Real Madrid wanavutiwa na beki wa Liverpool Trent Alexander-Arnold, Aston Villa wanataka pauni milioni 60 kutoka kwa Al-Ittihad kumuuza Moussa Diaby, Marseille wakubali dili la kumnunua Mason Greenwood wa Manchester United.
Real Madrid wana hamu ya kumsajili beki wa Uingereza Trent Alexander-Arnold, 25, ambaye amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake na Liverpool. (Talksport)
Manchester United hawana nia ya kumnunua kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate endapo wataamua kumfuta na Erik ten Hag. Badala yake, mkufunzi wa zamani wa Chelsea Thomas Tuchel anaonekana kupendelewa zaidi. (Mail)
Newcastle United wamesema watapambana kumbakisha mkufunzi wao Eddie Howe baada ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 46 kuhusishwa na tetesi za kuchukua nafasi ya Gareth Southgate aliyejiuzulu kama kocha wa Uingereza. (Guardian)
Aston Villa wanataka pauni milioni 60 kutoka kwa Al-Ittihad ikiwa klabu hiyo ya Ligi ya Saudi Pro inataka kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Moussa Diaby, 25. (Sportsport)
Manchester United wanajadiliana kuhusu masuala ya kibinafsi na wawakilishi wa mlinzi wa Ufaransa Leny Yoro baada ya kupokea ofa ya pauni milioni 52 iliyokubaliwa na Lille kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18, ambaye amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake. Yoro pia ananyatiwa na Real Madrid. (Guardian)
Marseille wamefikia makubaliano ya kimsingi ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Muingereza Mason Greenwood, 22. (The Athletic - usajili unahitajika)
0 Comments