Simba SC imetangaza kumsajili Kiungo mpya Mkabaji Raia wa Nigeria, Augustine Okajepha (20) kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Rivers United ya Nigeria.
Okajepha ndio Mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Nigeria msimu wa 2023/2024 lakini alitajwa katika kikosi bora cha Wiki cha Kombe la Shirikisho Afrika mara mbili msimu ulioisha.
Simba SC sio tu wameamua kuamini Vijana bali Wachezaji bora baada ya Okajepha kuwa MVP wa pili kusajiliwa na Simba SC msimu huu baada ya Ahoua Jean Charles wa Ivory Coast.
0 Comments