MJUNBE wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Salim Abri Asas amewataka viongozi wa Chama Cha mapinduzi (CCM )wa kuchaguliwa na wananchi kabla ya kuchukua fomu ya kugombea tena nafasi zao kujitathimini wamezitendeaje kazi nafasi hizo na kama hawajafanya kazi wasijaribu kuchukua fomu tena.
Asas ameyasema hayo leo katika ziara yake ya kuzungumza na wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Kilolo pamoja na kukagua ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Ihimbo .
Alisema kuwa Kila kiongozi wa CCM wakati akigombea alitakiwa kukitendea Haki Chama kwa kutekeleza vyema Ilani ya CCM pamoja na kushughulikia changamoto za wananchi hivyo kama kwa kipindi Cha Miaka mitano kiongozi aliyechaguliwa atakuwa hajafanya chochote Hana sababu ya kuchukua tena fomu ya kugombea.
"Lazima Kila mmoja ajipime mwenyewe kwa kipindi Cha Miaka mitano umekifanyia nini Chama kama hujawajibika kutekeleza kazi vizuri hata fomu usichukue maana CCM haitamna nafasi kiongozi asiyewajibika kwa wananchi ushindi Wetu unatokana na uwajibikaji wa wale waliochaguliwa kama tunavyoona kwa Rais Wetu Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kazi kubwa amefanya"alisema Asas
Kuwa CCM inapoelekea kwenye Uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi mkuu 2025 lazima Chama kiende kifua Mbele kwa wananchi kwa kueleza utekelezaji mkubwa wa Ilani hivyo kama kiongozi uliyepewa nafasi ya Miaka mitano na umeshindwa kuitumia basi huna sababu ya kuchukua tena fomu ya kugombea .
Katika hatua nyingine MNEC Asas amesema ataendelea kuunga mkono ujenzi wa ofisi za CCM kata kama Chama kilivyoahidi kujenga ofisi Zote za CCM kata ndani ya wilaya Zote za mkoa wa Iringa na tayari wilaya ya Iringa Vijijini ujenzi unaendelea na baada ya kukamilika ujenzi utaanza wilaya ya Kilolo na wilaya nyingine Zote .
0 Comments