Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, Bi. Ainess Anderson, akizungumza wakati wa
mafunzo ya elimu ya fedha kwa Watumishi wa Manispaa hiyo, yaliyotolewa na
Wataalamu wa Wizara ya Fedha, ikiwa imeambatana na wataalamu wengine
kutoka Taasisi za Serikali ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Kampuni ya
Uwekezaji ya UTT AMIS na NSSF pamoja na Taasisi za Kibenki ikiwemo TCB, CRDB,
NMB, NBC.Benki Kuu, yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Musoma, mkoani Mara.
Afisa Msimamizi wa Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Bi. Elizabeth Mzava, akielezea umuhimu wa kujiwekea akiba na kufanya uwekezaji kabla ya kustaafu kwa watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma ambapo walijitokeza kupata elimu ya fedha iliyotolewa na Wataalamu wa Wizara ya Fedha, pamoja na wataalamu wengine kutoka Taasisi za Serikali ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS na NSSF pamoja na Taasisi za Kibenki ikiwemo TCB, CRDB, NMB, NBC.Benki Kuu, yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, mkoani Mara.
Mkuu wa Kitengo cha
Usafi na Udhibiti Taka Halmashauri ya Manispaa ya Musoma Bw. Mwizarubi Nyaindi,
akiuliza swali kuhusu utaratibu wa kujiunga na Hazina Saccos wakati wa mafunzo
ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wataalamu wa Wizara ya Fedha, ikiwa
imeambatana na wataalamu wengine kutoka Taasisi za Serikali ikiwemo Benki
Kuu ya Tanzania (BoT), Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS na NSSF pamoja na
Taasisi za Kibenki ikiwemo TCB, CRDB, NMB, na NBC, yaliyofanyika katika
ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, mkoani Mara.
Meneja Maendeleo ya Biashara wa Benki ya CRDB-Musoma, Bw. Denis Ndagara, akitoa elimu ya umuhimu wa kukopa katika Taasisi rasmi zinazotambuliwa na Serikali kwa watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma ambapo walijitokeza kupata elimu ya fedha iliyotolewa na Wataalamu wa Wizara ya Fedha, pamoja na wataalamu wengine kutoka Taasisi za Serikali ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS na NSSF pamoja na Taasisi za Kibenki ikiwemo TCB, CRDB, NMB na NBC.Benki, yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, mkoani Mara.
Baadhi ya Watumishi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, wakifuatilia mafunzo ya elimu ya fedha
yaliyotolewa na Wataalamu wa Wizara ya Fedha, ikiwa imeambatana na
wataalamu wengine kutoka Taasisi za Serikali ikiwemo Benki Kuu (BoT), Kampuni
ya Uwekezaji ya UTT AMIS na NSSF pamoja na Taasisi za Kibenki ikiwemo TCB,
CRDB, NMB na NBC, yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa
ya Musoma, mkoani Mara.
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, wakiangalia filamu iliyokuwa na mada mbalimbali ikiwemo masuala ya mikopo, akiba, uwekezaji, kujiandaa kustaafu wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wataalamu wa Wizara ya Fedha, ikiwa imeambatana na wataalamu wengine kutoka Taasisi za Serikali ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS na NSSF pamoja na Taasisi za Kibenki ikiwemo TCB, CRDB, NMB na NBC, yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, mkoani Mara.
(Picha na Kitengo cha
Mawasiliano WF, Mara)
...........................
Na. Josephine Majura
WF, Mara
Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, Bi. Ainess Anderson, amezikaribisha Taasisi
mbalimbali zinazojihusisha na masuala ya fedha kwenda kutoa elimu ya fedha
ikiwemo uwekezaji na matumizi sahihi ya mikopo kwa wananchi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Musoma.
Alitoa wito huo wakati
wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha, Taasisi za
Serikali na Binafsi kwa Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma ili
waweze kujikwamua kiuchumi.
“Tunawakaribisha muda
wowote kuja kutoa elimu hii muhimu kwa watumishi na wakazi wa Halmashauri yetu
ili waweze kuwa na uelewa mpana wa masuala ya fedha”, alisema Bi. Ainess.
Aliongeza kuwa Taasisi
za Fedha zinatakiwa kuchangamka kutafuta wateja maeneo yote nchini hivyo
wasikae ofisini hadi wakisikia Wizara ya Fedha inaenda kutoa elimu ndipo nao
watoke ofisini waambatane nao.
“Wametoa mada nzuri
ikiwemo aina za mikopo inayotolewa, vigezo vya kutambua Taasisi rasmi za
kukopa, uwekaji wa akiba, kwakweli mada za leo zimetujengea uelewa mpana
wa masuala ya fedha, hivyo niwaombe na niwasisitize mrudi tena kwa wananchi
wetu ili elimu hii nzuri kila mwananchi aipate iweze kumsaidia katika shughuli
za kila siku za kiuchumi”, alisisitiza Bi. Ainess.
Naye mmoja wa
washiriki wa mafunzo hayo ambae ni Mtumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Musoma, Bw. Juma Njwayo, ,alisema kuwa amepata elimu ya masuala ya fedha katika
maeneo mbalimbali ikiwemo namna ya kuweka akiba, mikopo, Taasisi rasmi za
kuchukulia mikopo na namna bora ya kujiandaa kabla ya kustaafu.
Kwa upande wake Afisa
Msimamizi wa Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Bi.
Elizabeth Mzava, alisema kuwa katika mkoa wa Mara wamepata mwitikio mkubwa wa
wananchi kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya fedha.
“Tunaendelea kuwaomba
wananchi tunapoendelea na zoezi la kutoa elimu ya fedha waendelee kujitokeza
kwa wingi kupata elimu hiyo ili wawe na uelewa mpana wa masuala ya
fedha”, alisema Bi. Elizabeth.
Katika zoezi la kutoa elimu kwa wananchi Timu ya Wataalamu wa Wizara ya Fedha imeambata na Wataalamu kutoka Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS na NSSF pamoja na Taasisi za Kibenki ikiwemo TCB, CRDB, NMB na NBC.
0 Comments