Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewanasihi Wananchi wa Tanzania kuendelea kudumisha umoja, mshikamano na amani kwa mustakabali mwema wa Taifa kwa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo na kujiepusha na matendo yanayoweza kuleta mgawanyiko.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipofungua Dua Maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Mamufti, Masheikh, na Waislamu waliotangulia mbele ya haki iliofanyika katika Msikiti wa Mohamed VI-Bakwata Makao Makuu, Kinondoni Jijini Dar es Salaam tarehe 8 Mei 2025.
Aidha , Rais Dkt.Mwinyi amewapongeza Uongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kuendeleza utaratibu wa Dua ya kila Mwaka na kuiombea nchi amani .
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa amani ina umuhimu mkubwa katika Uchaguzi Mkuu Mwaka huu kabla , wakati na baada ya Uchaguzi huo.
Rais Dkt.Mwinyi amesema jukumu la kuwaombea Dua Masheikh, Walimu, na Waislamu waliohai na waliotangulia mbele ya haki na kuiombea amani Nchi ni miongoni mwa dalili za imani ya kweli kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu kwa mikusanyiko yenye kheri kwa mustakabali wa Taifa.
0 comments:
Post a Comment