
Ameeleza kusikitishwa na baadhi ya Wanasiasa wa vyama vya upinzani kusambaza taarifa za kibaguzi na kubeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Dk. Mwinyi ametoa tanko hilo katika Ziara ya kukutana na Kamati za Siasa za Matawi, Wadi na Majimbo ya Mikoa ya Zanzibar ambapo leo tarehe: 07 Agosti 2024 amezungumza na wajumbe wa kamati za Siasa wa Mkoa Mjini Kichama, ukumbi wa CCM Mkoa Amani.
Kuhusiana na masuala ya Uwanja wa Ndege na Bandari Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Mwinyi amebainisha kuwa Serikali imeingia mikataba ya uendeshaji wa taasisi hizo na sio kuzibinafsisha kama inavyodaiwa na wapinzani.
0 Comments