Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MARIAM MWINYI AKUTANA NA UJUMBE WA SHIRIKA LA ACTION AID

 

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi amesema  hakuna maendeleo endelevu na ya haraka endapo Wanawake hawatashirikishwa na kuwezeshwa Ipasavyo  Kiuchumi .


Mama Mariam Mwinyi ambae pia ni Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation amesema  hayo alipozungumza na  timu ya Watendaji wa Shirika la Action Aid Tanzania  Waliofika Ofisini  kwake Migombani, Mkoa wa Mjini Magharibi. 


Aidha Mama Mariam Mwinyi ameeleza kuwa bado kuna Kazi kubwa ya kufanya inayohitaji Ushirikiano wa Taasisi hizo mbili  Ili kuwainua Wanawake Kiuchumi Hususani Wakulima wa zao

 la Mwani.



Ameainisha eneo jengine la Ushirikiano kuwa ni  Mapambano dhidi ya Vitendo vya Udhalilishaji wa Jinsia  wanavyofanyiwa Wanawake na Watoto alilosema linahitaji kuwa na Mkakati Maalum wa kuwajengea Uwezo wa kupaza sauti zao na kutambua haki zao za Msingi.


Mama Mariam Mwinyi amefahamisha kuwa tatizo la muhali  ni  kubwa linaloikabili Zanzibar Katika  Juhudi za kukabiliana na Vitendo vya Udhalilishaji.


" Ninatamani kuona Watoto wote wanafundishwa kujua haki zao ili kuwalinda na Udhalilishaji" alisisitiza Mama Mariam.  


Akizungumzia Mradi wa Maji Safi na Salama  kwa Wanafunzi uliowasilishwa na Action Aid katika Kikao Kazi  hicho amesema ni Mradi Muhimu  utakaowahakikishia Wanafunzi Upatikanaji wa maji Salama  wakiwa Skuli pamoja na kuwalinda na Magonjwa yanayotokana na matumizi ya maji Yasio salama 


Ameihakikishia Action Aid Tanzania kuwa  Zanzibar Maisha Bora Foundation iko tayari kushirikiana nao  kufanya Kazi kwa Ukaribu zaidi kuyafikia Matarajio na Malengo ya Taasisi hizo ambayo yanafanana.

Post a Comment

0 Comments