JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Jumatano, 4 Juni 2025

KAMPUNI YA KIZALENDO (MOFAT) YAULA MABASI YA ENDAYO HARAKA (BRT)


 Na Mwandishi wetu 


KAMPUNI ya Kizalendo ya Mofat imepewa mkataba wa miaka 12 na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Dart) kwa ajili ya kuendesha Awamu ya Pili ya mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT), unaotoka Gerezani hadi Mbagala. 


Kampuni hiyo ya Kizalendo ya Mofat inatarajiwa kuanza kutumia mabasi 255 yanayotumia gesi ifikapo Agosti 2025.

Akizungumza hayo hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji wa Dart, Dkt. Athuman Kihamia, alithibitisha kuhusu mkataba huo jana katika mahojiano ya simu akiwa nje ya nchi.


Alisema maendeleo yanakuja wakati serikali ikihamia rasmi katika kuhamisha uendeshaji wa awamu ya kwanza na ya pili ya mfumo wa BRT kwa sekta binafsi, ikiwa ni juhudi za kuongeza ufanisi na kushughulikia changamoto za muda mrefu za usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

''Hii ni kampuni ya kizalendo na tayari imepata mitaji na dhamana zinazohitajika kuendesha huduma hii.


"Hivyo hii ni hatua kubwa katika juhudi zetu za kutoa huduma za usafiri wa uhakika na bora kwa wakazi wa jiji. Kampuni hiyo imejitolea kuleta mabasi ndani ya muda tuliokubaliana,"alisema Dkt. Kihamia.

Mwelekeo wa kuwashirikisha zaidi waendeshaji wa ndani ulisisitizwa pia Jumatatu na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, aliyewaambia wahariri jijini Dar es Salaam kuwa Dart sasa inalenga kuvutia wawekezaji zaidi—hasa kwa kuwa ujenzi wa Awamu ya Kwanza na ya Pili umekamilika, huku Awamu ya Tatu ikitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.


Kwa mujibu wa mfumo mpya, mfumo wa BRT utaendeshwa na kampuni kati ya nne hadi sita, badala ya mfumo wa sasa wa mtoa huduma mmoja unaoongozwa na UDA Rapid Transit (Udart).

0 comments:

Chapisha Maoni

Listen Mkisi Radio