....................
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imetangaza msimu wa Tuzo ya Waandishi wa Habari walioripoti taarifa na kuandaa makala mbalimbali kuhusu kazi na majukumu ya TMDA katika kipindi cha mwaka 2025.
Kazi hizo ni zile zilizotoka kuanzia Julai, 2024 mpaka Machi 2025.
Taarifa ya Mamlaka hiyo kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Jumanne, Machi 18, 2025 imesema kuwa lengo la Tuzo hizo ni kutambua mchango wa waandishi wa habari na kuleta hamasa katika kuelimisha jamii kuhusu masuala ya udhubiti wa Dawa na Vifaa Tiba, Vitendanishi na bidhaa za Tumbaku kupitia vyombo vya habari ili kulinda afya ya jamii.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kazi zitakazolengwa ni zile zilizoripotiwa kupitia Runinga, Radio, Magazeti na Mitandao ya Kijamii kwa kipindi tajwa.
"TMDA inawaalika waandishi wote wa habari kushiriki Tuzo hizi kwa kuwasilisha kazi zao ifikapo au kabla kabla ya Aprili 18, 2025 kupitia anuani ya barua pepe ya commpedtmda@gmail.com au kwa njia ya CD katika ofisi za TMDA zilizopo Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Mtwara, Tabora na Geita.
Tags
Top Stories