Na Fredrick Siwale -Mufindi.
RAI hiyo imetolewa wakati wa Mahafali ya 48 ya Chuo cha afya na Sayansi Shirikishi Mafinga (MaCHAS) yaliyofanyika Mjini Mafinga.
Akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dr.Linda Selekwa , Afisa Tarafa ya Ifwagi Bi.Faraja Ndapo alisema umefika wakati ambao Wadau wa Sekta ya Afya wanapaswa kusaidia kufadhili mafunzo kwa Wanafunzi na Wakufunzi.
"Kada hii ni nyeti kwa majukumu na Utendaji wake hivyo niwaombe Wadau msaidie katika kutoa ufadhili kwa Wanachuo na Wakufunzi wao ili kuwapunguzia ukali wa changamoto"Alisema Bi.Ndapo.
Aidha akijibu risala ya Mkuu wa chuo cha MaCHAS Bi.Ndapo ,alisema Serikali inaendelea kufanya jitihada za makusudi ili kuhakikisha changamoto zinapungua au kuondolewa kabisa.
Alisema juhudi , mikakati na majukumu yaliyoelezwa na Mkuu wa chuo Juma Mkamba ,inayatambua na itaendelea kuboresha Mazingira ya Chuo hicho hatua kwa hatua kadri bajeti na uchumi wa Nchi unavyokua.
Kuhusu Changamoto ya kukosekana kwa Maji ya ya kutosha katika Chuo hicho Bi.Ndapo alisema atawasiliana na mdau ( Water for Afrika ili aweze kuchimba kisima kama alivyoahidi siku za nyuma.
Bi.Ndapo alisema ni sera ya Taifa kutoa mikopo kwa Wanafunzi wa vyuo vya kati ili kupambana na changamoto wanazokutana nazo wakati wanasoma.
" Natoa wito kwa Wadau wa elimu kusaidia ufadhili wa mafunzo kwa Wakufunzi ili kuongeza mapato ya Chuo ,napendekeza Wanafunzi na Wakufunzi kutumia fursa ya kutoa ushauri ( Consultancy) na utafiti (research) kwani hii ndio njia pekee inayoweza kufutia Wahisani." Alisema Bi.Ndapo.
Aliendelea kuwaomba Wadau wa Maendeleo katika Sekta ya afya Wilayani Mufindi kuwatumia Wataalamu wa Chuo na Wanafunzi katika kufanya kazi zao.
Mkuu wa Chuo Juma Mkamba alisema Chuo kinakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa Ukumbi wa kufanyia sherehe na kupelekea kufanyika eneo la wazi na hivyo mvua ,Jua na vumbi ni sehemu ya maisha.
Mkamba aliwataka Wanafunzi kuendelea kufikiria kusonga mbele badala ya hapo walipo fikia,
"Wahitimu elimu haina mwisho na hapa ni hamjafika safari bado ndefu na msije kung'ang'ania eti nilisoma afya huko mbele kuna fursa ni suala la kijiongeza kielimu na kitaaluma.
Makamu Mkuu wa chuo Keneth Lihokolelo aliwataka Wahitimu kwenda kuwa nuru waendako kwa kuonyesha tabia njema na sio kuwa giza na kuchafua uwepo wao wa kukaa chuoni kipindi chote cha miaka mitatu.
" Hiyo itakuwa ni hasara kwenu na kwa Wazazi pamoja na Taifa ambalo linawategemea kuwa mkaendelee mbele zaidi na kuja kuisaidia Jamii ya Watanzania " Alisema Lihokolelo.
Madau wa Sekta ya afya Wilayani Mufindi Dr.Basil Tweve Mkurugenzi wa Chuo na hospitali ya Tumaini Jipya Mafinga,alisema Chuo hicho ni kikongwe kwani kilianzishwa mwaka 1977 na kina jina zuri.
Dr.Tweve aliwataka Wahitimu waendako wakawe mabalozi wazuri na wakajihusishe na taaluma ya Utabibu na wasiende kuingia kwenye kujihusisha Uganga wa kienyeji itakuwa ni fedheha .
" Kazingatieni miiko ya kazi ya Utabibu na taratibu zote za Wizara ya afya mtadumu na kusonga mbele lakini mkienda kujigeuza " makalunjila mtapotea mchana kweupe" Alisema Dr.Tweve.
Awali katika risala ya Wahitimu iliyosomwa na Hadija Khatibu Nsumiyinda ,aliomba Serikali kuharakisha utatuzi wa changamoto kadhaa zinazo kikabili Chuo hicho ikiwa ni pamoja na upungufu wa vitendea kazi kama magari , kompyua ,viwanja vya michezo na Ukumbi.
Alisema pamoja na jitihada za Serikali ya awamu ya sita kupambana kuboresha Sekta ya Elimu Nchini ,Wadau nao wameombwa kuisaidia Serikali kwa kuwezesha pale inapobidi
0 Comments