JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Jumatatu, 7 Julai 2025

RAIS WA ZANZIBAR ATEMBELEA BANDA LA ETDCO KWENYE MAONESHO YA 49 YA SABASABA

wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO) wakiongozwa na Kaimu Meneja, CPA. Sadock Mugendi wakimkabidhi zawadi  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam Sabasaba leo Juni 7, 2025 na kujionea jinsi  inavyotekeleza miradi mbalimbali ya umeme nchini (PICHA NA NOEL RUKANUGA)

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bw. Lazaro Twange (kulia) akisalimiana na Kaimu Meneja Kampuni ya ETDCO CPA. Sadock Mugendi wakati akitembelea banda la kampuni hiyo lililopo ndani ya Banda la TANESCO  katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam Sabasaba.

Afisa Uhusiano wa Kampuni ya ETDCO Bi. Samia Chande akitoa elimu kwa wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme.Kaimu Meneja Kampuni ya ETDCO, CPA Sadock Mugendi, akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo leo, Julai 7, 2025, katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam.

.....

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo 7 Julai 2025, ametembelea banda la Kampuni ya ETDCO katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam na kujionea namna Kampuni hiyo inavyotekeleza miradi mbalimbali ya umeme nchini.

Akiwa katika banda hilo, Mhe. Rais Dkt. Mwinyi amekabidhi zawadi ya sikukuu ya Sabasaba kwa wafanyakazi wa ETDCO wakiongozwa na Kaimu Meneja wa Kampuni hiyo, CPA. Sadock Mugendi.

Akizungumza na kuhusu na ushiriki wao katika maonesho hayo, CPA. Mugendi amesema kuwa lengo la ETDCO kushiriki meonesho ya sabasaba ni kuonesha utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya umeme nchini.

CPA. Mugendi ameeleza kuwa Kampuni hiyo imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya usafirishaji umeme, ikiwemo mradi wa kusafirisha umeme wa kilovolti 132 kutoka Tabora hadi Katavi, ambao umewezesha wananchi wa maeneo hayo kupata umeme wa uhakika.

Aidha, amebainisha kuwa wameweza kukamilisha mradi mwingine wa kilovolti 132 kutoka Tabora Mjini hadi Urambo, wenye urefu wa kilomita 115, umeendelea kuimarisha upatikanaji wa umeme katika Mkoa huo.

"Tunawakaribisha wananchi wote kutembelea banda letu la ETDCO lililopo ndani ya banda la TANESCO. Lengo letu ni kuwaonesha wadau namna tunavyotekeleza miradi mbalimbali ya umeme kwa lengo la kuhakikisha watanzania wanafikiwa na huduma nchi zima," amesema CPA. Mugendi.

Ameongeza kuwa kampuni hiyo imefanikiwa kutekeleza miradi ya REA katika Mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Arusha, Katavi, Mbeya, Geita, pamoja na Kigoma.

CPA. Mugendi ameeleza kuwa utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa kusafirisha umeme kutoka Urambo – Nguruka – Kigoma, utakuwa wa kilovolti 132 wenye urefu wa kilomita 260.

Ameongeza kuwa mafanikio haya ni matokeo ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita, inayolenga kuhakisha watanzania wanafikiwa na huduma bora ya umeme nchini.

Mwisho.

0 comments:

Chapisha Maoni

Listen Mkisi Radio