Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibi wa Mbolea Tanzania –(TFRA) Joel Laurent akimsikiliza Afisa Udhibiti ubora Mwandamizi kutoka katika Mamlaka hiyo Azizi Mtambo alipotembelea banda la Mamlaka hiyo katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya biashara 'Sabasaba' yanayoendelea jijini Dar es salaam leo tar 10/7/2025.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibi wa Mbolea Tanzania –(TFRA) Joel Laurent (kushoto) akimsikiliza Meneja wa Uhusiano, Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa TFRA, Bi. Matilda Kasanga (kulia) alipotembelea banda la Mamlaka hiyo katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya biashara 'Sabasaba' yanayoendelea jijini Dar es salaam leo tar 10/7/2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibi wa Mbolea Tanzania –(TFRA) Joel Laurent akimsikiliza Afisa kutoka TARI alipotembelea Banda la Taasisi hiyo katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya biashara 'Sabasaba' yanayoendelea jijini Dar es salaam leo tar 10/7/2025
.............................
NA MUSSA KHALID
Mamlaka ya Udhibi wa Mbolea Tanzania –TFRA imewasisitiza watanzania kutumia fursa ya uwepo wa maabara ya kisasa iliyoanzishwa na Mamlaka hiyo ili kujua afya ya udongo na ubora wa mbolea kuwa katika kiwango sahihi.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA Joel Laurent wakati alipotembelea banda la Mamlaka hiyo katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya biashara 'Sabasaba' yanayoendelea jijini Dar es salaam ambapo amesema ni vyema wakaondoa wasiwasi kwani maabara hiyo inakwenda kuwasaidia katika shughuli zao za kilimo
Mkurugenzi huyo amesema kuwa lengo lao ni kuonyesha fursa zilizopo katika mnyororo wa thamani katika mbolea lakini pia kuwaelimisha watanzani namna ya kutumia matumizi sahihi ya mbolea.
Amesema mpaka kufika mwaka 2030 matumizi ya mbolea yatakuwa mara mbili ya kiwango cha sasa hivyo wameendelea kuyashawishi makampuni mbalimbali yaweze kuzalisha.
‘Mipango yetu ni kuendelea kuwa na mbolea sahihi kwa matumizi sahihi kwa wakulima wetu ambapo inatokana na wizara ya Kilimo kuendelea kupima afya ya udongo nchi nzima hivyo tunahitaji wenzetu wanaozalisha waweze kuagiza mbole ambazo zinaendana na afya ya udongo ili kuongeza tija’amesema Laurent
Aidha Laurent amesema kuwa Mamlaka hiyo imeanzisha mfumo wa kielekroniki ili wakulima waweze kujisajili jambo litakalosaidia wapate manufaa ya mbolea kwa bei himilivu.
Mkurugenzi huyo wa TFRA pia amesema kwa mwaka huu wameandaa mpango maalum wa kuongeza uzalishaji wa mbolea kwa viwanda vya ndani kwa ajili ya wakulima ili ziweze kupatikana mapema,kwa urahisi na bei nafuu zaidi.
0 comments:
Chapisha Maoni