JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Sports. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Sports. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 22 Mei 2025

PONDEZA ASISITIZA KUWA WANABEBA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ambaye pia ni mwanachama wa klabu ya Simba Mhe. Ussi Salum Pondeza asisitiza kuwa komba la Shirikisho barani Afrika ni lazima litwaliwe na vigogo wa soka nchini Simba SC.


“Lazima kombe tubebe, nasema tena lazima kombe tubebe lakini hatutashinda kama hatutakuwa kitu kimoja, kila Mwanasimba ana mchango katika Simba yetu, sio lazima kitu kikubwa.” Amesema


Aidha mwanachama huyo amewahimiza wanachama,mashabiki na wapenzi wa klabu ya simba kujitokeza kwa wingi siku ya Jumapili ya May 25, 2025 kwenye fainadi hiyo ili waweze kumlaza Mmorocco.


“Siku ya tarehe 25 twende uwanjani mapema na kushangilia muda wote. Deni kubwa ambalo tupo nalo ni kumheshimisha mtoto wa Hayati Rais Mwinyi ambaye ni Rais wa sasa Dkt. Hussein Mwinyi. Na kumheshimisha ni kumpa kombe.” ameongeza


Simba SC itacheza fainali hiyo Dhidi ya RS Berkane ya nchini Morocco katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.

 

Jumanne, 29 Aprili 2025

MALIASILI SC YATIKISA SINGIDA.


Na Sixmund Begashe 

Club ya Michezo ya Wizara ya Maliasili na Utalii maarufu kama MNRT SPORTS CLUB imeibua gumzo la shangwe Mkoani Singida kwenye mashindano ya Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi Duniani MEI MOSI 2025, Mkoani Singida, kutokana ushujaa wa timu zake hususani timu ya mchezo wa kuvuta kamba wanaume iliyofanya vizuri mpaka mwisho.

Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Singida na viunga vyake wamesikika wakiwapongeza wachezaji wa timu za Club hiyo yenye wachezaji wenye mbinu na ujuzi mkubwa, kwa kupambana vikali kwenye michuano hiyo hali inayoleta hamasa ya watu kupenda michezo na burudani ya aina yake.

Akizungumza na Maliasili Media, Bi. Mwantum Shabani wa Manyoni Singida amesema japo timu ya Maliasili Sports Club Wanaume Kamba imeshika nafasi ya pili lakini imeonesha upinzani mkali dhidi ya timu zingine pinzani.

" Singida kama burudani tumepata, mimi timu yangu ilikuwa Maliasili, si kwa sababu tu wanatulindia Maliasili zetu na kutuletea mapato kupitia Utalii, pia kwa namna walivyojipanga kwenye michezo hii, yaani ukishangilia hii timu haikuangushi, najivunia kuona wameibuka na Kombe hili naamini mwakani watakuwa washindi wa kwanza". Aliongeza Bi. Shabani.

Akizungumzia mashindano hayo makubwa hapa nchini, Mwenyekiti wa MNRT SPORTS CLUB Bw. Gervas Mwashimaha ameushukuru uongozi wa Wizara hiyo kwa kuiunga mkono club hiyo hali iliyowatia moyo na hari kubwa Kipindi chote cha michuano hiyo na kuahidi kuendelea kufanya vyema zaidi katika michezo mingine watakayo shiriki.

Katika mchezo wa Fainali wa Kamba wanaume, timu ya Maliasili imeshika nafasi ya pili dhidi ya timu 47 zilizoshiriki mashindano hayo huku timu ya Uchukuzi wanaume Kamba ikishika nafasi ya kwanza. 

Jumatatu, 28 Aprili 2025

RAIS SAMIA IPONGEZA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE KWA KUFUZU KATIKA MASHINDANO YA FUTSAL KWA AFRICA


 Hongereni wanangu Timu ya Taifa ya Wanawake katika Mchezo wa Futsal kwa kufuzu kuingia fainali ya mashindano hayo kwa Bara la Afrika, na wakati huo huo kufuzu kucheza Mashindano ya Kombe la Dunia la Futsal kwa Wanawake 2025 ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), yatakayofanyika huko Manila, Ufilipino baadaye mwaka huu. 

Nimefurahishwa na juhudi na nidhamu yenu katika mashindano haya. Ushindi wenu ni heshima kwa nchi yetu, na hamasa zaidi kwa watoto wa kike kushiriki katika michezo, si tu kwa burudani lakini pia kama ajira. Ninawapenda na ninawatakia kila la kheri.


Jumapili, 27 Aprili 2025

SIKU HAZIGANDI HATA UKIZIWEKA KWENYE FRIJI

 

Macho na akili za mashabiki wa mpira wa miguu nchini tanzania na duniani kote waliokuwa wakiisubilia siku ya leo tarehe 27.04.2025 kuushuhudia mtanange wa maamuzi makubwa sana , Baadhi ya mashabiki wa club ya Simba wamesema wapotayari kufanya chochote na popote imradi timu yao iweze kushinda


Juma hamis ni mkazi wa Temeke Mwembeyanga anasema yeye ni mnazi wa club ya Simba na leo hii simba anaibuka na ubingwa na kusonga kwenye fainali kisha kurudi na kombe nyumbani baada ya ushindi katika fainali itakayo fanyika baada ya Simba kushinda mechi ya leo ninafuraha sana kwa sababu hii siku niliisubilia kwa hamu sana nimeamini kwamba SIKU HAZIGANDI HATA UKIZIWEKA KWENYE FRIJI


Kwa upande wake Rose Anthony mkazi wa Dodoma ambaye yeye ni shabiki kindaki ndaki wa club ya Young Africans, Amesema watani wetu wameweza kupiga hatua kubwa sana kufikia hii leo kiasi kwamba ninawivu sana kwaajili yao, japokua mimi ni shabiki wa yanga sina kinyongo na watani wetu wa jadi kwa sababu wanacho kifanya wanaiwakilisha Taifa kiujumla kwa hiyo sina budi kuwa shabikia katika michuano hii ya kimataifa, wamalize salama waje na kombe nyumbani lakini wajue kwamba kwenye ligi yetu ya NBC sisi ndiyo mabingwa licha ya viporo walivyo bakisha


BIG SCREEN ya kumuangalia Mnyama akitinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika inakusubiri pale viwanja vya Mbagala Zakhiem. Mo Cola wamesimamia mpango mzima kufanikisha hili.

NJE SPORTS YAICHABANGA WIZARA YA AFYA

 

Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) imeendelea kuonesha ubora mkubwa kwa kuichapa Wizara ya Afya na kufuzu hatua ya nusu fainali katika mchezo wa mashindano ya Mei Mosi uliopigwa katika uwanja vya Airtel, eneo la Mtipa mkoani Singida. 


Mchezo huo uliokuwa wa kuvutia, ulimalizika kwa sare ya 1-1 katika dakika 90 za kawaida ambapo mshindi alipatikana kwa mikwaju ya penati na Nje Sports iliibuka kidedea kwa penati 4-2.


Kocha Mkuu wa Nje Sports, Bw. Shaban Maganga, ameonyesha furaha yake kutokana na juhudi kubwa za wachezaji wake waliopambana hadi mwisho wa mchezo. Ameeleza kuwa nidhamu na utekelezaji mzuri wa maelekezo ndio silaha ya ushindi wao.


"Nawapongeza wachezaji kwa kuonesha nidhamu na kufuata maelekezo, ndiyo siri ya ushindi wetu leo. Tunaendelea kujiandaa zaidi kwa nusu fainali." Alisema kocha Maganga.


Mwenyekiti wa timu, Bw. Ismail Abdallah, naye hakuficha furaha yake, akieleza kuwa ari ya wachezaji na sapoti waliyoipata kutoka kwa uongozi wa wizara ndiyo iliyowasaidia kupata matokeo mazuri.


"Wachezaji wameonyesha juhudi kubwa. Salamu za hamasa tulizopokea leo kutoka kwa Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara yetu zimewapa nguvu ya ziada. Tunapambana hadi kulichukua kombe," alisema.


Mashindano haya ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Mei Mosi kitaifa, yakihamasisha mshikamano na afya miongoni mwa watumishi wa umma.

Listen Mkisi Radio