Header Ads Widget

Responsive Advertisement

DCEA yamtia mbaroni mtengenezaji Dawa za kulevya aina Heroin.

 


Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) inamshikilia Shaban Musa Adam (54) mkazi wa Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kutengeneza dawa za kulevya aina ya heroin kwa kutumia dawa tiba zenye asili ya kulevya na kuchanganya na kemikali bashirifu.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Kamisha Jenerali wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema mtuhumiwa baada ya kutengeneza dawa hizo husafirisha kwa kutumia mabasi ya abiria kama vifurushi kwenda mikoa mbalimbali nchini.

“Mtuhumiwa ameieleza Mamlaka kuwa siku za nyuma alikuwa akitengeneza dawa hizo za kulevya katika nchi za Bara la Asia kwenye magenge ya wazalishaji wa dawa hizo akitumika kama mbebaji wa dawa hizo na aliporejea hapa nchini aliendelea na uhalifu huo” Amesema Kamishna Lyimo.

Aidha ameongeza kuwa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya imekamilisha kanzi data ya wauzaji wakubwa wa dawa za kulevya na imeanza uchunguzi ambapo wengi wao wapo nje ya nchi.

Sambamba na hayo Mamlaka hiyo pia inamshikilia mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Mbaba Rabini Issa mtanzania aliyekamata uwanja wa Ndege wa Burundi akiwa na kilogramu 3.8 za skanka ambazo zilikuwa zimeshonewa na kufichwa kwenye begi la nguo akijiandaa kusafiri kuelekea Dubai.

Ameongeza kuwa katika operesheni wanazofanya kupitia ofisini za Kanda Mwanza, Dodoma, Mtwara na Mbeya wamekata gunia 285 za bangi kavu kilogram 350 za aina mbalimbali ya dawa za kulevya, milimita 115 za dawa tiba zenye asili ya kulevya pamoja na lita 16,523 za kemikali bashirifu zilizokuwa zinasambazwa kinyume na sheria ambapo watu 48 wamekamatwa kuhusika na uhalifu huo.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa hospitali ya Muhimbili Prof. Muhamed Janabi amesema ongezeko kubwa la wagonjwa wa Figo, saratani na tatizo la umeme wa moyo huchangiwa na matumizi ya dawa za kulevya ambazo hutengenezwa na dawa Kali na zile zilizoisha mda wake hivyo kusababishia watumiaji vifo vya ghafla.

Hata hivyo amesema licha ya serikali kujitahidi kuongeza hospital na matibabu ya wagonjwa badala ya kupunguza idadi ya wagonjwa inakuwa inaongezeka kutokana na matumizi ya dawa hizo hivyo ipo haja ya serikali kudhibiti watu wanaochanganya dawa ikiwemo zilizoisha muda wake kwani wanaongeza idadi ya wagonjwa na vifo vya ghafla hususani kwa vijana wadogo.

Katika hatua nyingine Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya kwa kuthamini na kutambua ushirikiano na Vyombo vingi vya ulinzi na Usalama wananchi na Mamlaka nyingine za kudhibiti dawa hizo wametoka tuzo kwa wadau mbalimbali ikiwemo Vyombo vya Habari taasisi za serikali na binafsi.




Post a Comment

0 Comments