Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (Mb) Mussa Zungu amewataka wahitimu wa Chuo cha ufundi stadi Furaika kufanya kazi kwa bidii na kujiendeleza kitaaluma zaidi ili elimu wanayoipata chuoni hapo iweze kuwasaidia.
Wito huo ameutoa jijini Dar es Salaam, wakati alipokua katika mahafali ya 19 ya chuo hicho yaliofanyika katika viwanja vya chuo hicho kilichopo Buguruni Malapa ambapo amesema ajira zipo wanachotakiwa ni kuweka bidii katika masomo yao ili waweze kufanya vizuri pindi watakapoajiriwa au kujiajiri wenyewe.
Aidha, amewapongeza wahitimu hao kwa kuhitimu mafunzo ya fani mbalimbali jambo la muhimu, huku akiwataka wasiishie hapo na wajiendeleze zaidi kitaaluma kwani elimu haina mwisho.
"Serikali imeweka mazingira wezeshi ambayo kipaumbele chake ni vijana hivyo ni wajibu wenu kujituma na kufanya kazi kwa bidii popote mtakapo ajiriwa au kujiajiri wenyewe na kuwa wabunifu katika fani zenu mulizosomea "amesema Naibu Spika Zungu.
Aidha, amewaasa wahitimu hao ni kuwa na nidhamu huko waendako na kuwa mabalozi wazuri wa chuo hicho kwa kutangaza ubora wa huduma zinazotolewa chuoni hapo.
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Dkt David Msuya ameiomba Serikali kuwapatia vifaa vya kuendeleshea chuo hicho ikiwemo Komputa kwani wanatoa elimu bila malipo huku mwanafunzi akichangia gharama ya shill 50000 pekee kwa ajili ya mitihani.
"Tunakushukuru sana Naibu Spika Zungu kwa kuja kwenye mahafali haya ya 19 na nikuombe utuchangie komputa pamoja na viongozi wenzako, tunakozi ya ushonaji hivyo mukitusaidia vyerehani itakua mumetusaidia sana pamoja kutupatia vifaa vyengine kwa ajili ya kufundishia kwa vitendo hivyo kufanya hivyo mymtakua mmewasaidia wanafunzi hao"
Jumla ya wahitimu ni 45 wamehitimu mafunzo ya ufundi katika fani mbalimbali na wengi waliohitimu katika chuo hicho wameajiriwa katika sekta mbalimbali hapa nchini.
Aidha, chuo hicho kinatoa kozi mbalimbali ikiwemo Sekretari, Hoteli, pamoja na Ualimu na nyenginezo ambazo zipo chini ya Veta .
0 Comments