Mamlaka za serikali za mitaa watakiwa kufanya Ukaguzi wa Malezi ya Watoto Madarasani na Vituo vya Mchana
OR-TAMISEMI
Maafisa elimu, ustawi wa jamii na lishe katika mamlaka za serikali za mitaa wametakiwa kufanya ziara za mara kwa mara za ukaguzi na ufuatiliaji wa malezi na makuzi ya watoto katika madarasa ya awali na vituo vya kulelea watoto mchana, ili kuhakikisha viwango vya mafunzo vinazingatia miongozo rasmi ya serikali.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Elimu anayeshughulikia Elimu ya Msingi kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Bi. Suzan Nussu, wakati wa mkutano wa siku mbili wa tathmini ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) uliofanyika jijini Mwanza.
Bi. Suzan alisisitiza kuwa jamii imara hujengwa tangu mtoto akiwa mdogo, hivyo ni muhimu kwa taasisi zote zinazohusika kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha watoto wanalelewa katika mazingira bora na salama, wakifundishwa kwa kuzingatia miongozo ya kitaifa inayolenga kuandaa msingi thabiti wa maendeleo yao ya baadaye.
0 comments:
Chapisha Maoni