JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Top Stories.. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Top Stories.. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 4 Juni 2025

KIWANDA CHA KUSAFISHA NA KUONGEZA THAMANI MADINI ADIMU KUJENGWA KIJIJINI NGWALA,SONGWE

 

KIWANDA CHA KUSAFISHA NA KUONGEZA THAMANI MADINI ADIMU KUJENGWA KIJIJINI NGWALA,SONGWE


▪️Uendelezaji wa Mradi kuanza rasmi    Disemba 2025


▪️Ni mradi wa Madini Adimu utakaogharimu Bilioni 771


▪️Waziri Mavunde azindua zoezi la ulipwaji fidia wananchi 192


▪️Wananchi wamshukuru Rais Samia kwa mazingira ya uwekezaji


▪️Serikali kuvuna mapato ya zaidi ya Trilioni 12 


Ngwala,Songwe


Kampuni ya Mamba Minerals Ltd inayowekeza kwenye mradi wa Madini adimu imeweka wazi mpango wake wa kujenga kiwanda cha kusafisha na kuongeza thamani madini adimu kijijini,Ngwala Mkoani Songwe badala ya kusafirisha madini hayo yakiwa ghafi.


Hayo yamesemwa leo Kijijini Ngwala,Songwe wakati wa uzinduzi wa zoezi la ulipwaji fidia wananchi waguswa wa mradi takribani 192 zoezi ambalo limezunduliwa na Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde.

Akitoa maelezo ya awali,Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mamba Minerals Ltd Ndg. Ismail Diwani amesema zoezi hilo la fidia litagharimu kiasi cha Tsh 5.3 Bilioni kwa kuhusisha wananchi waguswa wa mradi 192 ambapo mpaka sasa wananchi 116 wamepokea malipo yao tayari.


“Hatua hizi ni za awali kuelekea kwenye utekelezaji wa mradi ambapo shughuli rasmi za ujenzi wa mradi zitaanza Disemba 2025 sambamba na ujenzi wa kiwanda cha kusafisha madini adimu na ujenzi wa mtambo wa kufua umeme utakaozalisha megawati 12”Alisema Ismail

Waziri Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Mamba Minerals Ltd kwa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha madini hayo hapa nchin ikiwa ni uongezaji wa thamani wa madini hayo kabla ya kusafirishwa ikiwa ni sehemu ya kuitikia wito uliotolewa na Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan juu ya uongezaji thamani madini nchini.


“Mradi huu pamoja na Ajira,mrabaha,ushuru wa Halmashauri pia utaipa serikali mapato ya moja kwa moja ya zaidi ya Tsh 12 Trilioni wakati wote wa uhai wa mgodi.


Tutahakikisha wananchi wa Ngwala wananufaika na mradi huu mkubwa kupitia maudhui ya ndani(𝙡𝙤𝙘𝙖𝙡 𝙘𝙤𝙣𝙩𝙚𝙣𝙩) na hivyo mradi huu kuwa kichocheo cha maendeleo ya kiuchumi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Mradi huu una wastani wa mashapo ya  Tani 18.5 milioni  za madini adimu ni kati ya miradi mikubwa  duniani ya madini adimu na hivyo itaifanya Tanzania kuwa mzalishaji wa malighafi kwa ajili ya vifaa vya matibabu,kieletroniki na ufuaji wa umeme wa upepo”Alisema Mavunde


Naye Mkuu wa Wilaya wa Songwe Mh. Solomon Itunda amesema mradi huu utachochea ukuaji wa sekta ya madini Mkoani Songwe kwa kiwango kikubwa na hivyo kuufanya mkoa huu kuwa kati ya wachangiaji wakubwa katika kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya madini.

KAMPUNI YA KIZALENDO (MOFAT) YAULA MABASI YA ENDAYO HARAKA (BRT)


 Na Mwandishi wetu 


KAMPUNI ya Kizalendo ya Mofat imepewa mkataba wa miaka 12 na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Dart) kwa ajili ya kuendesha Awamu ya Pili ya mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT), unaotoka Gerezani hadi Mbagala. 


Kampuni hiyo ya Kizalendo ya Mofat inatarajiwa kuanza kutumia mabasi 255 yanayotumia gesi ifikapo Agosti 2025.

Akizungumza hayo hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji wa Dart, Dkt. Athuman Kihamia, alithibitisha kuhusu mkataba huo jana katika mahojiano ya simu akiwa nje ya nchi.


Alisema maendeleo yanakuja wakati serikali ikihamia rasmi katika kuhamisha uendeshaji wa awamu ya kwanza na ya pili ya mfumo wa BRT kwa sekta binafsi, ikiwa ni juhudi za kuongeza ufanisi na kushughulikia changamoto za muda mrefu za usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

''Hii ni kampuni ya kizalendo na tayari imepata mitaji na dhamana zinazohitajika kuendesha huduma hii.


"Hivyo hii ni hatua kubwa katika juhudi zetu za kutoa huduma za usafiri wa uhakika na bora kwa wakazi wa jiji. Kampuni hiyo imejitolea kuleta mabasi ndani ya muda tuliokubaliana,"alisema Dkt. Kihamia.

Mwelekeo wa kuwashirikisha zaidi waendeshaji wa ndani ulisisitizwa pia Jumatatu na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, aliyewaambia wahariri jijini Dar es Salaam kuwa Dart sasa inalenga kuvutia wawekezaji zaidi—hasa kwa kuwa ujenzi wa Awamu ya Kwanza na ya Pili umekamilika, huku Awamu ya Tatu ikitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.


Kwa mujibu wa mfumo mpya, mfumo wa BRT utaendeshwa na kampuni kati ya nne hadi sita, badala ya mfumo wa sasa wa mtoa huduma mmoja unaoongozwa na UDA Rapid Transit (Udart).

Ijumaa, 30 Mei 2025

CHAMA CHA MAPINDUZI CHAZINDUA ILANI YAKE YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2025

Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 yazinduliwa leo katika mkutano mkuu maalum wa chama cha mapinduzi (CCM) Taifa unaonedelea katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.


Akizundua ilahi hiyo Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) na Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu na mgombea mwenza wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, makamu mwenyekiti wa CCM Mhe. Stephen Wasira pamoja na viongozi wengine wa chama hicho.







WAKUU WA MAJESHI YA POLISI NCHI ZA SADC KUKUTANA TANZANIA


 

JICA YAAHIDI KUENDELEA KUISHIKA MKONO SERIKALI YA TANZANIA-MAJALIWA


JICA YAAHIDI KUENDELEA KUISHIKA MKONO SERIKALI YA TANZANIA-MAJALIWA


_▪️JICA, Benki ya Dunia na AFDB watoa Dola za Marekani mil 516 miradi ya kilimo_


_▪️Washauri elekezi wawili Mjapan na Mtanzaniia wawekwa TIC kurahisha uwekezaji_

 

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) limeihakikishia Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa itaendelea kushirikiana nayo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi.


Hatua hiyo imetokana na namna ambavyo Serikali imekuwa ikisimamia kikamilifu matumizi ya fedha mbalimbali zinazotolewa na wadau wa maendeleo likiwemo shirika hilo. Waziri Mkuu amesema “Serikali itaendelea itaendelea kusimamia ipasavyo fedha zote za maendeleo zinazoletwa nchini na kuhakikisha zinatumika kama ilivyokusudiwa.”


Ameyasema hayo juzi (Jumatano, Mei 28, 2025) alipokutana na Makamu wa Rais wa JICA, Miyazaki Katsura kwenye ukumbi wa Mikutano wa Tachibana uliopo katika hotel ya New Otani, Tokyo nchini Japan akiwa katika ziara yake ya kikazi.

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa JICA kuendelea kutafuta wadau zaidi wa maendeleo kwa ajili upatikanaji wa fedha zitakazowezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuwafanya Watanzania kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi.


Amesema lengo la wito huo ni kuwezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa malengo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha kuwa wanafungua milango ya kiuchumi ili wananchi wengi washiriki katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kujiongezea kipato.


“Lengo la kutafuta wadau hawa ni kuwawezesha wananchi washiriki kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi, wanaotaka kuingia kwenye biashara, wanaotaka kuingia kwenye kilimo, sekta ya madini, sekta ya uvuvi na ufugaji haya ni maeneo ambayo tumeyawekea umuhimu.”


Waziri Mkuu amesema Serikali inataka kuona wananchi wanaendesha shughuli za kibiashara kukiwa na huduma zote katika mazingira rahisi, ikilinganishwa pia na utekelezaji wa miradi ya elimu, afya, miundombinu, nishati, ujenzi wa barabara pamoja na kilimo ni maeneo yanayotiliwa mkazo.


Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa JICA, Miyazaki Katsura alisema shirika lao linaendelea kutekeleza miradi mbalimbali nchini kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo Benki ya Dunia katika mradi wa Ustahimilivu wa Chakula.


Makamu huyo wa Rais wa JICA alisema kuwa shirika lao litaendelea kushirikiana na Serikali katika kufanikisha miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini ikiwemo ya kuimarisha sekta ya miundombinu na usafirishaji.


Naye, Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde ametumia fursa hiyo kuushukuru uongozi wa JICA kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (WB), Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 516 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kilimo.


Mheshimiwa Silinde ametaja miradi hiyo kuwa ni Mradi wa Ustahimilivu wa Chakula (TSRP) unaogharimu zaidi ya Dola za Marekani milioni 371 ambazo kati yake Benki ya Dunia imetoa Dola milioni 300.05 na JICA imetoa Dola milioni 71.09, ambapo utekelezaji wa mradi huo unafanyika kwa miaka mitano kuanzia 2025 hadi 2030.


Amesema mradi mwingine ni wa Tanzania Agricultural Inputs Support Project (TAISP) unaotekelezwa kwa ubia kati ya Benki ya Maendeleo Afrika na JICA unaohusika na utoaji wa ruzuku katika pembejeo za kilimo.


Waziri Shilinde amesema mradi huo unaotarajiwa kugharimu Dola za Marekani milioni 145, ambapo kati ya fedha hizo, JICA wanatoa dola milioni 70 na AfDB dola milioni 75.49 na ulianza kutekelezwa mwaka 2024 na utakamilika 2028. Tayari dola milioni 40 zimelipwa kwa kampuni 17 kwa ajili ya usambazaji wa mbolea.


Waziri Silinde amesema fedha hizo zimetolewa baada ya wadau hao kuridhishwa na namna ambavyo Serikali inasimamia sekta ya kilimo kwa mafanikio makubwa. Hata hivyo amewaomba wawekezaji na wafanyabiashara wa Japan waje kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji hususan kwenye teknolojia ya umwagiliaji.


Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Ali Mohamed Ameir amesema katika vikao hivyo amewahakikishia wawekezaji na wafanyabiashara wa Japan uwepo wa mazingira wezeshi ya kutekeleza majukumu yao Zanzibar ikiwemo hali ya amani na utulivu.


Pia, Mheshimiwa Ameir ametumia fursa hiyo kuiomba JICA kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kukamilisha miradi miwili ya ujenzi ikiwemo upanuzi wa soko na jiko la samaki katika eneo la Malindi hususani kutoa vifaa kwa wafanyabiashara pamoja na mradi wa usambazaji maji mijini katika Mkoa wa Mjini Magharibi. Miradi yote inatekelezwa kwa awamu ya pili.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri ameishukuru Serikali ya Japan kupitia JICA kwa kugharamia washauri elekezi wawili ambao watakuwa kiungo kati ya wawekezaji na wafanyabiashara wa Japan na Tanzania.


Amesema washauri hao elekezi ambao watakuwepo TIC mmoja ni Mtanzania na mwingine Mjapani watakuwa na majukumu ya kutoa taarifa za namna ya kufanikisha uwekezaji kati ya Tanzania na Japan.


“Lengo la huyu mwelekezi kutoka Japan ni kuzungumza na kusaidia makampuni na wawekezaji kutoka Japan kupata taarifa za namna ya kuja kuwekeza Tanzania na huyu wa Tanzania ni kusaidia Watanzania wote wanaotaka kuuza bidhaa zao Japan waweze kupata usaidizi kupitia kituo cha uwekezaji.”


Awali, Meneja Uenezi na Masoko wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Khamis Dunia alisema ushiriki wa Tanzania kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Osaka (World Expo Osaka 2025) yanayoendelea nchini Japan umeiwezesha mamlaka yao kutangaza fursa za uwekezaji na biashara zilizopo Zanzibar.


Alisema mbali na maonesho hayo, pia kitendo cha kushiriki katika mikutano iliyomhusisha Waziri Mkuu pamoja na wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa wa Kijapan vilivyofanyika jijini Tokyo alipata fursa ya kuelezea vipaumbe vya uwekezaji vilivyopo Zanzibar ikiwemo uchumi wa buluu na utalii jambo ambalo liliwavutia wawekezaji hao ambao tayari baadhi yao wameonesha nia ya kuwekeza Zanzibar.

Mbeto : Wana CCM wameondoka Dodoma kibabe ,vifua mbele tayari kwa ushindi


 Mbeto : Wana CCM wameondoka Dodoma kibabe ,vifua mbele tayari  kwa ushindi


Na Mwandishi  Wetu, Dodoma 



Chama Cha Mapinduzi kimesema Wajumbe wake wa Mkutano  Mkuu wa  Taifa , wanaondoka katika Jiji la Dodoma huku  wakiwa wamebeba  matumaini  ya kupata  ushindi kuliko  wakati  wowote. 


Mamia  ya  Wajumbe hao  toka Mikoa  ya Tanzania Bara na Zanzibar  wameliacha Jiji Kuu hilo la Tanzania ,wakiamini chama  chao kitashinda uchaguzi  Oktoba  Mwaka huu. 


Matamshi hayo yametamkwa na Katibu  wa Kamati  Maalum  yya  NEC Zanzibar  , Idara ya itikadi , Uenezi na Mafunzo,  Khamsi Mbeto Khamis ,aliyesema  kazi iliobaki  ni kuinadi Ilani  mpya  ya CCM ya Uchaguzi   Mwaka 2025 -2030 kwa nguvu zote .


Mbeto  alisema hakuna Chama cha Siasa wala mgombea atakaehimili  kimbunga cha Kampeni  za CCM ambazo zitaanza Miezi michache ijayo toka sasa.


Alisema Uwasilishaji wa  taarifa ya matokeo ya Ilani  Uchaguzi ya Mwaka 2020-2025, tija na  mafanikio ya utekelezaji wa maendeleo  ya kisekta , kumedhihirisha nia thabit walionayo Marais ,  Dk Samia  Suluhu  Hassan na mwenzake , Dk Hussein  Ali Mwinyi .


"Wajumbe  wa Mkutano Mkuu wameondoka  Dodoma  wakiwa wamebeba vikapu vya matumaini ya ushindi . Silaha ya ushindi  wa chama cha siasa hutokana na ubora wa Ilani ,  sera  na mipango ya maendeleo " Alisema Mbeto .


Aidha, Katibu huyo Mwenezi , alisifu kazi kubwa iliiofanywa na Serikali zote mbili  katika  azma ya kutumikia wananchi na kuweka mkazo  katika utatuzi wa changamoto za  maendeleo ya kisekta. 


Alisema  matokeo  ya utekelezaji wa Ilani iliopita ya Mwaka  2020-2025 , imeelezea mafanikio ya Sekta za Afya , Elimu , Uwekezaji , Miundombinu , Nishati ya Umeme na gesi  , Ufugaji na  ukuzaji Kilimo.


 'Taifa limepiga hatua nyingi za kimaendeleo hususan  katika sekta ya Usafiri,  Mawasiliano  na Makaazi ya Nyumba  bora za  kisiasa, ujenzi  wa Masoko, Barabara ,  Shule  za Msingi na 

Sekondari ikiwemo  Ujenzi wa Vituo vya Afya na Zahanati " Alieleza 


Pia alisema  Ilani iliopita imetaja na kuonyesha mafanikio  katika ukuaji wa  Uchumi  wa Taifa , pato la Taifa,   Viwanda, Uhusiano wa Kimataifa , Diplomasia, Michezo na Siasa  pia mikopo ya  taaisis za  kimatiafa na Elimu ya juu .


Kadhalika  Mbeto  alisema taarifa katika  ilani iliopita  imeonyesha jinsi halmashauri   za wilaya zilivyoanzisha miradi ya Maji Safi na Salama ,  Barabara za Vijijini, Wilaya na Mikoa hadi  kukamilika kwake.


"Matumaini makubwa ya Wananchi yamebebwa na ilani mpya Uchaguzi wa  Mwaka huu  2025-2530 .Utekelezaji  wa mipango iliiomo katika   ilani hiyo itaipaisha na kuifanya Tanzania kuwa miongoni   mwa Nchi za uchumi  Kati "Alieleza katibu  huyo Mwenezi

Vijana 26 Kushiriki progranu ya Mandela Washington Fellowship 2025 nchini Marekani



 Vijana 26 Kushiriki progranu ya Mandela Washington Fellowship 2025 nchini Marekani 


Vijana waliochaguliwa kushiriki progranu ya Mandela Washington Fellowship kwa mwaka 2025, wamekumbushwa kuwa fursa waliyoipata haikuja kwa bahati, isipokuwa kutokana na majukumu wanayoyafanya ambayo yana mchango mkubwa kwa jamii.


Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa wakati anawapa nasaha za kuwaaga vijana hao 26 jijini Dodoma Mei 30, 2025.

Balozi Mussa aliwataka kutumia fursa hiyo kujifunza mambo mapya kwa kuwa nchi wanayokwenda imeendelea kiuchumi na kiteknolojia duniani na itawapa fursa pia ya kukutana na raia wa mataifa mbalimbali wenye uzoefu na mila tofauti.


Vijana hao ambao wanatarajiwa kwenda nchini Marekani Juni na kurejea Agosti 2025,  wametakiwa kulitangaza jina la Tanzania kwa watu watakaokutana nao. "Mtalitangaza jina la nchi yetu kwa kuheshimu sheria za nchi mnayokwenda,  kutangaza utamaduni mzuri wa Tanzania na kuelezea kwa ufasaha mambo makubwa na mazuri ya nchi kama vile mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, maziwa, mito na maendeleo ya miundombinu", Balozi Mussa alisema. 


Balozi Mussa alisema kuwa kuwepo kwao katika programu hiyo ni kielezo cha uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Marekani ambao umedumu tokea ulipoanzishwa mwaka 1961.


Pogranu ya Mandela Washington Fellowship ilizinduliwa mwaka 2014 na hadi sasa vijana 6500 kutoka nchi za Afrika wamefaidika na mpango huo ambao unalenga kuwajengea uwezo vijana, kupata mbinu na ujuzi wa uongozi utakaosaidia kuleta mabadiliko chanya ya kiuchumi, kisiasa na kijamii barani Afrika.

Jumatano, 28 Mei 2025

OFISI YA TRA MBULU KUJENGWA 2026/27

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akijibu swali la  Mbunge wa Mbulu Mjini, Mhe. Zacharia Paulo Issaay, aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kujenga Ofisi ya TRA katika Wilaya ya Mbulu, jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Wizara ya Fedha)

......................

Na. Josephine Majura, WF, Dodoma

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), amesema kuwa Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ina mpango wa kuanza ujenzi wa Ofisi ya TRA katika Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara, katika mwaka 2026/27. 

Aliyasema hayo bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbulu Mjini, Mhe. Zacharia Paulo Issaay, aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kujenga Ofisi ya TRA katika Wilaya hiyo.

Alifafanua kuwa katika kipindi ambacho hakuna Ofisi ya TRA, shughuli za ukusanyaji wa mapato ya Serikali zinafanyika kwenye jengo la iliyokuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.

Mwisho.

Jumapili, 25 Mei 2025

MBUNGE PONDEZA AMWAGA MAMILIONI UWT

 

MBUNGE PONDEZA AMWAGA MAMILIONI  UWT


Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Mhe. Ussi Salum Pondeza amechangia shilingi milioni tano kwa Umoja wa Wananake  UWT CCM Wilaya ya Amani kichama na Milioni tano kwa Wilaya ya Mjini Kichama ili kusaidia kuendeleza miradi ya jumuiya hiyo hali itakayoondosha hali ya utegemezi.


Mbali na fedha hizo Pondeza pia amekabidhi vyarahani vinne vinne kwa wilaya hizo vitakavyochochea uzalishaji wa bidhaa zitakazoongeza uchumi wa jumuiya hiyo ndani ya Wilaya hizo.


🗓️  24 May 2025


📍 Kisonge Mnarani

Jumamosi, 24 Mei 2025

DKT. BITEKO AWATAKA WAZAZI KUVUMILIANA KUTUNZA FAMILIA ZAO


 DKT. BITEKO AWATAKA WAZAZI KUVUMILIANA KUTUNZA FAMILIA ZAO


📌 Asisitiza wazazi kutenga muda wa kuwa na watoto wao


📌 Asema familia imara ni msingi wa dunia imara


📌 Mashirika, Wadau wa Maendeleo waipongeza Serikali kuimarisha malezi ya watoto


📌 Zaidi ya kaya 15,000 zapata elimu ya malezi jumuishi na huduma za afya ngazi ya jamii


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa rai kwa wazazi nchini kuvumiliana na kushirikiana katika malezi ya watoto wao ambao ndio msingi wa familia yeyote na Taifa kwa ujumla. 


Dkt. Biteko ametoa rai hiyo Mei 24, 2025 jijini Mwanza wakati akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdory Mpango katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia yenye Kaulimbiu inayosema “ Mtoto ni Malezi: Msingi wa Familia Bora kwa Taifa Imara”


“ Mtoto ni zao la matokeo ya wazazi wawili, Naomba wazazi tuthamini kuwa mtoto ni mtu muhimu na anahitaji  kulelewa, jambo hili la kutolea watoto likiendelea tutakuwa na jamii isiyo na msingi imara wa familia,” amesema Dkt. Biteko.


Ameendelea kusema “ Na sisi tukumbuke kuwa tumefika hapa kwa kuwa wako wazazi walivumiliana na wakatulea katika familia, sisi tusiwe watu wa kutelekeza familia zetu, ni wajibu wa kila mmoja kujua kuwa familia ni msingi, tukijua kuwa kila mtu ana mapungufu hivyo tuvumiliane tulee familia zetu, ”


Dkt. Biteko amebainisha kuwa familia ikiimarika na dunia itaimarika hivyo wazazi watenge muda wa kuwa na familia zao ili kuwarithisha mila na tamaduni zao. Aidha, matokeo ya wazazi kushtakiana kwa watoto yanajenga chuki miongoni mwa watoto hata katika maisha yao ya baadaye.


Pia, ametoa rai kwa watoto kuwa watiifu kwa wazazi na walimu wao sambamba na kujifunza kwa bidii na kuishi kwa kufuata miongozo ya dini.


Katika kuadhimisha siku hiyo ya familia, Dkt. Biteko ametaja baadhi ya majukumu ya familia kuwa ni kutoa huduma ili kukidhi mahitaji ya watoto na familia, kusimamia malezi na makuzi mema ya watoto na kurithisha mila na tamaduni nzuri kwa watoto na familia kwa ujumla kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine.


Fauka ya hayo, amesema katika kuimarisha malezi bora kwa watoto chini ya miaka 8, Serikali kwa kushirikiana na Wadau imeandaa na inatekeleza Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kwa kipindi cha mwaka 2021/22 – 2025/26.


Programu ambayo inahakikisha kuwa watoto wanapata huduma stahiki na jumuishi za malezi kwa uwiano ulio sawa kuanzia mtoto anapokuwa tumboni mwa mama yake hadi anapofikisha umri wa miaka 8.  


Ametaja mafanikio ya programu hiyo kuwa ni kuwajengea uwezo walimu wa awali 12,000 kutoka Halmashauri 184 kwa kutoa elimu ya malezi chanya ya watoto, wakihudumia zaidi ya watoto 360,000, kujenga vituo vya kulelea watoto wadogo mchana 4,178, kutoa huduma za malezi na elimu ya awali kwa zaidi ya watoto 400,000. Aidha, vituo vya kijamii 206 vinavyomilikiwa na jamii yenyewe vimeanzishwa vikitoa huduma kwa watoto 11,675.


“ Katika kuimarisha huduma za kundi la watoto wa miaka 5 hadi 8, Serikali imejenga madarasa mapya ya awali 1,316 na kupatiwa vifaa vya kujifunzia. Pia, zaidi ya kaya 15,000 zimefikiwa na elimu ya malezi jumuishi na huduma za afya ngazi ya jamii wakipata huduma muhimu za afya, lishe, malezi yenye kuitikia hisia za mtoto, elimu ya awali na uchangamshi wa mtoto na ulinzi na usalama na mtoto,  amesititiza Dkt. Biteko


Aidha, Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine imetoa mafunzo kwa wataalamu zaidi ya 15,000 wakiwemo Walezi wa Vituo vya Kulelea Watoto Wadogo mchana, Wahudumu wa Afya, Waandishi wa Habari, na Maafisa wa Ustawi na Maendeleo ya Jamii katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.


Naye, Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amesema kuwa Maadhimisho hayo yanalenga  kutathmini nafasi ya familia katika malezi ya watoto ambao ndio msingi wa familia yeyote na Taifa kwa ujumla. Vilevile, malezi ya mtoto yanaanza mara tu mtoto anapozaliwa na Serikali inasisitiza baba na mama kuwa karibu na mtoto wakati huo.


“ Akina mama na akina baba washirikiane  kwa pamoja kulea watoto ili wawe na  malezi bora, wapate elimu na huduma zingine muhimu kwao,” amesema Mhe. Mwanaidi.


Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu amesema kupitia maadhimisho hayo wameandaa maazimio matano yanaloyenga kukuza malezi na makuzi ya mtoto ili kuimarisha familia.


Ametaja maazimio hayo kuwa ni kueneza vituo vya malezi na makuzi ya mtoto nchi nzima ili kila mtoto apate huduma jumuishi, lishe na kuwa na usalama wao pamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana na sekta binafsi.


Ameendelea kusema maazio hayo ni pamoja na kuimarisha huduma za  utambuzi ili watoto wapate huduma mapema na kukuza eneo la smart malezi kwa kuimarisha matumizi ya TEHAMA ili wazazi waweze kubadilishana  mawazo kwa kutumia TEHAMA na watoto kupata nafasi ya kukua vizuri.


“ Kukuza na kuimarisha ushirikiano na taasisi za dini na mila ili kuimarisha masuala ya malezi, makuzi na taasisi  ya familia na kuongeza idadi ya watoa huduma wenye uwezo ili waweze kuenea  nchi nzima,” amemalizia Dkt. Jingu.


Akitoa salamu za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Elizabeth Maganga amesema kuwa Mashirika hayo yameendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika malezi na makuzi ya mtoto nchini.


Amesema umri wa kisayansi wa kumlea mtoto ni mwaka 0 hadi 8 na kuwa ni kipindi kizuri cha kumsaidia mtoto kukua vizuri hivyo ni fursa kwa Taifa kuwekeza katika malezi ya mtoto.


Akitoa salamu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Laximi Bhawan amesema kuwa Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali katika kuweka mikakati ya kusaidia malezi ya watoto.


Aidha, pamoja na Maadhimisho hayo, Dkt. Biteko amezindua Miongozo ya Afua za Utekelezaji wa Malezi na Matunzo ya Watoto na Familia, Kutambua Mchango wa Wadau kwenye Malezi na Ustawi wa Familia na Kuzindua Kampeni ya Malezi kwa Mtoto.

TASACO YAPOKEA MSAADA KUTOKA KWA MH. JERRY SILAA


 Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia na Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mh .Jerry Silaa ametoa Shilingi Millioni 1na laki 7 kwa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayohudumia jamii kwa kutoa Elimu ya huduma ndogo za kifedha (TASACO) ili kusaidia kikundi hicho Katika huduma wanayoitoa ya kukodisha,viti maturubai na vyombo kwenye shughuli mbalimbali.


Mh.Silaa ametoa Viti hivyo  Mei 23, 2025  siku ya Uzinduzi wa Taasisi hiyo  iliyopo katika Jimbo la Ukonga,Wilaya ya Ilala Jijini Dar es salaa ambapo amesema Viti hivyo vitawasaidia katika majukumu ya Kijamii na pale mtu atakapo pata tatizo.

Mh.ametoa wito kwa Viongozi wa Jimbo la Ukonga kuwakimbilia wananchi pindi wapatapo Changamoto kwasababu Mwananchi akipata Changamoto haangalii kama una pesa ila Imani Yako na kujitoa kwako wakati wa matatizo.


Aidha Mh.Silaa amewaasa Wanachama wa TaSaCo kutumia njia nzuri wa utunzaji wa Fedha ili kujihakikishia usalama wake huku akitolea Mfano kuwa mwanadamu Kila siku anachangamoto na wakati wowote anaweza akajikopesha Fedha za Taasisi na baadae akashindwa kuzirudisha.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa TaSaCo hiyo Paul Chegere amesema kuwa wao kama Taasisi wanaamini kuwa maisha yao yameunganishwa na umoja ili kujiwekea akiba na kukopeshana hatimaye kuleta maendeleo binafsi,kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa tumqini lao limejikita kwenye fursa na uwezeashaji ili kizifikia fursa hizo kwa kujikwamua kiuchumi huku hatma yao ukiwa imefungamana na uwepo wa Taasisi mbalimbali zenye kutoa huduma rafikiza binafsi na Serikali kama vile Benki ,Bima za afya na nyinginezo.


Kadhalika amesema lengo na natamanio yao ni kwamba  wajasiriamali ambao hawako kwenye mifumo rasmi ya ajira ni kujiunga na bima za afya na kupata Matibabu kwa gharama nafuu.



TaSaCo ni Taasisi inayojumishwa na vikundi vya ujasiriamali vya kuweka na kukopa(vicoba) ambayo idadi yake inafikia 57,huku ukiwa na Wanachama 510 ambao wengi wamenufaika,wamefanikisha kuendesha maisha yao pamoja na kuinuka kiuchumi.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan awaapisha Tumain Joseph na John MgettaIkulu Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2025.

 


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Prof. Tumaini Joseph Nagu kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia masuala ya Afya kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 24 May 2025.


Kadharika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Jaji Mstaafu John Samweli Mgetta kuwa Mjumbe wa Baraza la Maadili kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2025.

WANANCHI LINDI WATAKIWA KUCHAMKIA FURSA ZA MADINI

Wananchi Lindi watakiwa kuchangamkia fursa za madini


· *Waaswa kuacha uvivu*


· *Mgodi wa Elianje, injini ya maendeleo Namungo*


WANANCHI wa Mkoa wa Lindi wametakiwa kuacha uvivu na badala yake wachangamkie fursa zilizopo kwenye sekta ya  madini hususani katika mgodi wa kati  wa Elianje uliopo kitongoji cha Namungo, Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.


Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti  wa  Kijiji  cha  Chingumbwa, kilichopo Kata ya Namungo, Abdallah Rashid akielezea fursa zilizopo mkoani humo kupitia Sekta ya Madini.

“Fursa zipo nyingi ni uvivu tu wa wananchi wetu, ukiangalia kwenye mgodi huu unaotuzunguka wa Elianje Genesis kuna fursa ya usambazaji vyakula, vinywaji, usafi, kupika, kusambaza vifaa vya usalama migodini, uchimbaji na uchenjuaji lakini ndio hivyo,”amesema Abdallah


Aidha, Mwenyekiti huyo amesema uwepo wa mgodi huo umetoa manufaa makubwa kwa wananchi kwa kuchimbiwa kisima cha maji ambacho kwa sasa kinahudumia kaya 918, awali kulikuwa na shida ya maji na wananchi walilazimika kutembea umbali mrefu kuchota maji.

“Pia, mwekezaji ametujengea shule ambayo kwa sasa ina wanafunzi 79, awali watoto walitembea umbali mrefu zaidi ya kilomita tatu kufuata shule vijiji vya jirani hali iliyopelekea baadhi yao kuacha shule. Pia mwekezaji amekua akitoa chakula kwa wanafunzi kipindi cha mitihani, kuwaletea vifaa vya michezo vya mpira  wa miguu kwa wanaume na netball kwa  wanawake na yupo mbioni kununua basi la shule,”amesema.

Kwa upande wa Mkuu wa shule ya msingi Chingumbwa iliyopo kata ya Mbekenyela mkoani humo, Joseph Raymond amesema mgodi wa Elianje umejenga ofisi za Walimu, kuwawekea umeme  kwa ajili ya kambi kwa darasa la saba na la nne itakayoanza mwenzi ujao wa sita  wakijiandaa na mitihani ya taifa.



Naye, Meneja wa Mgodi wa Elianje, Philibert Masawe akizungumzia mgodi huo amesema wanajishughulisha na  uchenjuaji wa madini ya dhahabu na uchimbaji wa ‘green garnet’,


Amesisitiza pia Kampuni ya Elianje imejenga  kituo cha mfano cha uchenjuaji wa madini ya dhahabu kinachotumia teknolojia ya CIP ambacho kina uwezo wa wa kuchenjua mbale (mwamba) ya dhahabu kiasi cha tani 500 kwa siku.

Amesema pia kiwanda hicho kimeajiri watanzania 300 na kuipongeza Serikali kuweka sera rafiki na sheria nzuri ambazo zinavutia uwekezaji.

 

MADINI YA ALMASI YENYE THAMANI YA TSH 1.7 BILIONI YAKAMATWA YAKITOROSHWA UWANJA WA NDEGE MWANZA


 

MADINI YA ALMASI YENYE THAMANI YA TSH 1.7 BILIONI YAKAMATWA YAKITOROSHWA UWANJA WA NDEGE MWANZA


▪️Waziri Mavunde awapongeza RC Mtanda,Kamati ya Usalama,Uwanja wa Ndege na Kikosi kazi Madini


▪️Aelekeza uchunguzi zaidi kubaini mtandao wote wa wahusika


▪️Atoa rai kwa wadau wa madini kuzingatia sheria ya biashara ya madini nchini


▪️Raia wa Kigeni mwenye asili ya India ashikiliwa 



*Mwanza*


Madini ya almasi yenye thamani ya zaidi ya Sh1.7 bilioni yamekamatwa yakitoroshwa kupitia Uwanja wa ndege wa Mwanza.


Akizungumza na waandishi wa habari ljumaa usiku,Mei 23, 2025, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema madini hayo yalikamatwa Mei 18, 2025 kwa ushirikiano kati ya vyombo vya ulinzi na taasisi mbalimbali za Serikali na kutumia fursa hiyo kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Said Mtanda,Vyombo vya usalama,uongozi wa uwanja wa Ndege wa Mwanza na Kikosi Kazi cha Wizara ya Madini kwa kazi kubwa na ya kizalendo ambayo wameifanya.


“Mtu mmoja raia wa kigeni ambaye ana asili ya India , anashikiliwa kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani uchunguzi na taratibu

Katika tukio hilo,almasi ghafi yenye uzito wa karati 2,729.82 na thamani ya takriban USD 635,887.66 (sawa na Shilingi za Kitanzania 1,715,434,129.67) yaligunduliwa yakiwa yamefichwa kwenye mabegi manne na raia mmoja mwenye asili ya India kwa lengo la kuyasafirisha bila vibali halali wala kufuata taratibu za kisheria.


Nitoe rai kwa wadau wote wa Sekta ya Madini nchini kuhakikisha wanafuata sheria ya biashara ya madini nchini Tanzania ili wasipate hasara kwa kupoteza madini hayo ambayo hutaifishwa na serikali” Alisema Mavunde

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Saidi Mtanda amesema Mkoa wa Mwanza unaendelea kuimarisha ulinzi na udhibiti wa biashara zote haramu ili kuhakikisha nchi yetu ya Tanzania inanufaika na rasilimali madini.

UKAGUZI WA MALEZI YA WATOTO MADARASANI NA VITUO VYA MCHANA WAPASWA KUFANYIKA.


Mamlaka za serikali za mitaa  watakiwa kufanya  Ukaguzi wa Malezi ya Watoto Madarasani na Vituo vya Mchana


 OR-TAMISEMI


Maafisa elimu, ustawi wa jamii na lishe katika mamlaka za serikali za mitaa wametakiwa kufanya ziara za mara kwa mara za ukaguzi na ufuatiliaji wa malezi na makuzi ya watoto katika madarasa ya awali na vituo vya kulelea watoto mchana, ili kuhakikisha viwango vya mafunzo vinazingatia miongozo rasmi ya serikali.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Elimu anayeshughulikia Elimu ya Msingi kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Bi. Suzan Nussu, wakati wa mkutano wa siku mbili wa tathmini ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) uliofanyika jijini Mwanza.

Bi. Suzan alisisitiza kuwa jamii imara hujengwa tangu mtoto akiwa mdogo, hivyo ni muhimu kwa taasisi zote zinazohusika kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha watoto wanalelewa katika mazingira bora na salama, wakifundishwa kwa kuzingatia miongozo ya kitaifa inayolenga kuandaa msingi thabiti wa maendeleo yao ya baadaye.

MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI


Na. James K. Mwanamyoto OR-TAMISEMI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Maafisa Habari  Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Seriksali za Mitaa kuhakikisha wananchi wanapata habari sahihi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yao ya kazi.


Waziri Mchengerwa ametoa wito huo leo, wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Habari wa Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi za Ofisi ya Rais-TAMISEMI kinachofanyika katika Ukumbi wa Jiji la Dodoma uliopo kwenye Mji wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma.


“Mmebeba dhamana kubwa ya kuhakikisha wananchi wanapata habari sahihi hivyo msiwaache watanzania walishwe habari potofu” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.


Mhe. Mchengerwa amesema kuwa, Maafisa Habari nchini ni rasilimaliwatu muhimu hivyo wakitambua wajibu wao na kujiimarisha kiutendaji ni wazi kuwa wananchi watapata taarifa sahihi kwa wakati.


“Iwapo kila mmoja wenu akiwa mzalendo na kutambua wajibu wake, habari mtakazozitoa ndio zitaaminiwa na kupokelewa na watanzania kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ambayo imeshamiri hivisasa,” Waziri Mchengerwa amehimiza.


Waziri mchengerwa amesema, ana amini kwamba maafisa habari waliopo wana weledi na ujuzi unaowawezesha kutoa taarifa sahihi zenye tija kwa wananchi na maendeleo ya taifa kwa ujumla.


Sanjari na hilo, Waziri Mchengerwa ameelekeza Maafisa Habari wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa washiriki kwenye ziara za viongozi ili wapate uelewa utakaowawezesha kutangaza kwa ufanisi mafanikio ya Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.


Aidha, Waziri Mchengerwa amewaelekeza waajiri katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha Maafisa Habari wanaokaimu ukuu wa vitengo ambao wana sifa, wapewe vitengo ili waweze kutekeleza kikamilifu jukumu la kuuhabarisha umma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya taasisi zao ikiwa ni pamoja na kutangaza mafanikio yaliyopatikana kwenye eneo la utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambalo limepewa kipaumbele na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 

KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA WASIOONA NA KUJADILI MASUALA YA MAENDELEO, CHANGAMOTO NA UWEZESHAJI WAO.


 KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA WASIOONA NA KUJADILI MASUALA YA MAENDELEO, CHANGAMOTO NA UWEZESHAJI WAO.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu- Mhe. Ridhiwani Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Halmashauri kuu ya Chama cha wasioona Tanzania (TLB) ambao pia ni wenyeviti wa Mikoa wakiongozwa na Marco Mashauri Mwenyekiti wa chama cha wasioona mkoa wa Shinyanga, Yohana Mwoga kutoka Mbeya, Fred Fred Mwankosole kutoka Kilimanjaro na Pascal Msigwa kutoka Njombe.

Kikao hicho kimefanyika leo Mei 23, 2025 katika Ofisi ya Mhe. Ridhiwani Kikwete jijini Dodoma na kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo, changamoto na uwezeshaji wa watu wasioona Tanzania.





Ijumaa, 23 Mei 2025

𝗡𝗔𝗜𝗕𝗨 𝗪𝗔𝗭𝗜𝗥𝗜 𝗔𝗞𝗔𝗚𝗨𝗔 𝗠𝗜𝗡𝗔𝗥𝗔 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗪𝗔𝗦𝗜𝗟𝗜𝗔𝗡𝗢 𝗞𝗜𝗕𝗔𝗛𝗔


 𝗡𝗔𝗜𝗕𝗨 𝗪𝗔𝗭𝗜𝗥𝗜 𝗔𝗞𝗔𝗚𝗨𝗔 𝗠𝗜𝗡𝗔𝗥𝗔 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗪𝗔𝗦𝗜𝗟𝗜𝗔𝗡𝗢 𝗞𝗜𝗕𝗔𝗛𝗔


Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi, ameanza ziara ya kikazi leo Mei 23, 2025, kwa ajili ya kukagua ujenzi wa minara ya mawasiliano katika Jimbo la Kibaha Vijijini, Mkoa wa Pwani.

Akizungumza wakati wa mapokezi yake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, amesema mkoa huo una maeneo 27 makubwa ya uwekezaji wa viwanda, na ameiomba Wizara kuhamasisha wadau wa sekta binafsi kuwekeza katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa.

Kwa upande wake, Mhandisi Mahundi amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ina dhamira thabiti ya kuhakikisha maendeleo ya kidijitali yanafikiwa nchini kote. Ameahidi kuwa Wizara itaendelea kuchukua hatua madhubuti kushughulikia changamoto za mawasiliano katika Mkoa wa Pwani kwa suluhisho la kudumu.

Listen Mkisi Radio