Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Tanzania sekta ya sukari ni
kipaumbele katika kilimo kwa kuwa viwanda vya sukari ni vitovu vya kilimo na
uchumi.
Rais Dkt.Mwinyi aliyasema hayo alipofungua mkutano
wa wazalishaji sukari wa nchi za SADC katika ukumbi wa Hoteli ya Golden
Tulip iliopo uwanja wa ndege Zanzibar.
Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Tanzania imeweka mazingira
wezeshi ya uwekezaji katika kilimo cha Miwa na uzalishaji sukari.
Rais Dkt.Mwinyi ametoa rai kwa nchi za SADC kutumia
fursa zilizopo kwa kuweka mazingira bora zaidi ya uwekezaji ili kukuza
uzalishaji wa Sukari.
Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa
washiriki wa mkutano huo wa siku moja kuwekeza kikamilifu katika teknolojia za
kisasa na mbinu za kilimo za kisasa zinazoongeza tija ili kuboresha mavuno ya
miwa na uzalishaji sukari Afrika.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha
wazalishaji wa sukari Tanzania Seif Ali Seif amesema mkutano huo
utawasaida kuwa na sera a pamoja za kufikia malengo na kutatua changamoto
mbalimbali.
Waziri wa Viwanda na Biashara Selemani Jaffo
amesema serikali itaendelea kuwalinda wazalishaji wa sukari ili kuongeza
uzalishaji wa sukari.
Akimkarishisha rais wa Zanzibar na mwenyekiti
wa baraza la mapinduzi kufungua mkutano huo,waziri wa biashara na maendeleo ya
viwanda Omar Said Shaaban amesema kwa Zanzibar bado wanafasi kubwa ya
kuwakaribisha wawekezaji ili kuongeza mnyororo wa thamani.
Ni mkutano
wa Wazalishaji wa sukari wa nchi za sadec ambao pamoja na mambo mengine
unajadili masuala muhimu ya Sekta ya Sukari hususan, changamoto
katika Sekta na namna ya kuzipatia ufumbuzi wake, mkutano huo
umefunguliwa na rais wa Zanzibar dkt Hussein ali mwinyi ambae amesema mkutano
ho utasaidia kuimarisha mazingira wezeshi kwa maendeleo endelevu ya sekta ya
sukari katika nchi wanachama wa SADC.
0 comments:
Post a Comment