Header Ads Widget

Responsive Advertisement

TAKUKURU SINGIDA YAOMBA VIONGOZI WA DINI,VYAMA VYA SIASA,NGO's KUTOA USHIRIKIANO MAPAMBANO YA RUSHWA

 


Na Thobias Mwanakatwe,SINGIDA 

TAASISI ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida imewataka viongozi wa dini, vyama vya siasa na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo ili kuweka mazingira mazuri yatakayowezesha uchaguzi kufanyika bila kuwepo na mazingira ya rushwa.

Naibu Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Singida, Petro Horombe, amesema hayo leo (Julai 31,2024) wakati akifungua semina kwa viongozi wa dini,vyama vya siasa,mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na waratibu wa uchaguzi kutoka halmashauri zote za mkoa huu.

"Kama mnavyofahamu nchi yetu tunaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu na uchahuzi mkuu utakaofanyika mwakani,sasa Takukuru kama mratibu wa mratibu wa kupambana na rushwa haiwezi kufanya mambo haya pekee bila ushirikiano inahitaji wadau muhimu katika jamii ili kukomesha rushwa," amesema Horombe

Amesema Takukuru inatambua kuwa viongozi wa dini na wa vyama vya siasa ni wadau muhimu sana katika kuzuia na kupambana na rushwa hasa katika uchaguzi ili vitendo vya rushwa ambavyo vimekuwa vikifanyika kipindi hiki viweze kukomeshwa.

"Tunatambua nafasi ya viongozi wa dini ni kubwa sana katika kushepu tabia za wananchi,tunatambua viongozi wa siasa ndio wamiliki wa wagombea kwa hiyo wana nafasi ya kuweka misingi mizuri kuepuka vitendo vya rushwa katika uchaguzi," amesema.

Horombe amesema katika kuhakikisha wananchi wana uelewa juu ya madhara ya rushwa imekuwa ikitoa semina na mikutano vijijini kuwaelimisha waepuke na vitendo vya rushwa anbavyo vinazorotesha maendeleo nchini.

Naye Afisa wa Takukuru, Joseph John, akiwasilisha mada kuhusu athari za rushwa kwa jamii, amesema rushwa imekuwa tatizo sana kipindi cha uchaguzi ambapo mgombea akifika kijijini tu wananchi wanamkimbilia awape rushwa.

"Wakati wa uchaguzi wananchi huwa wanaamini kuwa mgonbea asiyetoa rushwa huyo hafai, inabidi tuondoe dhana hii ili kufanya uchaguzi ulio huru na haki usiohusisha vitendo vya rushwa," amesema.


Post a Comment

0 Comments