Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MATIVILA AWATAKA WAJUMBE WA BARAZA LA WAFANYAKAZI TAMISEMI KUFANYA KAZI KWA BIDII ILI KUFIKIA MALENGO YA SERIKALI

 

Na. Asila Twaha. OR – TAMISEMI


Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Rogatus Mativila amewataka watumishi wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI ambao ni  wajumbe wa baraza la wafanyakazi  kufanyakazi kwa bidi ili  kuendana na kasi ya Serikali.


Mhandisi Mativila  ameyasema hayo leo tarehe 4 Machi, 2025 wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa ofisi ya Rais – TAMISEMI kilichofanyika jijini Dodoma, chenye lengo la kutoa fursa kwa watumishi kupitia wajumbe wao  kujadiliana juu ya masuala mbalimbali yanayohusu tija na ufanisi  kwa upande mmoja na maslahi yao kama watumishi kwa upande mwengine


“Baraza la wafanyakazi linaongeza ushiriki wa wafanyakazi katika uendeshaji wa  shughuli za Taasisi kama ilivyofafanuliwa katika sheria ya majadiliano ya pamoja katika Utumishi wa Umma Sura 105”amesema Mativila



Mhandisi Mativila amewataka watumishi kutumia baraza la wafanyakazi kujadili malengo na mipango ya Taasisi ikiwa ni pamoja na maslahi ya watumishi pia amewasisitiza kuwa, mabaraza ya wafanyakazi yanatakiwa kujadili utendaji kazi wa kila siku na jinsi ya kuboresha utendaji kazi zaidi. 


“Tija na maslahi lazima viwe na uwiano ili kuwa na matokeo bora ya utendaji kazi unaolenga kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi” Mativila


Amewasisitiza wajumbe hao kuhakikisha baraza la wafanya kazi linatakiwa kuwa na wajibu wa kuhakikisha kunakuwepo na maelewano, ushirikiano na mshikamano kati ya wafanyakazi na uongozi wa Taasisi na vilevile linatakiwa kuhakikisha kunakuwepo na nidhamu ya kazi kwa lengo la kuleta tija na ufanisi katika uendeshaji wa shughuli za Taasisi.


Kwa upande wa Mkurugenzi wa  Utawala na Rasilimali  Watu Ofisi ya Rais – TAMISEMI Bi. Emma Lyimo amemueleza Katibu Mkuu kuwa, kikao hicho ambapo wajumbe ni wawakilishi wa watumishi wengine watapata nafasi ya kuuliza maswali na changamoto zinazowakabili katika majukumu yao ya  kazi na  pia hupatiwa ufafanuzi  hapo hapo sababu kunakuwepo na  wakuu wa Idara na Vitengo husika.


“Nitoe rai kwa wakuu wa Idara na Vitengo kushiriki vikao vya baraza la wafanya kazi  ambavyo ni muhimu sana sababu ni sehemu ya  watumishi  kuuliza maswali na kupata majibu” amesema Lyimo


Kikao cha baraza la

 wafanyakazi kwa watumishi wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI  na Taasisi zake kitakuwa ni cha siku mbili ambapo pia watumishi  watapata fursa ya kufundishwa mada mbalimbali ili kujengewa uwezo wa utendaji wa majukumu yao na maisha.

Post a Comment

0 Comments