Newcastle wako tayari kufufua tena mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 27 baada ya mazungumzo ya awali na Everton kugonga mwamba. (Football Insider)
Napoli bado wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku, 31. (Sky Sports)
Mshambuliaji wa zamani wa Italia, Manchester City na Liverpool Mario Balotelli, 33, anajadiliana kuhusu mpango wa kujiunga na Corinthians kama mchezaji huru, anasema mkurugenzi wa vijana katika klabu hiyo ya Brazil. (ESPN)
Barcelona wanakaribia kufikia hali ya kifedha ambayo itawawezesha kumnunua winga wa Athletic Bilbao Nico Williams, 22, kulingana na mkufunzi wa La Liga Javier Tebas. (Sport - kwa Kihispania)
Arsenal wanakaribia kufikia makubaliano ya kumnunua beki wa Italia na klabu ya Bologna Riccardo Calafiori mwenye umri wa miaka 22. (Football Insider)
Mlinda mlango wa Chelsea Mhispania Kepa Arrizabalaga, 29, yuko kwenye mazungumzo na Al-Ittihad kuhusu kuhamia Saudi Arabia. (Athletic - usajili unahitajika)
Kocha wa zamani wa Paris Saint-Germain Laurent Blanc anatarajiwa kuteuliwa kuwa meneja wa Al-Ittihad hadi Juni 2026. (Fabrizio Romano)
Mshambuliaji wa Tottenham na Jamhuri ya Ireland Troy Parrott, 22, anatazamiwa kufanyiwa uchunguzi wa matibabu kabla ya kuhamia AZ Alkmaar. (Football Insider)
Kiungo wa kati wa Ufaransa Desire Doue, 19, anatazamiwa kuamua kati ya Bayern Munich na Paris Saint-Germain ikiwa ataondoka Rennes msimu huu wa joto. (Sky Germany)
Tottenham pia wana nia ya kumleta Doue kaskazini mwa London. (Football.London)
Lyon wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa kundi la umri wa Southampton mwenye umri wa miaka 16 Alejandro Gomes Rodriguez. (Athletic - Usajili inahitajika)
Kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez, 29, amekubali kuondoka Atletico Madrid na kujiunga na Sevilla. (Fabrizio Romano)
0 Comments