Yunus amechaguliwa kuongoza serikali ya mpito ya Bangladesh baada ya waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Sheik Hasina kujiuzulu na kuikimbia nchi hiyo kufuatia wiki kadhaa za machafuko.
Mkosoaji mashuhuri wa Bi Hasina, Yunus mwenye umri wa miaka 84 aliita siku ya kuondoka kwa Hasina "siku ya pili ya ukombozi."unus amechaguliwa kuongoza serikali ya mpito ya Bangladesh baada ya waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Sheik Hasina kujiuzulu na kuikimbia nchi hiyo kufuatia wiki kadhaa za machafuko.
Mkosoaji mashuhuri wa Bi Hasina, Yunus mwenye umri wa miaka 84 aliita siku ya kuondoka kwa Hasina "siku ya pili ya uko
Yeye ni mmoja wa watoto tisa, Yunus alizaliwa katika familia ya wafanyabiashara Waislamu katika mji wa pwani wa Bangladesh wa Chittagong. Akiwa na umri wa miaka 25 alisafiri hadi Marekani kusoma chini ya udhamini wa Fulbright, na akarejea Bangladesh mwaka 1971.
Na ndio mwaka ambao nchi hiyo ilijipatia uhuru kutoka kwa Pakistan katika vita vya kikatili na vya umwagaji damu.
Aliporejea, Yunus alichaguliwa kuwa mkuu wa idara ya uchumi ya Chuo Kikuu cha Chittagong, kisha akaingia kupambana na njaa iliyoikumba Bangladesh katikati ya miaka ya 70.
"Nilijihusisha na suala la kupambana na umaskini sio kama mtunga sera au mtafiti," alisema katika mhadhara wa 2005 katika Taasisi ya Jumuiya ya Madola huko London.
“Nilijihusisha kwa sababu umaskini ulinizunguka. Sikuweza kugeuza macho yangu na kukosa kuuona. Nilitaka kufanya kitu kusaidia watu walio karibu nami."
Kwa sababu hiyo Yunus akawa mwanzilishi wa dhana inayojulikana kama "mikopo midogo." Watu ambao ni maskini hawawezi kukopa katika mabenki makubwa, wanapewa mikopo midogo, ambayo huwaruhusu kujiajiri.
Mwaka 1983 Yunus alianzisha Benki ya Grameen, iliyojitangaza kuwa "muasisi wa shirika la mikopo midogo duniani," ambalo tangu wakati huo limekusanya zaidi ya wateja milioni tisa.
Katika mahojiano na BBC mwaka 2002, alielezea mikopo midogo kama "hitaji la watu. Kwa sababu sio haki kabisa kuwanyima huduma za kifedha nusu ya idadai ya watu duniani," alisema.
Mpango wa Yunus ulifanikiwa sana hata ombaomba waliweza kukopa pesa chini ya mpango wake.
Yunus na Benki ya Grameen walitunukiwa Tuzo ya Amani mwaka 2006 kwa kazi yao ya "kuunda maendeleo ya kiuchumi na kijamii kutoka chini," kulingana na tovuti ya Tuzo ya Nobel.
Yunus mwenyewe amepitia dhoruba ya kupingwa na utata nchini Bangladesh, ikiwemo kutoka kwa Hasina, kiongozi ambaye sasa anatazamiwa kuchukua nafasi yake.
Alisababisha hasira ya waziri mkuu huyo wa zamani baada ya kutangaza mipango ya kuanzisha chama chake cha kisiasa "Citizen Power" mwaka 2007.
Hasina alimshutumu Yunus kwa "kunyonya damu za maskini," na mwaka 2011 serikali yake ilimuondoa kama mkuu wa Benki ya Grameen.
Mwaka 2013, alikabiliwa na tuhuma zilizoungwa mkono na serikali, kuwa hafuatia Uislamu na anashabikia mapenzi ya jinsia moja, baada ya kutia saini kauli ya pamoja ya kukosoa kuandamwa kwa wapenzi wa jinsia moja nchini Uganda.
Yunus pia alikabiliwa na mashtaka kutokana na madai ya kupokea pesa bila idhini ya serikali, na madai ya hivi karibuni zaidi ni kwamba alifuja pesa kutoka katika mfuko wa mafao ya wafanyakazi wa kampuni yake.
Januari mwaka huu alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kukiuka sheria za kazi, jambo ambalo alilikanusha, na mwezi Juni, yeye na wengine 13 walifunguliwa mashtaka ya ubadhirifu. Lakini alipewa dhamana.
Ila bado anakabiliwa na zaidi ya kesi 100 kuhusu ukiukaji wa haki za wafanyakazi na tuhuma za rushwa.
Yunus amekana mashtaka yote, akidai kuwa mashambulizi dhidi yake yanachochewa kisiasa.
Tuhuma hizo hazijasaidia kuondoa umaarufu na uungwaji mkono wa Yunus kwa wafuasi wake wengi, ambao wanadai analengwa kutokana na uhusiano wake mbaya na Bi Hasina.
Asif Mahmud, kiongozi mkuu wa kundi la Wanafunzi wanaopinga Ubaguzi (SAD), alichapisha picha ya kushangaza kwenye Facebook siku ya Jumanne: kigae chekundu chenye maandishi meupe - muundo sawa na ambao Mahmud ameutumia kwa jumbe kadhaa zinazohusu maandamano.
Lakini wakati huu ujumbe huo ulikuwa na maneno matano tu: "Tunamwamini Dk Yunus."
0 Comments