JSON Variables

Thursday, March 20, 2025

UKOROFI WAMPONZA SERGIO RAMOS WAMEXICO WAMJIA JUU

  Mkongwe wa timu ya Taifa ya Hispania Sergio Ramos mwenye rekodi za kipekee Ulaya na Duniani  amejikuta katikati ya utata baada ya mechi ya hivi majuzi huko Mexico. Nyota huyo anayekipiga Monterrey  aliwekwa kikaangoni na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka la Mexico na kuthibitisha rasmi kumfungia Ramos, kwa kukiri makosa makubwa ya mwamuzi wakati wa mchezo.


. Tukio hilo lilitokea katika dakika ya 20 wakati Ramos alipopiga teke la kizembe lililoelekezwa kwa mshambuliaji Guillermo Martรญnez.Ugomvi huo ulipelekea  machafuko katika mchezo na  tukio hilo limesababisha mzozo kutoka kwa viongozi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kocha mkuu wa Pumas Efraรญn Juรกrez.

 Juรกrez alionyesha kutoridhika kwake, akisisitiza kwamba Ramos hakupaswa kuruhusiwa kusalia uwanjani kwa zaidi ya dakika 70 baada ya kumzonga mlinzi Pablo Bennevendo. Hali hii inazua maswali kuhusu uthabiti wa wasimamizi wa ligi na viwango vinavyotarajiwa vya mwenendo wa wachezaji. 

Wakati jumuiya ya soka ikifuatilia kwa makini, vitendo vya Ramos na maamuzi yatakayofuata ya waamuzi bila shaka yataibua mjadala juu ya hitaji la uwajibikaji katika mchezo huo, na kuhakikisha kuwa matukio kama hayo yanashughulikiwa kwa haraka na kwa ufanisi. Athari za hali hii zinaenea zaidi ya Ramos pekee, na kuathiri mitazamo ya usalama wa wachezaji na uadilifu wa mchezo wenyewe.

MAGAZETI YA TZ YA LEO ALH MACH 20,2025...HAYA HAPA

 

Wednesday, March 19, 2025

MRADI WA TAZA MBIONI KUKAMILIKA - KAPINGA


...........................

๐Ÿ“Œ Unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Iringa hadi Sumbawanga

๐Ÿ“Œ Kapinga asema Mkoa wa Rukwa kuunganishwa na gridi ya Taifa kupitia mradi wa TAZA

๐Ÿ“Œ Serikali yatoa Bilioni 21.4 kwa ajili ya kulipa fidia wananchi

๐Ÿ“Œ Wananchi Wilaya ya Mufindi kunufaika na mitungi ya Ruzuku


Serikali imesema kuwa, itaukamilisha kwa wakatil mradi wa kuziunganisha na gridi ya Taifa mchi za Tanzania na Zambia (TAZA) unaohusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga kutokana na umuhimu wa mradi huo wa kuunganisha Mkoa wa Rukwa na gridi ya Taifa ambao hivi sasa unatumia umeme wa mafuta ya diseli. 

Hayo yameelezwa leo machi 19, 2025 na Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kukagua utekelezaji wa ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Kisada Iringa ambacho ni sehemu ya mradi huo.

"Miradi ambayo inafanyika na Serikali ya Awamu ya Sita kwa kweli ni miradi ya kimkakati, Mheshimiwa Rais aliahidi mkoa wa Rukwa nao kuingia kwenye gridi ya Taifa kupitia mradi huu". Amesema Mhe. Kapinga

Ameongeza kuwa, mradi wa TAZA ni muhimu katika kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme ndani ya Nchi huku akitolea mfano Mkoa wa Songwe ambao baadhi ya maeneo yyanapata umeme mkoa wa Mbeya na laini kuwa imetembea umbali mrefu hivyo kusababisha changamoto za upatikanaji wa umeme. 

Serikali imetoa takribani Shilingi Bilioni 21.4 kwa ajili ya malipo kwa
wananchi 6,279 ambao maeneo yao yamechukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa mradi.

Aidha, wananchi 5,929 sawa na asilimia 94.43 wamelipwa na Serikali inaendelea na malipo kwa wananchi waliobaki.

Kuhusu nishati safi ya kupikia Mhe. Kapinga amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Mufindi kunufaika na mradi wa mitungi ya Ruzuku ambayo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaitoa kwenye kila Wilaya nchini. 

Amesema kwa kila Wilaya kunamitungi takribani 3,255 ambayo itapatikana kwa bei ya ruzuku ya nusu bei ya shilingi 20,825 kutoka shilingi 45,000 kwa mtungi mmoja.

Mhe. Kapinga amesisitiza kuwa azma ya Serikali ni kuhakikisha umeme wa uhakika na unaotabirika unawafikia wananchi wote ili waweze kunufaika kwa shughuli za kiuchumi.