Argentina iliishinda Colombia 1-0 na kunyakua taji la kuvunja rekodi la 16 la Copa America lakini mchezo huo ulitatizwa kwa kucheleweshwa kwa dakika 80 kwa sababu ya matatizo nje ya uwanja huko Miami.
Lautaro Martinez alifunga bao katika kipindi cha pili cha muda wa nyongeza kutoka kwa krosi ya Giovani lo Celso .
Nahodha Lionel Messi alitokwa machozi alipolazimika kubadilishwa katikati ya kipindi cha pili baada ya kuumia alipokuwa akiutafuta mpira - lakini alikuwa akisherehekea michuano mikuu ya tatu mfululizo ya nchi yake wakati wa kipenga cha mwisho.
Mchezo wa kwanza ulicheleweshwa kwa sababu ya fujo nje ya Uwanja wa Hard Rock.
Waandalizi walisema mashabiki wasio na tiketi walijaribu kuingia uwanjani, na kuwaacha mashabiki wengine wakisubiri kwa saa nyingi kwenye joto la Miami ili milango ifunguliwe.
Mashabiki na maafisa wa polisi na usalama walikabiliana na kuwakamata kwa watu kadhaa. Wafuasi kadhaa walihitaji matibabu kutoka kwa wahudumu wa afya.
0 Comments