NA MUSSA KHALID
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya
nchini –DCEA inandelea kuwadhibiti baadhi ya wahalifu wa Dawa za kulevya ambao
wameanza kutumia maiti za Binadamu kubeba dawa hizo maarufu kwa jina la begi
ili kukosemsha uhalifu huo.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo Aretas Lyimo
amebainisha hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wanahabari akitoa
taarifa ya operesheni waliyoifanya kwa kipindi cha mwezi Mei hadi Julai mwaka
huu.
Kamishna Jenerali Lyimo amesema wamebaini kumekuwa
na matukio ya raia wa kigeni kuwatumia watanzania kusafirisha na kusambaza dawa
za kulevya kwa kutumia njia hizo hivyo amewasisitiza wananchi kuwa makini na
kuchukua tahadhari wanapotumwa au kupokea mizigo.
‘Mara niyingi huanzisha mahusiano ya kirafiki na
kisha kuwahusisha katika biashara hii haramu kwa kutumia kampuni zao na vyombo
vyao vya usafiri hususani bodaboda,bajaji,Tax na wasambazaji wa vifurushi’amesema
Kamisha Lyimo
Aidha Kamishna Jenerali Lyimo amesema katika
operesheni hizo pia wamekamata dawa za kulevya jumla ya Kilogram 37,197.142 na
watuhumiwa 64 waliohusishwa na dawa hizo.
Amesema kuwa Dawa hizo zinajumuisha kilogram
11,031.42 za dawa mpya za kulevya aina ya Mitragyna Speciosa,bangi kilogram
24,873.56,mirungi kg 1,274.47,skanka kg 13.42,heroin kg 2.21 na methamphetamine
gramu 1.42.
Ameendelea kueleza kuwa katia ukamataji huo
umehusisha dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya ketamine kilogramu
1.92,Fluni-trazepam vidonge 1000,lita 6 za kemikali bashirifu aina ya
hydrochloric acid na uteketezaji wa ekari 1,045.5 za mashamba ya bangi.
Kamishna Lyimo amesema katika mkoa wa Dar es salaam eneo
la Sinza waliwakamata watu wawili wamiliki wa kiwanda bubu kinachotengeneza
biskuti zinazochanganywa na bangi kisha kuzisambaza katika mikoa ya Dar es
salaam,Mwanza,Lindi na Mtwara amba pia wakati huohuo mkoani Lindi alikamatwa
mfanyabiashara wa madini akisambamba biskuti zilizochanganywa na bangi.
‘Vilevile kwa upande wa dawa za kulevya za mashambani zilikamatwa jumla ya Kilogram 26,191.45 za bangi,mirungi,skanka na kuteketeza akari 1,045.5 za mashamba ya bangi katika mikoa ya Ruvuma,Mbeya,Mara,Kagera,Dodoma,Tabora,Morogoro na Arusha.
Hata hivyo Mamlaka hiyo imetoa tahadhari kwa mtu yeyote atakayeendelea kujihudisha na biashara,usambazaji na uzalishaji wa Dawa za Kulevya kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria pindi atakapobainika.
0 comments:
Chapisha Maoni