mchezo huo mgumu uliopigwa dimba la Estádio José Alvalade nchini Ureno uliibua hisia kwa mashabiki wa soka duniani kote baada ya Cristiano Ronaldo kukosa penati muhimu lakini alisahihisha makosa hayo na kufunga bao muhimu.
Tathmini ya Mchezo
Ureno waliingia vichwa chini katika mchezo huo baada ya kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza kwa bao 1-0 nchini Denmark kwa bao la mshambuliaji kinda Hojlund. Ureno walianza mchezo huo kwa mashambulizi makali na kujipatia penati dakika ya 6 lakini mpigaji Cristiano Ronaldo alishindwa kufunga baada ya golikipa wa Denmark Kasper Schmeichel kudaka mpira mwepesi.
Ureno walizidisha mashambulizi na dakika ya 38 Joachim Andersen wa Denmark alijifunga na kuwafanya Ureno kwenda mapumziko kwa bao 1-0. Dakika ya 56 Rasmus Kristen wa Denmar alifanikiwa kusawazisha bao.
Dakika ya 72 Ronaldo alirejesha furaha kwa mashabiki wa Ureno kwa kufunga bao la pili na kusawazisha makosa ya kukosa penati lakini Cristien Eriksen alisawazisha bao hilo dakika ya 76 na matokeo kuwa 2-2.
Kocha wa Ureno alifanya mabadiliko kwa kuwatoa washambuliaji wote wakiongozwa na Ronaldo ,Rafael Leao na na kuwapa nafasi Trincao aliyefunga mabao mawili ya dakika ya 86 na 91kisha bwana mdogo goncalo Ramos kufunga bao la 5 dakika ya 115 na kuwaondosha Denmark kwenye michuano hiyo.
Matokeo hayo yanawafanya Ureno kutinga nusu fainali ya Ligi ya ulaya wakichuana na Ujerumani katika hatua hizo,kama watashinda mchezo huo basi watatinga fainali ya michuano hiyo
Sunday, March 23, 2025
URITHI WA MALIKALE NCHINI NI TUNU ADHIMU: DKT ABBASI
Na Sixmund Begashe -Njombe
Wanaosimamia maeneo ya Malikale nchini wametakiwa kuongeza kasi ya uhifadhi na uendelezaji wa maeneo ya urithi huo kwani ni kielelezo muhimu cha kurithisha kizazi cha sasa tunu muhimu za Taifa ambazo zimeasisiwa na waasisi wa taifa wakiongozwa na Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi, Mkoani Njombe, kwenye kikao kazi cha Wizara hiyo na taaasisi zilizokasimishwa maeneo ya Malikale, lengo likiwa ni kujenga uelewa wa pamoja na kupanga mikakati ya Uhifadhi na uendelezaji endelevu wa maeneo hayo.
Dkt. Abbasi amesema Serikali ilikabidhi maeneo hayo kwenye taasisi hizo kwa dhamira kubwa ili yahifadhiwe vyema na kuendelezwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
"Nchi yetu imejaliwa kuwa na urithi adhimu na adimu wa Malikale, ambao ni wa kipekee ukiwa ni alama muhimu za kihistoria Duniani, hivyo ni lazima tuhakikishe maeneo haya yanahifadhiwa vyema na kutangazwa ili yazidi kulinufaisha Taifa"Alisema Dkt. Abbasi
Dkt. Abbasi ameongeza kuwa matumizi ya urithi huo wa Malikale ni pamoja na kuelimisha jamii hasa kizazi cha sasa hususani juu ya historia ya nchi, utu, umoja wa kitaifa, mshikamano, na ni muhimu zaidi katika kipindi hiki chenye kasi kubwa ya utandawazi unaopelekea vijana wengi kujifunza tamaduni za kigeni.
Aidha, Dkt. Abbasi licha ya kuzipongeza Taasisi hizo kwa kazi nzuri wanazozifanya amehimiza kuimarisha ushirikiano katika uhifadhi endelevu wa urithi wa maeneo hayo nchini.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Malikale Dkt. Christowaja Ntandu pamoja na kumshukuru Katibu Mkuu kwa kuzikutanisha Taasisi hizo, ameahidi kuwa Idara anayoiongoza itaendelea kutekeleza majukumu yake na kuunga mkono jitihada kubwa zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za uhifadhi wa maeneo ya kihistoria nchini na kuyatangaza ili yafahamike ndani na nje ya nchi.
Katika kikao hicho kilichoudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi CP, Benedict Wakulyamba, kilijumuisha Wakurugenzi na Maafisa waandamizi wa Wizara hiyo, Wakuu wa Taasisi na Maafisa wao kutoka Makumbusho ya Taifa, Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Mamlaka ya Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania.
Saturday, March 22, 2025
BARAZA LA SABA LA WAFANYAKAZI WIZARA YA NISHATI LAKUTANA DODOMA
📌 Dkt. Kazungu asema Wizara itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Kimkakati.
📌 Baraza lapitisha rasimu ya bajeti ya 2025/2026 .
📌 Hoja za TUGHE zajadiliwa kwa kina na kupatiwa ufumbuzi
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Khatibu Kazungu leo Machi 22, 2025 amefungua Baraza la saba la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati ambalo limepitia pamoja na mambo mengine Rasimu ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2025/2026 na kupitia hoja mbalimbali zilizowasilishwa na TUGHE.
Akifungua baraza hilo Dkt. Kazungu amesema Wizara ya Nishati itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya nishati nchini ili kuhakikisha nchi inakua na uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme, mafuta na gesi.
"Wizara ya nishati itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya nishati nchini ili kuhakikisha Nchi inakuwa na uhakika wa nishati na katika kutekeleza hili wizara itahakikisha inasimamia taasisi zilizochini yake pamoja na makampuni tanzu yanayojishughulisha na nishati nchini". Amesema Dkt. Kazungu.
Kazungu ameelza kuwa Wizara itaendelea kutekeleza miradi ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme ikiwa ni pamoja na kufikisha Gridi ya taifa katika Mikoa iliyosalia ya Rukwa, Kagera, Lindi na Mtwara.
Aidha, Wizara itaendelea kutekeleza mpango wa taifa wa nishati wa mwaka 2025/2026 kwa lengo la kuongeza upatikanaji na uunganishaji wa umeme kwa wananchi, kuongeza mchango wa nishati jadidifu katika uzalishaji wa umeme na mashirika binafsi katika maendeleo ya sekta ya nishati na kuhakikisha upatikanaji wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Kutekeleza miradi wa Gridi ya taifa, kufanya matengenezo na ukarabati wa mitambo ya kuzalisha umeme pamoja na uboreshaji njia za kusafirishaji na usambazaji wa umeme katika vitongoji, maeneo ya migodi, viwanda pamoja na vituo vya afya.
Kwa upande wa Sekta ya mafuta na gesi, Dkt. Kazungu amesema sekta ya mafuta na gesi Wizara itaendelea kuwezesha upatikanaji wa bidhaa ya mafuta ,kupitia ujenzi wa vituo vya mafuta maeneo mbalimbali nchini.
Kazungu amesisitiza Wizara itaendelea kujikita katika kuwezesha utafutaji,uendelezaji na usambazaji wa gesi asilia na kutekeleza miradi ya kimkakati ya gesi asilia ikiwemo Mnazi bay Kasikazini,mradi wa kuchakata gesi asilia kuwa kimiminika (Lindi) ,utafutaji na uendelezaji na usambazaji wa mafuta ikiwemo ujenzi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Ohima (Uganda) hadi Chonholeani (Tanga-Tanzania).
Kwa upande wa nishati safi ya kupikia kwa mwaka wa 2025/2026 Wizara itaendelea kutekeleza mkakati wa matumizi ya nishati safi ya kupikia na mpango wa Taifa wa nishati wa mwaka 2030.
Aidha, Wizara itaendelea kuhamasisha sekta binafsi katika kuimarisha upatikanaji wa malighafi na miundombinu ya nishati safi ya kupikia.
Mwenyekiti wa Balaza la Wafanya kazi Wizara ya nishati Ndugu Zuena Msuya aliweza kueleza umuhimu wa kudumisha stahiki za watumishi ili kuendeleza ufanisi wa ufanyaji kazi katika Wizara ya Nishati.
WAKOPAJI WAKUMBUSHWA KUSOMA MIKATABA KABLA YA KUCHUKUA MIKOPO
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Arch. Chagu Nghoma, akizungumza alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi zake ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali mkoani humo.




Friday, March 21, 2025
NAIBU WAZIRI KATAMBI AZINDUA MRADI WA ‘VIJANA PLUS’

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi (katikati) akisikiliza kwa makini mawasilisho mbalimbali katika uzinduzi wa mradi wa Vijana Plus ambao umeratibiwa na Shirika la Save the Children kwa Ushirikiano na Taasisi ya Tanzaniabora Initiative pamoja na Umoja wa Ulaya ambayo imefanyika leo tar 21/3/2025 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi (kushoto) sambamba na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Save the Children Tanzania Angela Kauleni (kulia) wakiwa katika uzinduzi wa mradi wa Vijana Plus ambao umeratibiwa na Shirika la Save the Children kwa Ushirikiano na Taasisi ya Tanzaniabora Initiative pamoja na Umoja wa Ulaya ambayo imefanyika leo tar 21/3/2025 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Save the Children Tanzania Angela Kauleni katika hafka ya uzinduzi wa mradi wa Vijana Plus ambao umeratibiwa na shirika hilo kwa Ushirikiano na Taasisi ya Tanzaniabora Initiative pamoja na Umoja wa Ulaya ambayo imefanyika leo tar 21/3/2025 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya ambaye pia ni Meneja wa Asasi za Kiraia na Vijana Neema Bwewra akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa Vijana Plus ambao umeratibiwa na Shirika la Save the Children kwa Ushirikiano na Taasisi ya Tanzaniabora Initiative pamoja na Umoja wa Ulaya ambayo imefanyika leo tar 21/3/2025 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Tanzaniabora Initiative Ismail Biro akizunguma katika uzinduzi wa mradi wa Vijana Plus ambao umeratibiwa na Shirika la Save the Children kwa Ushirikiano na Taasisi ya Tanzaniabora Initiative pamoja na Umoja wa Ulaya ambayo imefanyika leo tar 21/3/2025 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Vijana serikali ya Mapinduzi Zanzibari na Mwakilishi wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar Shaibu Muhamad akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa Vijana Plus ambao umeratibiwa na Shirika la Save the Children kwa Ushirikiano na Taasisi ya Tanzaniabora Initiative pamoja na Umoja wa Ulaya ambayo imefanyika leo tar 21/3/2025 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Wasanii wakitoa burudani katika uzinduzi wa mradi wa Vijana Plus ambao umeratibiwa na Shirika la Save the Children kwa Ushirikiano na Taasisi ya Tanzaniabora Initiative pamoja na Umoja wa Ulaya ambayo imefanyika leo tar 21/3/2025 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Vijana kutoka taasisi na mashirika mbalimbali walioshirikia katika uzinduzi wa mradi wa Vijana Plus ambao umeratibiwa na Shirika la Save the Children kwa Ushirikiano na Taasisi ya Tanzaniabora Initiative pamoja na Umoja wa Ulaya ambayo imefanyika leo tar 21/3/2025 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
..........................
NA MUSSA KHALID
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi amesema serikali itaendelea kuhakikisha inaongeza fursa za ajira na mitaji kwa vijana ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Naibu Waziri Katambi ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati akizungumzia katika uzinduzi wa mradi wa Vijana Plus ambao umeratibiwa na Shirika la Save the Children kwa Ushirikiano na Taasisi ya Tanzaniabora Initiative pamoja na Umoja wa Ulaya ukitarajiwa kutekelezwa katika mikoa zaidi ya saba Tanzania Bara na Zanzibar.
Naibu Waziri amesema mradi huo unalenga kuwawezesha vijana kuwa viongozi bora kwenye taasisi na makampuni na vyombo mbalimbali vya maamuzi.
Aidha Naibu Waziri Katambi amewasisitiza kutambua kuwa wakati ni sasa hivyo wahakikishe wanatumia fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Awali akizungumzia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Save the Children Tanzania Angela Kauleni ,amesema kuwa takriban vijana Laki saba (700,000) wanatarajia kunufaika na mradi huo.
‘Tukiwawezesha vijana kwa kupitia mafunzo na rasilimali wanazozihitaji wataweza kuzibaini changamoto wanazokabiliana nazo lakini pia watakuwa na ujasiri na ushawishi wa kuishauri serikali na watunga maamuzi na sera ya kwamba ni jinsi gani Tanzania iendele ili kuleta matokeo chanya”amesema Kauleni
Kwa upande wao Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya ambaye pia ni Meneja wa Asasi za Kiraia na Vijana Neema Bwewra amesema kuwa umoja wa ulaya wameweza kifanya mipango kwa kuyasaidia mashirika ya vijana ili kuweza kujiongezea maendelei
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Tanzaniabora Initiative Ismail Biro wamesema kuwa dhamira yao ni kuhakikisha mradi huo unafanikiwa na kuleta matokeo Chanya kwa vijana na taifa kwa ujumla.
Naye Mkurugenzi wa Vijana serikali ya Mapinduzi Zanzibari na Mwakilishi wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar Shaibu Muhamad ametumia fursa hiyo kuipongeza Shirika la Save the Children na washirika wengine kuhusu mradi huo na kuahidi kuwa watatoa kila aina ya ushirikiano ili uweze kufanikiwa.