Mchezo bora wa Lamine Yamal katika Mashindano ya Ulaya -Euro yanayoendelea unatazamiwa kukuza soka nchini Equatorial Guinea, linasema shirikisho la soka nchini humo.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 16, ambaye ameushangaza ulimwengu kwa weledi wake nchini Ujerumani, anaichezea Uhispania licha ya kuwa na mama wa Equatorial Guinea na baba wa kutoka Morocco.
Alizaliwa Barcelona, ambako alikulia na anakuja kupitia akademi ya La Masia kwa mabingwa hao mara tano wa Uropa, ambako hivi karibuni alihitimisha msimu wake wa kwanza wa kucheza.
"Ingawa Lamine haichezii Equatorial Guinea, tunamshikilia kwa karibu sana mioyoni mwetu na tunadhani atafanya mambo mengi kwa soka ya Equatorial Guinea," Venancio Tomas Ndong Micha, rais wa shirikisho la soka nchini humo alisema hayo.
0 Comments