JSON Variables

Tuesday, March 25, 2025

RAIS SAMIA ASHIRIKI MKUTANO WA PAMOJA SADC NA EAC ULIOFANYIKA KWA JIA YA MTANDAO


................

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 24 Machi, 2025 Ikulu ndogo ya Mkanyageni, Chake Chake, mkoa wa Kusini Pemba.

Mkutano huu ni wa pili kufanyika baada ya ule wa kwanza uliofanyika tarehe 08 Februari, 2025 Ikulu, Jijini Dar es Salaam na ulihudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali wafuatao:-

Rais William Ruto wa Kenya, Dkt. Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais Lazarus Chakwera wa Malawi, Rais Andry Rajoelina wa Madagascar, Rais Hakainde Hichilema wa Zambia, Dkt. Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Waziri Mkuu wa Somalia pamoja na Mawaziri kutoka Sudani Kusini na Angola.

 

Monday, March 24, 2025

WIZARA YA NISHATI YATAJA VIPAUMBELE VYA BAJETI YA MWAKA 2025/2026


................

πŸ“Œ Rukwa, Kagera, Lindi. Mtwara kuunganishwa na gridi ya Taifa.

πŸ“Œ Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kuendelea kuhamasishwa

πŸ“Œ Serikali kuendelea kuimarisha utendaji wa Taasisi, Mashirika  chini ya Wizara ya Nishati,

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametaja  vipaumbele vya Wizara  ya Nishati katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 ikiwemo kuendelea kutekeleza miradi ya uzalishaji, usafirishaji,  usambazaji  umeme na kufikisha gridi ya Taifa katika Mikoa iliyosalia ya Rukwa, Kagera, Lindi na Mtwara;

Akiwasilisha vipaumbele hivyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Njshati na Madini, leo jijini Dodoma, Dkt. Biteko amesema  vipaumbele hivyo vimezingatia mpango wa Taifa wa Nishati wa mwaka 2025 hadi 2030.

“Mhe. Mwenyekiti vipaumbele hivi vimezingatia mpango wa Taifa wa Nishati wa mwaka 2025 - 2030 (National Energy Compact 2025 - 2030) utakaosaidia upatikanaji na uunganishaji wa umeme kwa wananchi, kuongeza mchango wa nishati jadidifu katika uzalishaji wa umeme na ushiriki wa Sekta Binafsi katika maendeleo ya Sekta ya Nishati ”. Amesema Dkt. Biteko

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesema Serikali imewajengea wazawa uwezo mkubwa wa kutekeleza miradi ya umeme huku akitolea mfano wa ajira kwenye miradi ya umeme kufikia idadi ya  53,000.

Amesema  Dunia inahitaji nishati na mahitaji ya umeme yamekuwa yakiongezeka kwa kasi hivyo Serikali itaendelea kuongeza vyanzo vya kuzalisha umeme ili kukidhi mahitaji ya Watanzania.

Awali, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Nishati, Petro Lyatuu alisema kuwa katika kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa umeme wa uhakika Wizara itaendelea kuimarisha Gridi ya Taifa (National Grid Stabilization Project) pamoja na kufanya matengenezo na ukarabati wa mitambo ya kuzalisha umeme;

“Mhe. Mwenyekiti tutandelea na usambazaji wa nishati katika Vitongoji, maeneo ya migodi, kilimo, viwanda na pampu za maji pamoja na vituo vya afya ili kuwezesha shughuli za
uzalishaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.” Aliongeza Lyatuu

Kuhusu Nishati Safi ya Kupikia Lyatuu alisema Serikali itaendelea kuhamasisha na kuwezesha watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ikiwa ni utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034) na mpango wa Taifa ya Nishati wa mwaka 2025 - 2030 (National Energy Compact 2025 - 2030).

Aliongeza  kuwa Serikali itaendelea na shughuli za utafutaji, uendelezaji na usambazaji wa mafuta na gesi asilia pamoja na kutekeleza miradi ya kielelezo na kimkakati ya mafuta na gesi asilia
ikiwemo Mnazi Bay Kaskazini, Eyasi - Wembere, pamoja na mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi asilia kuwa Kimiminika (Liquefied Natural Gas - LNG Project).

Mradi mwingine ni ujenzi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania (East African Crude Oil Pipeline - EACOP).

Vile vile, amesisitiza kuwa Serikali itaendela kuimarisha utendaji wa Taasisi na Mashirika yaliyo chini ya Wizara ya TANESCO, REA, TPDC, PBPA, EWURA na PURA pamoja na Kampuni Tanzu ili yatoe huduma bora kwa wadau, kuimarisha mapato pamoja na tija na ufanisi katika uendeshaji;

Amesema lengo lingine ni kuongeza  kiwango cha upatikanaji wa umeme kutoka cha sasa cha asilimia 78.4 hadi kufikia asilimia 100 ifikapo mwaka 2030.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. David Mathayo ameipongeza Serikali kwa kuja na vipaumbele vitakavyowawezesha watanzania kuwa na nishati ya uhakika.

WATAALAM OFISI YA MSAJILI HAZINA WAJIFUNGIA KUCHAMBUA BAJETI


..............


Na mwandishi wa OMH

Dar es Salaam. Timu ya wataalamu 53 kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH), imejifungia kufanya uchambuzi wa mipango na bajeti za taasisi na mashirika ya umma, kazi ambayo ni muhimu katika kuhakikisha usimamizi mzuri wa rasilimali za serikali.

Joseph Mwaisemba, Mkurugenzi Msaidizi wa Usimamizi wa Mashirika yasiyo ya kibiashara, Ofisi ya Msajili wa Hazina, alisema timu hiyo itaanza vikao vyake leo Jumatatu, Machi 24, 2025 kwa muda ya wiki mbili.

Mkurrugenzi huyo amesdma uchambuzi wa bajeti za mwaka wa fedha 2025/26 unahusisha taasisi za umma 252.

“Zoezi la uchambuzi linalofanyika katika Shule ya Uongozi Mwalimu Nyerere, ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha kwamba fedha za umma zinatumika kwa njia bora na yenye ufanisi,” alisema.
Ili kufanikisha lengo lililokusudiwa na kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 10(2) (c) cha Sheria ya Msajili wa Hazina SURA 370 na kifungu cha 17(a) cha Sheria ya Bajeti SURA 439, OMH inatakiwa kufanya uchambuzi wa mipango na bajeti ya Taasisi na Mashirika ya umma yaliyochini yake.

Lengo lake ni kuidhinisha mikakati, mipango ya mwaka ya Taasisi na Mashirika ya umma na kuijumuisha katika Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa ajili ya usimamizi wa utekelezaji na kugharamiwa.

“Utekelezaji wa maelekezo ya Mwongozo huu kwa ukamilifu utachangia: udhibiti wa matumizi ya fedha za umma na kuleta tija iliyokusudiwa,” alisema Bw. Mwaisemba, ambaye pia ni msimamimizi wa zoezi la uchambuzi wa bajeti.

Aidha, alisema utekelezaji utapelekea kuongezeka kwa ushiriki wa sekta binafsi kwenye shughuli za uwekezaji na biashara na kutoa fursa sawa za ajira kwa wote.

Sanjari na hilo, alisema utekelezaji wa maelekezo ya muongozo utapelekea  kuendelea kuimarika kwa utoshelevu wa chakula nchini na kuongeza upatikanaji wa huduma za jamii kwa wote.

 Pia, matokeo tarajiwa (faida kwa Serikali, OMH na mashirika husika) ni pamoja na:  Kuongeza rejesho la uwekezaji wa mashirika ya umma kwa Serikali kupitia makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi, ulipaji wa kodi, utoaji wa huduma, na ajira.

Uwekezaji wa serikali katika taasisi, mashirika ya umma na wakala za serikali 252 ni Sh83.4 trilioni, ambao ni uthibitisho wa dhamira ya serikali katika kuimarisha sekta mbalimbali za uchumi na kuhakikisha kwamba huduma muhimu zinapatikana kwa wananchi.

Sambamba na kuongeza rejesho la uwekezaji wa serikali, inatarajiwa kushuhudiwa kuimarika kwa utawala bora, kuongezeka kwa ufanisi kwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, pamoja na kuelekeza rasilimali katika maeneo yenye tija ambayo yatachangia katika ukuaji wa uchumi.
Serikali inatoa Mwongozo wa Mpango na Bajeti ambao unaandaliwa kwa mujibu wa Kifungu Na. 21 cha Sheria ya Bajeti, Sura 439. 

Mwongozo huo unalenga katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 (TDV 2025) pamoja na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, na utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi ya Mwaka 2020.

Maeneo yanayopewa kipaumbele ni pamoja na maelekezo kuhusu ulazima wa kuzingatia vipaumbele vya mpango; maelekezo ya ujumla kuhusu uandaaji wa Mpango na Bajeti; na maelekezo mahususi kwa mashirika na taasisi za umma.

Vigezo vinavyotumika katika uchambuzi wa mipango na bajeti ni pamoja na: i. Utekelezaji wa maelekezo mahususi ya Serikali yaliyotolewa katika mwongozo wa mpango na bajeti wa Serikali katika mwaka husika. ii. Vigezo vya kupima utendaji wa taasisi na mashirika ya umma ambayo vinahusu masuala ya kifedha, rasilimali watu, utawala bora, huduma kwa wateja, na utekelezaji wa majukumu ya msingi ya taasisi.

Matokeo tarajiwa (faida kwa Serikali, OMH na mashirika husika) ni pamoja na:  Kuongeza rejesho la uwekezaji wa mashirika ya umma kwa Serikali kupitia makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi, ulipaji wa kodi, utoaji wa huduma, na ajira.

Pia inatarajiwa kushuhudiwa kuimarika kwa utawala bora, kuongezeka kwa ufanisi kwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, pamoja na Kuelekeza rasilimali katika maeneo yenye tija ambayo yatachangia katika ukuaji wa uchumi.

Bw. Mwaisemba alitoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano wa karibu kutoka kwa wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi, Menejimenti, na watumishi wa taasisi na mashirika ya umma. 

"Tunahitaji tushirikiane kwa pamoja kuhakikisha malengo ya serikali ya uanzishwaji wa mashirika hayo yanafikiwa ili yaweze kuchangia katika maendeleo ya nchi yetu," alisema. 

Hii ni muhimu hasa katika kipindi hiki ambapo dhamira ya serikali ni kuondokana au kupunguza utegemezi wa wadau wa maendeleo katika kutekeleza majukumu yake.




 

URENO YAISAMBARATISHA DENMARK IKITINGA NUSU FAINALI KIBABE

 Timu ya Taifa ya Ureno chini ya Kapteni Cristiano Ronaldo imefanikiwa kutinga nusu fainali ya Ligi ya Uropa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-3 dhidi ya Denmark. Mchezo huo mgumu uliopigwa dimba la EstΓ‘dio JosΓ© Alvalade nchini Ureno uliibua hisia kwa mashabiki wa soka duniani kote baada ya Cristiano Ronaldo kukosa penati muhimu lakini alisahihisha makosa hayo na kufunga bao muhimu.


Tathmini ya Mchezo

Ureno waliingia vichwa chini katika mchezo huo baada ya kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza kwa bao 1-0 nchini Denmark  kwa bao la mshambuliaji kinda Hojlund. Ureno walianza mchezo huo kwa mashambulizi makali na kujipatia penati dakika ya 6 lakini mpigaji  Cristiano Ronaldo alishindwa kufunga baada ya golikipa wa Denmark Kasper Schmeichel kudaka mpira mwepesi.

Ureno walizidisha mashambulizi na dakika ya 38 Joachim Andersen wa Denmark alijifunga na kuwafanya Ureno kwenda mapumziko kwa bao 1-0. Dakika ya 56 Rasmus Kristen wa Denmar  alifanikiwa  kusawazisha bao.

Dakika ya 72 Ronaldo alirejesha furaha kwa mashabiki wa Ureno kwa kufunga bao la pili na kusawazisha makosa ya kukosa penati lakini Cristien Eriksen alisawazisha bao hilo dakika ya 76 na matokeo kuwa 2-2.

Kocha wa Ureno alifanya mabadiliko kwa kuwatoa washambuliaji wote wakiongozwa na Ronaldo ,Rafael Leao na na kuwapa nafasi Trincao aliyefunga mabao mawili ya dakika ya 86 na 91kisha bwana mdogo goncalo Ramos kufunga bao la 5 dakika ya 115 na kuwaondosha Denmark kwenye michuano hiyo.

Matokeo hayo yanawafanya Ureno kutinga nusu fainali ya Ligi ya ulaya wakichuana na Ujerumani katika hatua hizo,kama watashinda mchezo huo basi watatinga fainali ya michuano hiyo

Sunday, March 23, 2025

URITHI WA MALIKALE NCHINI NI TUNU ADHIMU: DKT ABBASI

....................

Na Sixmund Begashe -Njombe

Wanaosimamia maeneo ya Malikale nchini wametakiwa kuongeza kasi ya uhifadhi na uendelezaji wa maeneo ya urithi huo kwani ni kielelezo muhimu cha kurithisha kizazi cha sasa tunu muhimu za Taifa ambazo zimeasisiwa na waasisi wa taifa wakiongozwa na Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi, Mkoani Njombe, kwenye kikao kazi cha Wizara hiyo na taaasisi zilizokasimishwa maeneo ya Malikale, lengo likiwa ni kujenga uelewa wa pamoja na kupanga mikakati ya Uhifadhi na uendelezaji endelevu wa maeneo hayo.

Dkt. Abbasi amesema Serikali ilikabidhi maeneo hayo kwenye taasisi hizo kwa dhamira kubwa ili yahifadhiwe vyema na kuendelezwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

"Nchi yetu imejaliwa kuwa na urithi adhimu na adimu wa Malikale, ambao ni wa kipekee ukiwa ni alama muhimu za kihistoria Duniani, hivyo ni lazima tuhakikishe maeneo haya yanahifadhiwa vyema na kutangazwa ili yazidi kulinufaisha Taifa"Alisema Dkt. Abbasi

Dkt. Abbasi ameongeza kuwa matumizi ya urithi huo wa Malikale ni pamoja na kuelimisha jamii hasa kizazi cha sasa hususani juu ya historia ya nchi, utu, umoja wa kitaifa, mshikamano, na ni muhimu zaidi katika kipindi hiki chenye kasi kubwa ya utandawazi unaopelekea vijana wengi kujifunza tamaduni za kigeni.

Aidha, Dkt. Abbasi licha ya kuzipongeza Taasisi hizo kwa kazi nzuri wanazozifanya amehimiza kuimarisha ushirikiano katika uhifadhi endelevu wa urithi wa maeneo hayo nchini.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Malikale Dkt. Christowaja Ntandu pamoja na kumshukuru Katibu Mkuu kwa kuzikutanisha Taasisi hizo, ameahidi kuwa Idara anayoiongoza itaendelea kutekeleza majukumu yake na kuunga mkono jitihada kubwa zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za uhifadhi wa maeneo ya kihistoria nchini na kuyatangaza ili yafahamike ndani na nje ya nchi.

Katika kikao hicho kilichoudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi CP, Benedict Wakulyamba, kilijumuisha Wakurugenzi na Maafisa waandamizi wa Wizara hiyo, Wakuu wa Taasisi na Maafisa wao kutoka Makumbusho ya Taifa, Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Mamlaka ya Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania.

HEADLINES ZA MAGAZETI YA TZ LEO JPILI MACHI 23,2025...HAYA HAPA

Saturday, March 22, 2025

BARAZA LA SABA LA WAFANYAKAZI WIZARA YA NISHATI LAKUTANA DODOMA

......................

πŸ“Œ Dkt. Kazungu asema Wizara itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Kimkakati.

πŸ“Œ Baraza lapitisha rasimu ya bajeti ya 2025/2026 .

πŸ“Œ Hoja za TUGHE zajadiliwa kwa kina na kupatiwa ufumbuzi

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Khatibu Kazungu leo Machi 22, 2025 amefungua Baraza la saba la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati ambalo limepitia pamoja na mambo mengine Rasimu ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2025/2026 na kupitia hoja mbalimbali zilizowasilishwa na TUGHE.


Akifungua baraza hilo Dkt. Kazungu amesema Wizara ya Nishati itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya nishati nchini ili kuhakikisha nchi inakua na uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme, mafuta na gesi.


"Wizara ya nishati itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya nishati nchini ili kuhakikisha Nchi inakuwa na uhakika wa nishati na katika kutekeleza hili wizara itahakikisha inasimamia taasisi zilizochini yake pamoja na makampuni tanzu yanayojishughulisha na nishati nchini". Amesema Dkt. Kazungu.


Kazungu ameelza kuwa Wizara itaendelea kutekeleza miradi ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme ikiwa ni pamoja na kufikisha Gridi ya taifa katika Mikoa iliyosalia ya Rukwa, Kagera, Lindi na Mtwara.


Aidha, Wizara itaendelea kutekeleza mpango wa taifa wa nishati wa mwaka 2025/2026 kwa lengo la kuongeza upatikanaji na uunganishaji wa umeme kwa wananchi, kuongeza mchango wa nishati jadidifu katika uzalishaji wa umeme na mashirika binafsi katika maendeleo ya sekta ya nishati na kuhakikisha upatikanaji wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.


Kutekeleza miradi wa Gridi ya taifa, kufanya matengenezo na ukarabati wa mitambo ya kuzalisha umeme pamoja na uboreshaji njia za kusafirishaji na usambazaji wa umeme katika vitongoji, maeneo ya migodi, viwanda pamoja na vituo vya afya.


Kwa upande wa Sekta ya mafuta na gesi, Dkt. Kazungu amesema sekta ya mafuta na gesi Wizara itaendelea kuwezesha upatikanaji wa bidhaa ya mafuta ,kupitia ujenzi wa vituo vya mafuta maeneo mbalimbali nchini.


Kazungu amesisitiza Wizara itaendelea kujikita katika kuwezesha utafutaji,uendelezaji na usambazaji wa gesi asilia na kutekeleza miradi ya kimkakati ya gesi asilia ikiwemo Mnazi bay Kasikazini,mradi wa kuchakata gesi asilia kuwa kimiminika (Lindi) ,utafutaji na uendelezaji na usambazaji wa mafuta ikiwemo ujenzi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Ohima (Uganda) hadi Chonholeani (Tanga-Tanzania).


Kwa upande wa nishati safi ya kupikia kwa mwaka wa 2025/2026 Wizara itaendelea kutekeleza mkakati wa matumizi ya nishati safi ya kupikia na mpango wa Taifa wa nishati wa mwaka 2030.

Aidha, Wizara itaendelea kuhamasisha sekta binafsi katika kuimarisha upatikanaji wa malighafi na miundombinu ya nishati safi ya kupikia.

Mwenyekiti wa Balaza la Wafanya kazi Wizara ya nishati Ndugu Zuena Msuya aliweza kueleza umuhimu wa kudumisha stahiki za watumishi ili kuendeleza ufanisi wa ufanyaji kazi katika Wizara ya Nishati.





WAKOPAJI WAKUMBUSHWA KUSOMA MIKATABA KABLA YA KUCHUKUA MIKOPO


Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Arch. Chagu Nghoma, akizungumza alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi zake ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali mkoani humo.

Kiongozi wa Timu ya Wataalamu wa utoaji wa elimu ya fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro, akielezea maeneo watakayofika na makundi watakayowapa elimu ya fedha wakati wa kikao cha kujitambulisha kwa Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza Arch. Chagu Nghoma , baada ya kufika mkoani humo kuanza kutoa elimu hiyo.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Arch. Chagu Nghoma, (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, Taasisi na Waratibu wa Elimu ya Fedha ngazi ya Mkoa baada ya kumaliza kujitambulisha kabla ya kwenda kuanza kutoa elimu hiyo kwa wananchi.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha, mkazi wa Buhongwa, Mwanza, Bi. Julieth Siange, akiuliza swali kuhusu namna ya kuzitambua Taasisi rasmi zilizosajiliwa wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na na Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake mkoani Mwanza.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha wakiangalia filamu yenye mada mbalimbali ikiwemo masuala ya mikopo, akiba na uwekezaji wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi zake mkoani Mwanza. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Mwanza)

.........

Na. Josephine Majura na Chedaiwe Msuya, WF, Mwanza

Serikali imewakumbusha wakopaji kusoma kwa kina masharti yote ya mikataba kabla ya kuchukua mikopo kutoka kwa Taasisi za kifedha ili kujiepusha na matatizo yanayoweza kutokea kutokana na masharti magumu au riba kubwa ambazo huathiri urejeshaji wa mkopo.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Arch. Chagu Nghoma, aliyasema hayo alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi zake ambayo imewasili mkoani humo kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha kwa Wananchi wa mkoa huo katika makundi mbalimbali.

“Tunaendelea kuwakumbusha wakopaji kuongeza umakini katika kusoma mikataba wanayoingia kutokana na kuongezeka kwa malalamiko kutoka kwa wakopaji ambao wanakabiliwa na riba kubwa, masharti magumu ya marejesho, na faini zisizoeleweka baada ya kushindwa kutimiza masharti ya mikopo.

Aliongeza kuwa ni muhimu kwa mkopaji ikiwa hajaelewa mkataba vizuri, atafute ushauri wa kisheria au wa kifedha kabla ya kutia saini mkataba wowote wa mkopo ili kujiepusha na matatizo yanayoweza kujitokeza baadae.

Arch. Chagu Nghoma, aliwasisitiza wakopaji kuwa waangalifu na kuepuka kukopa kwenye Taasisi za Fedha zisizo rasmi ambazo zinaweza kuwa na masharti kandamizi iwapo watashindwa kulipa mkopo.

Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha, mkazi wa Buhongwa, Mwanza, Bi. Julieth Siange, alishukuru kwa elimu waliyoipata ikiwemo msisitizo waliopewa wa kutojiunga na vikundi ambavyo havijasajiliwa bali wajiunge katika vikundi rasmi vilivyosajiliwa na vinavyotambulika na Serikali ili matatizo yanapotokea waweze kusaidiwa kisheria.

Kiongozi wa Timu ya Wataalamu wa utoaji wa elimu ya fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro, alisema kuwa, pamoja na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali kuweka sheria na kanuni mbalimbali kwa watoa huduma za fedha jinsi wanavyotakiwa kuendesha Taasisi hizo, bado kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya watoa huduma kutofuata sheria na kanuni.

Bw. Kimaro, alifafanua kuwa kutokana na changamoto hizo kutoka kwa watoa huduma kutokuwa waaminifu, Serikali itaendelea kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara na kuzichukulia hatua za kinidhamu ili kuhakikisha Taasisi hizo zinafanya kazi kwa kuzingatia taratibu, kanuni na sheria.

Wizara ya Fedha inaendelea na zoezi la utoaji elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi yote ikiwa ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa mwaka 2021/2022 hadi 2029/2030.