MJUMBE wa Halmashauri kuu ya Chama Cha mapinduzi (CCM)Taifa Salim Abri Asas amepongeza kazi nzuri ya usimamizi wa ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Kising'a Jimbo la Ismani huku akitaka wenyeviti wa serikali za Vijijini na vitongoji waliofanya vizuri wasitolewe kwenye Uchaguzi.
Kuwa wapo baadhi ya viongozi ambao wamefanya kazi nzuri ya usimamizi wa Ilani ya CCM kuwa viongozi hao wasiachwe kwenye Uchaguzi wa serikali za Vijijini na Miata na Uchaguzi mkuu mwakani.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa ofisi ya Kisasa ya CCM kata ya Kising'a leo MNEC Asas alisema ujenzi wa ofisi hiyo na nyingine amezijengwa kwa Udhamini wa asilimia 100 kama njia ya kukiwezesha Chama kuwa na ofisi zenye heshima.
Hivyo Asas alisema viongozi wa kuchaguliwa ambao wameweza kutekeleza ilani vizuri kutoachwa kwenye Uchaguzi ujao na kutaka viongozi hao kuendelea kutekeleza ilani ya Chama Cha mapinduzi pamoja na kuhakikisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na CCM inapata kura za kutosha Uchaguzi ujao.
Kuhusu ujenzi wa ofisi hiyo kuwa ya kwanza ndani ya mkoa wa Iringa alisema kata ya Kising'a ni kata ambayo yeye ni mwelezaji na ndio sababu ya kuanza ujenzi wa ofisi ya kwanza kwenye kata hiyo na kata nyingine za wilaya ya Iringa Vijijini ambako tayari ofisi zimekamilika na sasa wilaya ya Kilolo,Mufindi na wilaya nyingine wameanza.
Wakati huo huo MNEC Asas ameahidi kukamilisha maboma ya shule ya msingi Kising'a ambayo Bado kukamilika na kuwa ujenzi huo ataukamilisha kabla ya Uchaguzi wa serikali za mitaa kufika ili kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira Bora zaidi.
0 Comments