JSON Variables

Thursday, March 20, 2025

MAGAZETI YA TZ YA LEO ALH MACH 20,2025...HAYA HAPA

 

Wednesday, March 19, 2025

MRADI WA TAZA MBIONI KUKAMILIKA - KAPINGA


...........................

📌 Unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Iringa hadi Sumbawanga

📌 Kapinga asema Mkoa wa Rukwa kuunganishwa na gridi ya Taifa kupitia mradi wa TAZA

📌 Serikali yatoa Bilioni 21.4 kwa ajili ya kulipa fidia wananchi

📌 Wananchi Wilaya ya Mufindi kunufaika na mitungi ya Ruzuku


Serikali imesema kuwa, itaukamilisha kwa wakatil mradi wa kuziunganisha na gridi ya Taifa mchi za Tanzania na Zambia (TAZA) unaohusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga kutokana na umuhimu wa mradi huo wa kuunganisha Mkoa wa Rukwa na gridi ya Taifa ambao hivi sasa unatumia umeme wa mafuta ya diseli. 

Hayo yameelezwa leo machi 19, 2025 na Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kukagua utekelezaji wa ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Kisada Iringa ambacho ni sehemu ya mradi huo.

"Miradi ambayo inafanyika na Serikali ya Awamu ya Sita kwa kweli ni miradi ya kimkakati, Mheshimiwa Rais aliahidi mkoa wa Rukwa nao kuingia kwenye gridi ya Taifa kupitia mradi huu". Amesema Mhe. Kapinga

Ameongeza kuwa, mradi wa TAZA ni muhimu katika kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme ndani ya Nchi huku akitolea mfano Mkoa wa Songwe ambao baadhi ya maeneo yyanapata umeme mkoa wa Mbeya na laini kuwa imetembea umbali mrefu hivyo kusababisha changamoto za upatikanaji wa umeme. 

Serikali imetoa takribani Shilingi Bilioni 21.4 kwa ajili ya malipo kwa
wananchi 6,279 ambao maeneo yao yamechukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa mradi.

Aidha, wananchi 5,929 sawa na asilimia 94.43 wamelipwa na Serikali inaendelea na malipo kwa wananchi waliobaki.

Kuhusu nishati safi ya kupikia Mhe. Kapinga amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Mufindi kunufaika na mradi wa mitungi ya Ruzuku ambayo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaitoa kwenye kila Wilaya nchini. 

Amesema kwa kila Wilaya kunamitungi takribani 3,255 ambayo itapatikana kwa bei ya ruzuku ya nusu bei ya shilingi 20,825 kutoka shilingi 45,000 kwa mtungi mmoja.

Mhe. Kapinga amesisitiza kuwa azma ya Serikali ni kuhakikisha umeme wa uhakika na unaotabirika unawafikia wananchi wote ili waweze kunufaika kwa shughuli za kiuchumi.

MSD YAFANYA MAPINDUZI MKUBWA SEKTA YA AFYA MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA

..........................

Mkurungenzi wa Bohari ya Dawa nchini (MSD), Mavere Tukai amesema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu amefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya  na kuiweka nchi katika viwano vya juu.

Tukai amesema hayo leo Jumatano Machi 19, 2025 alipokuwa akizungumzia mafaniko ya miaka minne ya Rais Dkt. Samia Suliu Hassan tangu aingie madarakani katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo),jijini Dodoma ikiwa ni utaratibu uliowekwa na ofisi ya Msemaji wa Serikali.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Tukai, tangu Rais Samia aingie  madarakani amewezesha upatikanaji wa bidaa za afya na hadi kufikia mwaka huu, jumla ya bidhaa asiria 382 zilisambazwa  kutoka 290 za awali sawa na ongezeko la  asilimia 42 mwaka 2021/22 hadi asilimia 67 mwezi Februari 2024/25 sawa na  ongezeko la asilimia 23.

"Lengo letu ifikapo mwisho wa mwaka wa fedha 2054/2025 tufike asilimia 80 mpaka 90 na kwa mwendo huu tunaoenda nao hilo linawezekana kwani sasa tumeshavuka lengo. "

Alisema kwa kipindi cha miaka minne ya Rais Samia, MSD imefanya manunuzi na usambazaji wa vifaa na vifaa tiba vinavyohitajika katika vituo vya kutolea huduma za afya kuanzia ngazi ya msingi hadi vituo vinavyotoa huduma za kibingwa na ubingwa bobozi nchini. 

Alisema baadhi ya vifaa vilivyosambazwa ni pamoja na mashine za usingizi, CT-Scan, MRI 3T, Utrasound na Digital X-Ray vyenye thamani ya Sh376. 6 bilioni. 

Akizungumzia uwekewazaji uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kupunguza vifo vya mama na mtoto Mkurugenzi Mavere alisema MSD inajivunia kwa kuwezesha maono ya Rais Samia ya kupunguza vifo hivyo hadi kufikia 104 vya sasa  kutoka 556 vilivyokuwa vikitokea awali na kuwezesha kiongozi huyo kutambulika kimataifa na kupewa Tuzo. 

"MSD jukumu letu lilikuwa ni kupeleka vifaa tiba, tumetekeleza kwa asilimia 100 katika miradi ya unuinuzi wa vifaa vya dharura , uzazi pinamizi na huduma za watoto wachanga (CE)mONC) ambako vituo 316 vya kutolea huduma za afya vilinufaika kwa Sh100 bilioni. Mpaka sasa usambazaji huo umefikia asilimia 100," aliisisitiza Tukai. 

Tukai alisema fedha zote zilizowekezwa katika kipindi kifupi cha miaka minne  zinalengo la kuboresha huduma ya afya kwa wananchi. 

Kwa upande wa miradi inayohusisha magonjwa ya TB, HIV na Malaria, Mkurugenzi Tukai alisema  kwa kipindi cha mwaka 2021 mpaka 2023  MSD imefikia asilimia 95 ya malengo.

Kuhusu usambazaji wa vyandarua ili kujinga na ugonjwa wa maralia Tukai alisema jumala ya vyandarua milioni 7.2 vilisambazwa. 

"Mwaka 2023/2024 tulisambaza vyandarua  milioni tisa sawa na ongezeko la zaidi ya asilimia 30.

Alisema kuhusu vifaa tiba mwaka 2020 jumla ya Sh18 bilioni zilitumika  na mwaka uliofuatia zilitumika Sh56 bilioni wakati mwaka 2024 jumla ya Sh93 bilioni zilitumika.

" Hivi tunavyoongea yaani mwezi Machi , tayari zimeshatumika Sh109  ikiwa  bado miezi kadhaa kabla ya kumaliza mwaka wa fedha wa 2024/25.

Tukai alisema mafanikio yote hayo yametokana na uwekezaji wa Serikali chini ya Rais Samia na kwamba MSD wanapotumwa wanatekeleza kwa lengo la kuwapa huduma bora wananchi. 

"MSD pia imeboresha upatikanai wa huduma bora ya kinywa na meno kwa kununua viti vya kinywa na meno 693 pamoja na mashine zake za mionzi 533 kwa gharama ya Sh13 bilioni. 

Alisema sasa huduma hiyo imesogezwa karibu na wananchi zikiwa na ubora unaokubalika kuanzia ngazi ya kituo cha afya, wilaya, mkoa, rufaa mpaka Taifa.