Header Ads Widget

Responsive Advertisement

WAFUGAJI WAJENGEWA MAZIZI YA WAYA KUZUIA SIMBA NA FISI KULA MIFUGO YAO

 

Na,Jusline Marco; Babati.


Wafugaji wanaoishi ndani ya eneo la hifadhi ya jamii ya Wanyamapori ya Burunge(Burunge WMA) wilayani Babati, Mkoa Manyara na maeneo ya jirani, wamejengewa mazizi ya waya(Boma Hai) ili kuzuia wanyama wakali hususani Simba na Fisi kuvamia na kula  mifugo nyakati za usiku.

Mazizi hayo yamejengwa na Taasisi ya uhifadhi na Utalii ya Chem Chem, ambayo inafanya shughuli za uhifadhina Utalii katika eneo hilo lilipo kati kati ya hifadhi ya Taifa ya Tarangire na  Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ikiwa ni sehemu ya Mkakati wa Taasisi hiyo ili kupunguza migogoro baina ya Wanyamapori na Mifugo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mazizi hayo, Mkuu wa Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara, Lazaro Twange  alisema  mradi wa ujenzi mazizi hayo ni utekelezaji wa maagizo la serikali kupunguza migogoro baina ya wanyamapori na binaadamu.

Twange ambaye aliwakilishwa katika uzinduzi wa mazizi hayo na Katibu Tawala wa wilaya ya Babati, Khalfani Malipula alisema Kazi nzuri ya uhifadhi imefanyika na sasa kuna changamoto ya wanyamapori kula mifugo jambo ambalo limeanza kupatiwa suluhu.

Alisema uzinduzi wa Mazizi hayo ambao umeambatana na maadhimisho ya siku ya Askari wa hifadhi duniani unatarajiwa pia kuwaondolea wananchi adha ya kulala nje kulinda mifugo yao.

Peter Martin Mkazi wa kijiji cha Ngoley ameishukuru Taasisi hiyo na Serikali kuwajengea mazizi hayo kwani sasa watakuwa wanalala kwa amani.

Naye Msimamizi wa Miradi ya Maendeleo ya Jamii ya Chem Chem, Napendaeli Wazoeli alisema Chem Chem kwa kushirikiana na askari wanyamapori, waliona katika maadhimisho ya siku ya askari wa wanyamapori duniani wakabidhi mazizi hayo ambapo kila zizi limegharimu zaidi ya shilingi milioni 2.6.


Awali akizungumza katika maadhimisho na uzinduzi huo Mwenyekiti wa Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori Burunge WMA, Erick Lilayoni alisema hifadhi hiyo itaendelea kushirikiana na Taasisi ya Chem Chem na wadau wengine ili kuhakikisha hifadhi inaendelea kuwa kivutio cha watalii.

Post a Comment

0 Comments