JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ijumaa, 13 Juni 2025

STAMICO YAFANYA MAFUNZO YA UZALISHAJI BORA WA CHUMVI LINDI NA MTWARA

.............

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kushirikiana na Chama cha Wazalishaji wa Chumvi Tanzania (TASPA) limeendesha Mafunzo ya Kimkakati kwa Wazalishaji wa Chumvi kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara. 

Mafunzo haya yamefanyika Ruangwa Mkoani Lindi Leo tarehe 12 Juni 2025 ambapo Mgeni Rasmi kwenye Ufunguzi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye aliwakilishwa na Mhe. Victoria Mwanziva Mkuu wa Wilaya ya Lindi.

Katika hotuba yake ya ufunguzi DC Mwanziva aliwapongeza STAMICO kwa kuendesha Mafunzo haya hasa katika kipindi hiki cha Maonesho ya Madini kwani mwitikio umekuwa mkubwa sana. 

Kwa kuwa Wazalishaji wa chumvi wanazo changamoto zao , kupitia Mafunzo haya Watalaam kutoka STAMICO na Wizara ya Madini changamoto hizo zitapatiwa ufumbuzi. 

Akiwasilisha Neno kwa Niaba ya STAMICO, Bw. Denis Silas Mjiolojia alieleza uwepo wa fursa mbalimbali ambazo Shirika linawaletea wachimbaji wa madini. 

Fursa hizo ni Ujenzi wa Kiwanda cha Kusafisha chumvi (salt refinery plant) kinachojengwa eneo la Lingaula Kilwa Mkoani Lindi ambacho ni fursa la soko la uwakika kwa Wazalishaji wa chumvi mikoa ya Kusini.

Fursa nyingine ni Mafunzo haya yanayofanyika kwa Wazalishaji wa Chumvi. Mafunzo haya yanatolewa kwa lengo la kuboresha shughuli za uzalishaji wa chumvi ili kuleta tija kwa Wazalishaji na kuwaongezea Kipato sambamba na malengo ya Wizara ya Vision 2030 Madini ni Maisha na Utajiri. 

Fursa hizi pia zimetangazwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika kwenye Ufunguzi wa Maonesho ya Madini Lindi tarehe 11 Juni 2025.

Akiwasilisha changamoto za Wazalishaji wa chumvi Ndg. Ally Khaify - Mhazini wa Chama cha Wazalishaji wa Chumvi -TASPA alisema changamoto kubwa ya wanayokumbana nayo ni ukosefu wa soko la uhakika. 

Na changamoto hii inapata suluhisho kwa ujenzi wa kiwanda unaofanywa na STAMICO Kilwa.  Hivyo TASPA wanampongeza MD Kwa STAMICO kwa Kiwanda hiki ambacho kitaanza kazi Agosti 2025. 

Katika Mafunzo haya Mada mbalimbali zilitolewa kutoka TASPA, STAMICO na Tume ya Madini. 

Wengine walishiriki ni benki ya NBC,NMB , CRDB,Kiwanda cha Neelkant, Jitegemee, Wizara ya Madini, Ofisi ya Madini- Mtwara

0 comments:

Chapisha Maoni

Listen Mkisi Radio