Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Temeke, Holle Makungu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa taarifa ya utendaji wa kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2025.
Wanahabari na maafisa TAKUKURU walioshiriki kwenye mkutano wa Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Temeke, Holle Makungu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa taarifa ya utendaji wa kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2025.
..........
NA MUSSA KHALID
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Temeke imewafikisha mahakamani watuhumiwa kumi na wawili kwa mashtaka ya uhujumu uchumi,Ubadhirifu na Utakatishaji fedha kiasi cha zaidi ya milioni 165.14
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa TAKUKURU (M)Temeke,Holle Makungu wakati akizungumza na wananahabari akitoa taarifa ya kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu ambapo amesema mashtaka hayo yamefunguliwa katika mahakama ya Wilaya Kigamboni.
Mkuu huyo wa TAKUKURU
Temeke amewataja baadhi ya washtakiwa hao kuwa ni pamoja na Annie Nyabugumba
Maugo ambaye ni Afisa Hesabu(Ofisi ya Rais TAMISEMI)Tumsifu Christopher
Kachira,(afisa mwandamizi OR-TAMISEMI) na Aidani Zabron Mponzi (Ofisa hesabu
OR-TAMISEMI).
Wengine ni Jonathan
Stanley Manguli (aliyekuwa Afisa hesabu OR TAMISEMI),Godrey James
Martiny(aliyekuwa mkuu wa kitengo cha Fedha na Uhasibu),Juvenalis Mauna(Mkuu wa
kitengo cha udhibiti taka na Usafi wa Mazingira),Josephat
Mtembei(Mhandisi),Bibiana Mdete (Mtunza Bohari)na Henry Herman(Afisa
Ugavi).
Mbali na Watendaji hao wapo pia wakandarasi walioshatakiwa katika kesi hiyo ni Hamis Kashinje Manfred,Paulo Sam Mwakyusa na Godwin Adamson Cheyo ambao kampuni zao zinatumika kutakatisha fedha hizo.
Aidha,Makungu,amesema kwa mujibu wa hati ya mashtaka,makosa wanayoshtakiwa nayo ni kusababisha hasara kinyume cha kifungu cha 10(1) cha jedwali la kwanza na kifungu cha 57 na 60(2) cha sheria ya Uhujumu Uchumi sura ya 200 mapitio ya 2022,kosa la utakatishaji fedha k/f cha 12(1)(a) na 13(1) (a) cha Sheria ya utakatishaji fedha sura 423 ya mapitio 2022,ubadhirifu kinyume na k/f cha 28(2) cha Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa sura ya 329.
Aidha Makungu,amesema washtakiwa hao wamepelekwa mahabusu kwa kuwa makosa yao hayana dhamana hadi kesi yao itakapokuja tena mahakamani hapo tarehe 12/6/2025 kwa ajili ya kutajawa.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, watuhumiwa wanakabiliwa na kosa la kusababisha hasara, kinyume na kifungu cha 10(1) cha Jedwali la Kwanza pamoja na vifungu vya 57 na 60(2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi, Sura ya 200 (Marejeo ya 2022).
Kosa la utakatishaji fedha, kinyume na vifungu vya 12(1)(a) na 13(1)(a) vya Sheria ya Utakatishaji Fedha, Sura ya 423 (Marejeo ya 2022) pamoja na kosa la ubadhirifu, kinyume na kifungu cha 28(2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sura ya 329
Katika hatua nyingine,TAKUKURU mkoa wa Temeke imefuatili miradi 13 yenye thamani ya TZS zaidi Bilioni 11,ambapo kati ya miradi 13 miradi mitano (5) ilitolewa ushauri wa kurekebisha mapungufu yaliyobainika.
Hata hivyo Taasisi hiyo imetaja mikakati yake kwa kipindi cha April mpaka Juni mwaka huu kuwa ni kuimarisha juhudi za kuzuia rushwa kwa kuongeza ushiriki wa kila mwananchi na wadau mbalimbali katika kukabili tatizo la rushwa hasa katika uchaguzi wa viongozi wa kisiasa unaotarajiwa kufanyika kwa mwaka.
pIA TAKUKURU inaendelea kuelimisha jamii kwa njia mbalimbali, zikiwemo kuimarisha klabu za wapinga rushwa katika shule za msingi, sekondari, na vyuo, kufanya mikutano ya hadhara na semina, kushiriki maonesho mbalimbali pamoja na kurusha vipindi vya televisheni na redio
0 comments:
Chapisha Maoni