Header Ads Widget

Responsive Advertisement

SERIKALI KUSIMAMIA KIKAMILIFU UJENZI WA BARABARA NA MADARAJA: RAIS SAMIA


Na Mwandishi wetu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa Serikali itahahakisha inasimamia Utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya barabara na madaraja iliyopo katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025 pamoja na kurejesha miundombinu iliyoathiriwa na mvua za El nino.

Rais Dkt. Samia ameeleza hayo leo Agosti 05, 2024 wakati akizungumza na wananchi wa Ifakara Wilaya ya Kilombero katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa CCM, Mkoani Morogoro.

“Mwaka huu na mwakani tunaendelea kutekeleza yale yaliyopo kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi lakini maombi yote mapya yaliyoletwa tutakwenda kuyaweka kwenye Ilani kwa uchaguzi ujao mbeleni”, amesema Dkt. Samia.

Dkt. Samia amesema kukamilika kwa barabara ya Kidatu - Ifakara kutasaidia usafiri na usafirishaji wa bidhaa za wakulima kupitia Programu ya Uendelezaji Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania - SAGCOT na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha inasimamia mpango huo ambao umeanza kuleta matokeo chanya kiuchumi.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa, ameeleza kuwa Serikali ilitoa Shilingi Bilioni 55 kwa ajili ya kukaabati miundombinu ya barabara iliyoathiriwa na mvua za El nino mkoani humo.

Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa kukamilika kwa mtandao wa barabara ya Kidatu - Ifakara (km 66.9) kwa kiwango cha lami ni mwanzo wa kuendeleza barabara hiyo itakayounganisha Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Njombe ambapo tayari Wizara ya Ujenzi imeshapatiwa Kibali cha kuanza utekelezaji wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 100.








Post a Comment

0 Comments