Header Ads Widget

Responsive Advertisement

RAIS MWINYI:ZNZ ITAIMARISHA USHIRIKIANO WAKE NA CUBA KWA MAENDELEO.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar Ina Kila sababu ya Kuimarisha Ushirikiano na Cuba kutokana na Mchango  unaotolewa na Nchi hiyo kwa Maendeleo ya Zanzibar 


Rais Dkt, Mwinyi amesema hayo alipozungumza  na  Rais wa Baraza la Taifa na  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Cuba Esteban Lazo Hernandez na Ujumbe wake Waliofika Ikulu Zanzibar 



Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameishukuru Cuba kwa Misaada inayoendelea  kuitoa kwa Zanzibar kwani imekua ikichangia kwa Kiasi kikubwa  Maendeleo katika Sekta tofauti  Hususan Sekta ya Afya na Kuimarisha Ustawi wa  Wananchi wa Zanzibar.


Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amesema Ujio wa Ujumbe huo ni fursa Muhimu ya kufungua maeneo Mengine ya Ushirikiano  ikiwemo Uchumi wa Buluu, Elimu, Utalii , Teknolojia  ,Utamaduni ,Michezo .


Naye , Rais wa Baraza la Taifa na Spika wa Bunge  la Jamhuri ya  Cuba Esteban Lazo Hernandez ameihakikishia Zanzibar  Kuendelea na Ushirikiano  na Kupongeza Mabadiliko Makubwa yaliofikiwa na Zanzibar Katika  Ujenzi wa Viwanja vya Ndege , Miundonbinu ya Barabara ,  Hospitali na Vituo vya Afya hapa nchini.

Post a Comment

0 Comments