Chelsea wamefikia makubaliano na Atlanta United kumsajili beki wa kushoto wa Marekani Caleb Wiley, 19, kwa £8.5m - lakini wanatarajiwa kumtoa kwa mkopo kwa Strasbourg. (Sport Subscription Required}
Leeds United wanatarajiwa kuwauza winga wa Uholanzi Crysencio Summerville, 22, fowadi wa Ufaransa Georginio Rutter, 22, na mshambuliaji wa Italia Wilfried Gnonto, 20, msimu huu. (Football Insider)
Bayern Munich inahitaji kuuza wachezaji kabla ya kusajili mtu yeyote - huku winga wa Ufaransa Kingsley Coman, 28, mlinzi wa Uholanzi Matthijs de Ligt, 24, viungo wa Ujerumani Leon Goretzka, 29, Joshua Kimmich, 29, na Serge Gnabry, 28, na Mlinzi wa wa kushoto wa Canada Alphonso Davies, 23, miongoni mwa wanaotaka kuondoka. (Kicker, in Deutsch),
Beki wa Nice na Ufaransa Jean-Clair Todibo, 24, anataka kujiunga na Juventus baada ya uhamisho wake kwenda Manchester United kushindikana. (Gazeti)
Sevilla wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez, 29, kutoka Atletico Madrid. (SER, In Spanish).