Header Ads Widget

Responsive Advertisement

RUTO : Nimewasikiliza Wananchi

 


Rais wa Kenya William Ruto siku ya Alhamisi alivunja baraza lake la mawaziri na kuwafuta kazi mawaziri wake wote huku akiahidi kuunda serikali mpya ambayo itakuwa na gharama za chini na yenye ufanisi.

Katika hotuba yake kupitia televisheni, rais pia alimfuta kazi mwanasheria mkuu lakini akamsaza waziri mwandamizi wa masuala ya kigeni Musalia Mudavadi na makamu wake wa rais Rigathi Gachagua akisisitiza kwamba serikali yake itaongozwa na makatibu wa kudumu katika wizara hizo.

Hatua yake ilifuatia maandamano ya hivi majuzi ya kupinga ongezeko la kodi na utawala mbaya .

Ruto anasema alichukua uamuzi huo baada ya kuwasikiliza wananchi na kwamba ataunda serikali pana baada ya mashauriano.

Post a Comment

0 Comments