Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MNEC MWASELELA-CCM MBEYA KULINDA HESHIMA YA DKT.TULIA

 



MJUMBE  Halmashauri Kuu CCM Taifa (M-NEC)Mkoa wa  Mbeya ,Ndele Mwaselela amesema wataendelea kulinda heshima ya Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU)  Mbunge wa Mbeya mjini na Spika wa Bunge,DktTulia Ackson  na hawatakubali kuchonganishwa.

Mwaselela ametoa kauli  wakati wa hafla ya kukabidhi nyumba za wahitaji wawili ambao ni Daines Mbwiga,Solo   Mwantengule wakazi wa  Kata ya Isyesye  sambamba na viti mwendo viwili kwa walemavu.

Nyumba hizo zimejengwa na Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi wake  Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt.Tulia Ackson.

"Kama Chama hatufanyi majaribio wala hakitathubutu kufanya majaribio, hatuna mpango  tuna msimamo  ,binafsi  nasema siku zote na  hakuna mtu  wa kunibadilisha lazima tulinde heshima ya Mkoa "amesema.

 Amesema CCM hawana habari ya kuondoa heshima ya Dkt.Tulia na hawatakubali chama kichonganishwe kwa kuondoa heshima ya  nafasi Mbunge wa  IPU kwa  Nyanda za juu kusini .

"Sisi ndo wazazi wa Dkte.Tulia kung'aa kwake kwa ndio  chama cha mapinduzi kinazidi kung'aa hivyo asitokee mtu  hata kwa kupapasa awe ndani yetu awe nje yetu huyo  atakuwa halali yetu ,CCM mkoa wa Mbeya tumebahatika kupata Mhimili mmoja hivyo ni lazima tuulinde"amesema Mwaselela.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Isyesye Jijini Mbeya, Mbunge wa Jimbo la Mbeya na Spika wa Bunge na Rais umoja wa mabunge duniani,Dkt.Tulia Ackson amesema  kuwa mpaka Sasa ameweza kujenga nyumba 16 za wahitaji ambapo kati ya hizo mbili zimejengwa nje ya Mbeya.

Dkt amesema kuwa nyumba zilizokabidhiwa leo ambazo ni za wananchi wawili ambao walikuwa wakiishi katika mazingira magumu kwa kukosa makazi rasmi .

Meya wa Jiji la Mbeya ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Isanga ,DorMohamed amesema kuwa Dkt ni Mbunge makini na mnyenyekevu kwani ameleta  mkurugenzi  wa Jiji anayejitambua na kusimamia  vema miradi  yote ya maendeleo kikamilifu.


"Ndugu zangu wananchi msiruhusi sisimizi kuingia kwenye baraza la madiwani, tufanye kazi kwa uaminifu na kumsemea  mazuri aliyofanya  Dkt Tulia  hii tunu hatupaswi kuipoteza kamwe "amesema Meya huyo .


Post a Comment

0 Comments