Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Huna mchepuko?? Hujawahi kunisalti ??

 

Huna mchepuko?? 

Hujawahi kunisalti ??

Mimi na mama mkwe unampenda nani zaidi 🤔🤔🙄🙄🙄


Wanaume wengi si kwamba hawapendi kukaa na wake zao na kupiga nao stori no wanapenda sana tu

Changamoto Iko hapo👆👆👆


Mume anaanza tu kuongea na mke,, mke anaanza maswali ya kijinga jinga tu hayo hapo juu , unajua kwa Nini nimesema maswali ya kijinga jinga ??hivi hata kama anachepuka atakuambia kweli??


Halafu upendo wa mama mkwe na wako vinahusiana vipi ???na je atakupenda wewe kuliko mama yake ili iweje?? Mama ni mama huwezi chukua nafasi yake ,, na wewe ni wewe huwezi kuwa mama yake ,, ukweli ni kwamba anampenda mama yake ,,na wewe anakupenda pia


Mume hata kama alikuwa anapenda kukaa mpige stori mwisho anapata kichefu chefu anaamua kuondoka kwenda kuangalia Simba na Yanga

Unabaki mume wangu hanijali Wala kunisikiliza 


Tumieni akili Wala msitende dhambi enyi wanawake

0747484974 

Leah Ndabila.

Post a Comment

0 Comments