JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Jumatano, 9 Julai 2025

WATU ZAIDI YA LAKI 6 WATEMBELEA BANDA LA MALIASILI, SABASABA 2025

 

.................

Na Sixmund Begashe 

Witikio wa watu kwenye Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye Maonesho ya Biashara ya 49 ya Kimataifa yajulikanayo kama SABASABA umezidi kuwa mkubwa kutokana na mvuto wa huduma nzuri zinazotolewa na Idara na Taasisi zake, na kwa mujibu wa Bodi ya Utalii nchini hadi tarehe 8 Julai 2025, watu zaidi ya  laki 6 na sitini wameshatembelea banda hilo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania, Afisa Masoko Mwandamizi Bi. Flaviana Moshi amebainisha kuwa witikio huo unatokana na maandalizi mazuri yaliyofanywa na Wizara hiyo kupitia Bodi ya Utalii. 

Ameongeza kuwa licha ya huduma zingine wanazozipata kwenye Idara na taasisi za Wizara kama za utafiti, Malikale  pia kwenye banda hilo watu wanafanya Utalii wa Wanyamapori hai, wanapata bidhaa za Misitu na nyuki.

Naye Mzee Rashidi Jumanne, mkazi wa Bangala amesema licha ya kuwaona wanyama, amefurahishwa na utaratibu wa Wizara hiyo kuhakikisha watu wanapata huduma ya nyama ya Wanyamapori,  na vyakula mbalimbali.

"Nimefundishwa pale kwenye meza ya Chuo cha Utalii namna ya maandalizi ya meza ya chakula kwa wageni, nimekula nyama choma ya swala, nimeondoka na miche yangu ya miembe, naenda kupanda nyumbani". Alisema mzee Rashidi

Maonesho hayo ya SABASA yalianza tarehe 28 Juni 2025 na yanatarajiwa kufikia tamati tarehe 13 Julai 2025.







0 comments:

Chapisha Maoni

Listen Mkisi Radio