UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umekabidhiwa vifaa vya kilimo na Kampuni ya Kichina ya AMEC Group.
Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano hayo leo Julai 19, 2024 jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mohammed Kawaida amesema vifaa hivyo lengo ni kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi pasipo kujali vyama vyao.
Amesema kuwa hadi wanavipata vifaa hivyo, ni kwamba waliituma Kamati ya Utekelezaji ya Vijana Taifa kwenda China kuona ni namna gani wanaweza kuwatafutia fursa vijana ambapo walimtuma Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Jokate Mwegelo.
Kawaida pia amesema wamepata wadau Chuo cha Sayansi cha China ambacho kitawekeza Nchini kwenye ujenzi wa maabara kubwa ya kisasa.
Kwamba Uwekezaji huo ukikamilika utakuwa ni Moja ya Uwekezaji makubwa kufanya na Jumuiya ya UVCCM.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Mwegelo, ameeleza kuwa vifaa hivyo vinagharimu zaidi ya shilingi milioni 200.
Ametaja vifaa hivyo kuwa ni Power Tiller 24 na mashine za kukobolea mpunga (Rice Meal 18) na kwamba juhudi hizi wanafanya ikiwa ni kuunga mkono maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kawekeza kwenye kilimo kama BBT.
Kwamba watachakata namba ya kuvigawa vifaa hivyo na kuwafikia wahitaji wa vifaa hivyo pasipokujali vyama vyao.
0 Comments