Meya Kumbilamoto akizungumza na Viongozi wa Wafanyabiashara wa Machinjio ya Vingunguti ,kikao hiki kilikuwa cha kufafanua Uvumi na Uzushi Uongo ulioleta hofu na Taharuki kwa wachinjaji na wafanyabiashara wa machinjio ya Vingunguti
Uvumi huo ni kuwa eti Machinjio ya Vingunguti imeuzwa kwa Mwekezaji na wafanyabiashara wataondolewa kuchinja mle ndani watapelekwa Pugu ktk ufafanuzi wake Mh Meya ni kuwataka wafanyabiashara kupuuza Mbuli Kumlomo za walimwengu waendelee na biashara zao km kawaida huku serikali ya Mh
Rais Dkt Samia ikiendelea kulinda ajira zao na kuboresha biashara zao , wenyeji wa Dar wa Salaam Mtakumbuka kulikuwa na uvumi miaka ya 1990 pale kituo cha polisi buguruni Mtu kageuka CHATU kumbe ni uzushi
Upatapo taarifa hii mjulishe na mwenzio kupuuza upuzi huu Safari ya kuifanya Vingunguti kuwa Mji unaovutia kama Istanbul au Brunei inaendelea tutaendelea kuwapiga Spana Mbuli Kumlomo wote
Kazi Utu Tunasongambele mimi Mtumishi wenu Kumbilamoto .