w
Mlipuko huo ulisababisha vifo vya takriban watu watano na wengine ishirini kujeruhiwa, kulingana na Polisi wa Somalia.
Katika taarifa iliyotumwa kwenye ukurasa wao wa Facebook, polisi walisema kuwa mlipuko huo ulisababishwa na gari lililojaa vilipuzi lililokuwa limeegeshwa nje ya mgahawa.
Bomu lililotegwa ndani ya gari lililipuka saa 10:28 usiku kwa saa za huko, kulingana na polisi.
Mmoja wa walionusurika katika mlipuko huo aliambia vyombo vya habari kwamba alikuwa ndani ya mkahawa huo akitazama mpira wakati mlipuko huo ulipotokea.
"Tulisikia mlipuko mkubwa na wa kutisha katika kipindi cha kwanza cha mchezo ambao tulikuwa tukitazama. Kila mtu alilazimika kufikiria jinsi ya kujiokoa baada ya muda mfupi," aliambia BBC mmoja wa walionusurika, Mohamed Muse.
"Niliona watu wakiwa hatarini, watu waliojeruhiwa wakipiga kelele kuomba msaada, na wengine walichanganyikiwa; ilikuwa inatisha," Mohamed Muse alisema
Al-Shabaab walidai kuhusika na shambulio hilo.
0 Comments