Na Hamis Dambaya, Osaka-Japan
Tanzania imeendelea kuvutia watazamaji wengi wa kimataifa katika maonesho ya Expo 2025 yaliyoanza tarehe 13 aprili, 2025 katika Jiji la Osaka nchini Japan.
Katika maonesho hayo Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania Bwana Ernest Mwamwaja amesema kuwa tangu wiki ya utalii iliponza banda la Tanzania limekuwa limekuwa kivutio na kupokea wageni wengi wanaotembelea na kutaka kujua fursa vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji kwenye maeneo ya utalii yaliyopo Tanzania.
Bwana Mwamwaja amesema kuwa Tanzania itatumia maonesho hayo makubwa duniani pamoja na kupokea watembeleaji na kuwapa maelezo kuhusu fursa zilizopo Tanzania na kushiriki mijadala ya kimkakati yenye lengo la kuvutia wageni kutembelea Tanzania.
Amesema kuwa Tanzania imekuwa ikitumia fursa ya Maonesho hayo ya kimataifa kuelezea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo kama mbuga za Wanyama zikiwepo Ngorongoro, Serengeti,Manyara, Mikumi, Mlima Kilimanjaro na maeneo ya fukwe ikiwemo zilizopo Zanzibar.
Kwa upande wake Afisa Utalii Mkuu,masoko kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Bwana Michael Makombe amesema watembeleaji wengi katika maonesho hayo wamekuwa wakijifunza kuhusu namna Tanzania ilivyofanikiwa kuimarisha uhifadhi wa wanyama pori.
Maonesho ya mwaka huu yanakadiriwa kutembelewa na watazamaji zaidi ya milioni 26 yakihusisha waoneshaji kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Tags
Top Stories.