Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Marc Gueehi, Arsenal na Manchester United wako tayari kushindania kumsaini beki huyu


 Arsenal na Manchester United wako tayari kushindania kumsaini beki wa Uingereza Marc Guehi, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 akitarajiwa kukataa ofa ya kandarasi mpya ya Crystal Palace. (Sun).

Manchester United wanatarajiwa kufikia kipengee cha kutolewa kwa Joshua Zirkzee cha pauni milioni 34 ili kumsajili fowadi huyo wa Uholanzi, 23, kutoka Bologna. (Mail)

United inajadili iwapo itaanzisha kifungu hicho cha kutolewa au kujadili ada ya juu ambayo itaruhusu malipo kwa awamu. (Guradian)

Arsenal wanatarajia kukamilisha usajili wa Riccardo Calafiori wiki hii baada ya kufanya mazungumzo zaidi na Bologna kuhusu beki huyo wa Italia, 22. (Guardian)

Post a Comment

0 Comments