JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Jumatano, 2 Julai 2025

ETDCO YAONYESHA UTEKELEZAJI WA MRADI YA UMEME SABASABA

Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO) Mustapha Himba (kulia) akitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa miradi ya umeme kwa wananachi waliotembelea leo julai 2, 2025 katika banda la Kampuni hiyo katika  Maonesho  ya 49 ya Kimataifa ya Biashara sabasaba  katika Viwanja vya  Julius Nyerere, Dar es Salaam Afisa Uhusiano wa Kampuni ya ETDCO Bi. Samia Chande (kulia) akitoa maelezo ya utekelezaji wa miradi ya umeme kwa mwananachi aliyetembelea leo julai 2, 2025 katika banda la Kampuni hiyo katika  Maonesho  ya 49 ya Kimataifa ya Biashara sabasaba  katika Viwanja vya  Julius Nyerere, Dar es Salaam .

Wafanyakazi wa Kampuni ya ETDCO wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda la kampuni hiyo,  maonesho ya sabasaba.

..........

Wananchi wamehimizwa kutembelea banda la Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO), katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba, ili kuona namna Serikali ilivyowekeza katika kuboresha miundombinu ya umeme kwa lengo la kuhakikisha Watanzania wanapata umeme wa uhakika kwa maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza leo Julai 2, 2025, jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Maonesho ya Julius Nyerere, Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya ETDCO, Mustapha Himba, amesema kuwa katika utekelezaji wa miradi ya umeme nchini, wamefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati kwa mafanikio makubwa, hali ambayo imeleta tija kwa jamii.

Mhandisi Himba amesema kuwa mojawapo ya miradi waliyotekeleza ni mradi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Mtwara hadi Maumbika yenye kilovolti 132, ikiwa na urefu wa kilomita 80, pamoja na mradi mwingine kutoka Tabora hadi Urambo wenye kilovolti 132 na urefu wa kilometa 115.

Aidha, ameeleza kuwa kuna mradi mwingine wa kutoka Tabora hadi Katavi wenye kilovolti 132, ambao umewezesha wananchi wa mkoa huo kupata huduma ya umeme wa uhakika.

"Tunawakaribisha wananchi wote kutembelea banda letu la ETDCO lililopo ndani ya banda la TANESCO. Lengo ni kuwaonesha wadau namna kampuni yetu inavyotekeleza majukumu yake kwa weledi mkubwa ili kuisaidia Serikali katika kuboresha huduma ya umeme," amesema Mhandisi Himba.

Ameongeza kuwa kampuni hiyo imefanikiwa kujenga miradi ya REA katika mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Arusha, Katavi, Mbeya, Geita, pamoja na Kigoma.

Amefafanua kuwa hadi sasa, katika utekelezaji wa miradi hiyo, wamejenga njia za usafirishaji umeme zenye kilovolti 132 kwa urefu wa kilomita 578, na usambazaji wa kilovolti 33/11 kwa urefu wa kilomita 4,483.

Aidha, wamefanya ukarabati wa miundombinu ya umeme yenye urefu wa kilomita 534, na kufanikiwa kuunganisha umeme katika vijiji 291 na vitongoji 105.

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi waliotembelea banda la ETDCO, akiwemo Bi. Fatuma Yusuph, wameipongeza kampuni hiyo kwa kutekeleza miradi hiyo kwa wakati, huku wakitoa wito kwa Serikali kuendelea kuboresha miundombinu ya umeme ili kuchochea shughuli mbalimbali za kiuchumi.

0 comments:

Chapisha Maoni

Listen Mkisi Radio